Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)

Maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Pelvic Inflamatory Diseases’ yaani P.I.D

P.I.D ni ugonjwa mpya katika jamii yetu na ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake.

Maambukizi haya huweza kuhusisha shingo ya uzazi, yanaweza kuwa pia kwenye nyama ya mfuko wa uzazi, na katika mirija ya uzazi.

NI NINI HASA HUSABABISHA P.I.D?

Huu ni ugonjwa wa unaotokana na bakteria wanaojulikana kwa kitaalamu bakteria wa jamii ya ‘Neisseria Gonorrhoeae’ na kundi lingine la bakteria hawa hujulikana kama ‘Chlamydia trachomatis’.

Makundi haya mawili ya bakteria ndiyo wanahusika kwa sehemu kubwa na ugonjwa huu wa P.I.D.

JE P.I.D HUAMBUKIZWAJE?

Zipo njia kadhaa ambazo wanawake wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa P.I.D.

Baadhi ya hizo njia ni pamoja na:

1. Kushiriki tendo la ndoa bila kinga 
2. Maambukizi katika njia ya uzazi baada ya kujifungua 
3. Kutoa ujauzito kwa njia zisizo salama 
4. Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
5. Kuwa na wapenzi wengi 
6. Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea vya PID hasa katika harakati za upasuaji nk.

Dalili za P.I.D

Wapo baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na ugonjwa huu na wasionyeshe dalili wala ishara zozote za kuwa nao.

Mwanamke akianza kuonyesha dalili za ugonjwa wa P.I.D anaweza:

1. Kuhisi maumivu ya tumbo hasa maumivu chini ya kitovu
2. Kutokewa na maumivu ya mgongo mara kwa mara
3. Kupata utoko mchafu sehemu za siri ambao huambatana na harufu mbaya kama shombo ya samaki
4. Kupata maumivu wakati wa kukojoa
5. Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kupata damu bila mpangilio akiwa kwenye siku zake
7. Kuwa na homa mara kwa mara
8. Kichefuchefu na
9. Kutapika

Dawa ya asili ya P.I.D

Kama utahitaji dozi kamili ya P.I.D niachie ujumbe WhatsApp +255714800175.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imesomwa mara 599

Imehaririwa

Categories: P.I.D

Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp Bonyeza HAPA tuchat WhatsApp