Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)

Maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Pelvic Inflamatory Diseases’ yaani P.I.D

P.I.D ni ugonjwa mpya katika jamii yetu na ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake.

Maambukizi haya huweza kuhusisha shingo ya uzazi, yanaweza kuwa pia kwenye nyama ya mfuko wa uzazi, na katika mirija ya uzazi.

NI NINI HASA HUSABABISHA P.I.D?

Huu ni ugonjwa wa unaotokana na bakteria wanaojulikana kwa kitaalamu bakteria wa jamii ya ‘Neisseria Gonorrhoeae’ na kundi lingine la bakteria hawa hujulikana kama ‘Chlamydia trachomatis’.

Makundi haya mawili ya bakteria ndiyo wanahusika kwa sehemu kubwa na ugonjwa huu wa P.I.D.

JE P.I.D HUAMBUKIZWAJE?

Zipo njia kadhaa ambazo wanawake wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa P.I.D.

Baadhi ya hizo njia ni pamoja na:

1. Kushiriki tendo la ndoa bila kinga 
2. Maambukizi katika njia ya uzazi baada ya kujifungua 
3. Kutoa ujauzito kwa njia zisizo salama 
4. Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
5. Kuwa na wapenzi wengi 
6. Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea vya PID hasa katika harakati za upasuaji nk.

Dalili za P.I.D

Wapo baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na ugonjwa huu na wasionyeshe dalili wala ishara zozote za kuwa nao.

Mwanamke akianza kuonyesha dalili za ugonjwa wa P.I.D anaweza:

1. Kuhisi maumivu ya tumbo hasa maumivu chini ya kitovu
2. Kutokewa na maumivu ya mgongo mara kwa mara
3. Kupata utoko mchafu sehemu za siri ambao huambatana na harufu mbaya kama shombo ya samaki
4. Kupata maumivu wakati wa kukojoa
5. Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kupata damu bila mpangilio akiwa kwenye siku zake
7. Kuwa na homa mara kwa mara
8. Kichefuchefu na
9. Kutapika

Dawa ya asili ya P.I.D > Mafuta ya mbegu za mlonge

Mafuta ya Mbegu za Mlonge

Ili kutibu aina yoyote ya maambukizi ya ndani ya mwili ambayo yanahusu bakteria, virusi au fangasi kunategemea sana na uimara na ubora wa kinga yako ya mwili.

Kinga yako ya mwili inajumuisha aina ya seli nyeupe maalumu ambazo hutafuta na kuua bakteria na vijidudu vingine nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa.

Kinga yako ya mwili inapokuwa ni dhaifu bakteria wabaya wanaweza kuongezeka na kujirundika mwilini na kusambaa mpaka kwenye via vya uzazi kwa njia ya damu.

Kwahiyo ili kutibu na kukinga P.I.D unahitaji kuwa na dawa ya uhakika ya kuboresha kinga yako ya mwili ifanye kazi kwa kiwango chake cha juu kabisa.

Mafuta ya mbegu za mlonge ni dawa ya kuimarisha kinga ya mwili nzuri kuliko dawa nyingine yoyote unaifahamu chini ya jua.

Kwanza kabisa mlonge umebarikiwa kuwa na viinilishe vingi zaidi kuliko mti mwingine wowote ukiwa na viinilishe 92 ndani yake, una vitamini nyingi, madini na viondoa sumu mwilini tofauti tofauti 46!

Huu ndiyo ukweli wa kustaajabisha wa mti huu unaoleta afya na maisha.

Mafuta ya mlonge yanaondoa sumu mwilini.

Vitamini C ipatikanayo katika mafuta ya mbegu za mlonge ni mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili.

Vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Vitamini A ipatikanayo katika mafuta ya mbegu za mlonge ni moja ya vitamini zinazotajwa kuwa mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili.

Vitamini A ni mhimu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.

Kwa kuongezea mafuta ya mbegu za mlonge yana lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu.

Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu, madini ya shaba, potasiamu, zinki, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Mafuta ya mbegu za mlonge husafisha mwili wako wote, yanasafisha ini, figo, moyo, macho, yanaimarisha meno, ngozi na nywele.

Mafuta ya mbegu za mlonge ni dawa yenye nguvu dhidi ya bakteria (anti-bacteria), ni dawa dhidi ya virusi (anti-virus) na ni dawa pia dhidi ya fangasi (anti-fungus).

Mafuta ya mbegu za mlonge yametajwa kama dawa ya ajabu ya asili zaidi ya miaka 5000 iliyopita katika maandishi ya kidini huko nchini India.

Mafuta ya mbegu za mlonge yametajwa kwenye vitabu vya tiba huko Misri miaka 2480 kabla ya Yesu.

Siyo kutibu tu bakteria ndiyo kazi ya mafuta ya mbegu za mlonge bali pia ni dawa nzuri kwa mtu mwenye tatizo la kukosa usingizi.

Usingizi ni kitu mhimu katika kuongeza, kutunza na kuimarisha kinga ya mwili.

Kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku ni vigumu mwili wako kuwa na kinga nzuri ya mwili na hivyo utashambuliwa kirahisi na magonjwa ya bakteria, virusi na fangasi.

Magonjwa mengine unayoweza kupona kwa kutumia mafuta ya mbegu za mlonge ni pamoja na:

1. Upungufu wa damu (anaemia)
2. Maumivu kwenye maungio (joints pain)
3. Pumu (asthma)
4. Saratani mbalimbali
5. Kufunga choo
6. Kuharisha
7. Kifafa
8. Kisukari
9. Matatizo ya moyo
10. Maumivu ya kichwa
11. Vidonda vya tumbo
12. Mawe kwenye figo

Kujitibu maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani P.I.D kunywa kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya mlonge kutwa mara moja na unaweza kuongeza mpaka kutwa mara 2 kutegemea na mwili wako unavyoitika kwa dawa.

Ikiwa ni mjamzito usitumie dawa hii.

Mara zote pata ushauri toka kwa tabibu kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia:

1. Kula zaidi matunda na mboga za majani
2. Kunywa maji mengi kila siku
3. Fanya mazoezi ya viungo kila siku
4. Acha soda na juisi yoyote ya dukani
5. Acha sukari na utumie asali badala yake
6. Acha ice cream
7. Acha vyakula vya kuokwa kama vile mikate, biskuti, keki nk
8. Acha vilevi vyote
9. Acha chai ya rangi na kahawa
10. Kuwa msafi daima
11. Usifanye mapenzi kinyume na maumbile
12. Kuwa na mpenzi mmoja
13. Safisha sehemu zako za siri kila baada ya kushiriki tendo la ndoa
14. Nawa mikono na sabuni kila ukitoka kupata haja ndogo au kubwa – bakteria mwingine ajulikanaye kama ‘E.coli’ ambaye hupatikana kwenye kinyesi anahusika pia na ugonjwa wa P.I.D
15. Usishiriki tendo la ndoa ukiwa kwenye siku zako
16. Jiepushe na magonjwa ya zinaa
17.Tembea juani lisaa limoja ukiwa wazi sehemu kubwa ya mwili wako kila siku

Je unahitaji mafuta ya mbegu za mlonge? Kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp