U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo.

Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu.

Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.

Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra.

Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Kinachosababisha U.T.I:

1. Kisukari
2. Maumivu ya mishipa
3. Ajari katika uti wa mgongo
4. Ushoga (kwa wanaume)
5. Usafi duni
6. Upungufu wa maji mwilini
7. Kushikilia mkojo muda mrefu
8. Kurithi
9. Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.

Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

1. Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
2. Kukojoa mara kwa mara
3. Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
4. Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
5. Mikojo kukutoka pasipo kutaka
6. Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
7. Kukojoa damu
8. Harufu nzito au mbaya ya mkojo
9. Homa
10. Kusikia baridi
11. Kutokujisikia vizuri
12. Kujisikia uchovu

Dawa ya U.T.I > Mafuta ya Habbat Soda

Mafuta ya Habbat Soda

Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.

Haya ni moja ya majina yake:

1. Kalonji Oil
2. Black Cumin Seed Oil
3. Nigella Seeds
4. Graine De Nigelle
5. Black Onion Seeds
6. Schwarzkummel

Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’.

Kuna mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta yako mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado nakushauri ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.

Habbat soda ina sifa hizi:

1. Huondoa bakteria mwilini
2. Huondoa uvimbe
3. Huondoa sumu mwilini
4. Inaondoa fangasi
5. Inatibu kansa
6. Inatibu pumu
7. Inadhibiti kazi za histamini
8. Inaua virusi
9. Inazuia damu kuganda

Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!

Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo’

Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea ujulikanao kama ‘Nigella Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa. Asili yake ni Afrika kaskazini, mediterania/ulaya na Asia na kutoka hapo umesambaa kila sehemu ya dunia.

Habbat soda inachukuliwa kama moja ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.

Maambukizi na matatizo mengi kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo kwa ujumla yanatibika na mafuta ya habbat soda ikiwemo ugonjwa wa U.T.I (yutiai) unaowasumbua watu wengi miaka ya karibuni.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.

Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

1. Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
2. Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
3. Penda kuwa msafi.
4. Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma (hasa kwa wanawake) na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
5. Jisafishe vizuri mara baada ya tendo la ndoa.
6. Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
7. Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
8. Epuka kaffeina.
9. Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.

Kama utahitaji dozi kamili ya U.T.I niachie ujumbe WhatsApp +255714800175.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imesomwa mara 517

Imehaririwa

Categories: U.T.I

Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp