Dawa ya uvimbe kwenye kizazi

Published by Fadhili Paulo on

Dawa asili ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi

Dawa ya uvimbe kwenye kizazi

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid.

Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.

Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.

Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;

1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini
2. Ujauzito
3. Uzito na unene kupita kiasi
4. Jenetiki zisizo za kawaida
5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu
6. Sababu za kurithi
7. Lishe isiyo sawa
8. Sumu na taka mbalimbali nk

Dalili zitakazokuonyesha una uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na;

Dalili za uvimbe kwenye kizazi:

1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi
2. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi
3. Kuvimba miguu
4. Unaweza kuhisi una ujauzito
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kuhisi kuvimbiwa
7. Kupata haja ndogo kwa taabu
8. Kutokwa na uchafu ukeni
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo
10. Maumivu nyuma ya mgongo
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto
12. Upungufu wa damu
13. Maumivu ya kichwa
14. Uzazi wa shida
15. Kutopata ujauzito
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo
17. Maumivu ya nyonga
18. Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage)

Aina za Uvimbe kwenye kizazi

Kuna aina kuu nne za Fibroids

1. Intramural: Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe.

2. Subserosal fibroids: Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana.

3. Submucosal fibroids: Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi.

4. Cervical fibroids: Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

Dawa ya kuyeyusha uvimbe kwenye kizaziUzazi Mjarabu

 

Ikiwa mwanamke hapati shida ya namna yo yote katika shughuli zake za kila siku, anaweza asihitaji tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamke anapokaribia kukoma hedhi Uvimbe huu hunyauka wenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Ikitokea kwamba tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali ilivyo.

Dawa ya Uvimbe kwenye kizazi > UZAZI MJARABU

Moja kati ya dawa za asili zinazoaminika kuwa na matokeo mazuri katika kutibu na kuondoa uvimbe kwenye kizazi ni Uzazi mjarabu.

Uvimbe kwenye kizazi unaweza kutibika kirahisi kwa kutumia uzazi mjarabu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu mwilini na uwezo wake mwingine wa asili wa kuzuia kuongezeka kwa vivimbe visivyo vya kawaida mwilini.

Uzazi mjarabu ni dawa ambayo inao uwezo wa kuondoa uvimbe mwilini ikiwemo kuongeza kinga ya mwili.

Uzazi Mjarabu hutumika pia kuondoa uvimbe unaotokana na saratani.

Kwenye dawa hii uzazi mjarabu kuna kitu kinajulikana kwa kitaalamu kama ‘Polysaccharides’ ambacho huhamasisha kuundwa kwa ‘nitric oxide’ ambayo huudhoofisha na kuuondoa uvimbe wowote wa saratani.

Uzazi Mjarabu ni dawa ya asili yenye mchanganyiko wa mitishamba na mimea mbalimbali ya asili maalumu kwa ajili ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi na kukuwezesha kupata ujauzito.

Ni dawa ya asili yenye uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali yanayosababisha ugumba kwa pamoja.

Inasaidia kuweka sawa homoni, kuondoa uvimbe kwenye kizazi, kupevusha mayai, kuzuia ujauzito usiharibike, kuzibua mirija, kutibu maambukizi kwenye kizazi, kutoa sumu mwilini, kuleta ute wa uzazi na mengine mengi kwa pamoja.

Dawa hii ina viinilishe, madini na vitamini zote mhimu kama ifuatavyo;

Uzazi mjarabu ina:

1. Vitamini B6

Kazi kubwa ya vitamini B6 ni kusaidia mimba kukaa sawa na salama wiki mbili za mwanzo tangu ujauzito utungwe (Luteal phase).

Hiki ni kipindi cha maandalizi cha kipindi kingine kijacho katika safari ya ujauzito na ni lazima mazingira yawe ya afya katika mji wa uzazi wa mwanamke ili kweli ujauzito uendelee kukua.

Hivyo siku hizi 14 za mwanzo vitamini B6 ni ya mhimu ili ujauzito ubaki na afya.

Kama huna hii vitamini vya kutosha basi hizi siku 14 hazitafika na ndani ya siku 7 au 10 ujauzito utakutoka.

2. Vitamini B12

Vitamini B12 ni vitamini mhimu sababu husaidia kuweka sawa homoni. Kama matokeo yake inakusaidia kupata siku zako vizuri na kama siku zako zinaenda vizuri basi ni rahisi pia kwako kupata ujauzito wenye utulivu na afya bora ya mtoto.

Vitamini hii ni mhimu pia kwa baba kwani husaidia kumpa mwanaume mbegu nyingi na zenye ubora wa kutungisha mimba.

3. Vitamini C

Vitamini C imekuwa ikihusishwa na uzazi kwakuwa inasaidia kuweka sawa homoni na kukupa mzunguko mzuri wa hedhi vitu ambavyo ni mhimu ili uwe na afya ya kuweza kupata ujauzito.

Hii ni vitamini mhimu kwa kinamama ambao wamekuwa wakitumia dawa za uzazi wa mpango kwa kipindi kirefu. Husaidia mji wa uzazi uwe tayari na sawa kwa ajili ya kutunga ujauzito.

Vitamini hii inaisapoti homoni ya ujazi ijulikanayo kama ‘progesterone’ katika mwili na kuimarisha kuta za mji wa uzazi baada ya mimba kutungwa.  

4. Vitamini D

Upungufu wa Vitamini D umekuwa ukihusishwa na ugumba moja kwa moja.

Tafiti zinaonyesha upungufu wa vitamini D unaathiri tishu au ogani za uzazi za mwanamke kwamba ogani hizo haziwezi kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya.

Vitamini D pia ina umhimu mkubwa katika kukua kwa seli na ufanyaji kazi wake. Tafiti zinaonyesha wanawake wenye vitamini D ya kutosha wanakuwa na mji wa uzazi mzuri na wenye afya.

5. Vitamini E

Bila Vitamini E ni vigumu kupata ujauzito. Hii ni vitamini mhimu katika kulinda afya ya seli zetu na hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini na hivyo kuzilinda seli zisidhurike kirahisi.

Hii inajumuisha seli za mayai ya uzazi, kuta zinazozunguka yai zimetengenezwa kwa vitamini E.

Vitamini E pia husaidia kuweka sawa mbegu za mwanaume kwa kuongeza wingi na ubora wake kwa ajili ya uzazi.

6. Madini ya Folate

Kuwa na kiasi cha kutosha cha madini haya ni jambo la mhimu ikiwa unahangaika kupata ujauzito. Madini haya ni mhimu ili kuzuia ujauzito usitoke.

Ni mhimu mwili uwe na madini haya mapema wakati wowote unapojiandaa kushika ujauzito.

Ukisubiri mpaka upate ujauzito ndiyo uanze kutafuta haya madini tayari utakuwa umeshachelewa.

7. Madini ya chuma

Madini ya chuma yana uhusiano wa moja kwa moja na uzazi. Yanahitajika ili kuzizalisha homoni mbili mhimu za uzazi ambazo ni estrogen na progesterone, ambazo ni homoni mhimu kwa utungaji wa kawaida wa ujauzito.

Tafiti zinaonyesha wanawake wenye kiasi kidogo cha madini haya mwilini mwao wanapata wakati mgumu katika kushika ujauzito.

Mara tu upatapo ujauzito madini ya chuma ni ya mhimu sana ili kuwa na ujauzito wenye afya kipindi chote cha miezi 9.

8. Omega-3 na Omega-6

Haya hujulikana kama mafuta mazuri (good fats). Kumbuka siyo kila mafuta ni mabaya kwa mwili wako, yapo mafuta mazuri na ambayo yanahitajika na mwili wako ili kuwa na afya bora.

Omega-3 na Omega-6 husaidia kuweka sawa homoni zako na kuzifanya zifanye kazi kwa usahihi jambo linalohamasisha uhakika wa kuwa na uwezo wa kutunga kwa mimba na kuwezesha damu kusambaa vizuri kwenye ogani za uzazi.

9. Madini ya Selenium

Selenium ni madini madogo ambayo hufanya kazi kama kiondoa sumu mwilini na hivyo kuimarisha ubora wa seli zetu.

Pia ni madini mhimu kwa ajili ya uundwaji wa mayai na hudhibiti kazi za tezi ya thyroid, tezi ambayo ni mhimu kwa uzalishwaji na uwekaji sawa wa homoni.  

10. Madini ya Zinki

Madini ya zinki ni mhimu kwa pande zote mbili kwa mwanamke na mwanaume. Kwa wanawake zinki husaidia uzalishwaji wa mayai na kuyaweka mayai yenye afya na kuweka sawa homoni.

Upungufu wa madini ya zinki pia unahusishwa na mimba kuharibika katika wiki za mwanzo mwanzo tangu kutungwa kwake.

Hivyo kama umekuwa na bahati ya kupata ujauzito halafu haichukuwi muda zinatoka kuna uwezekano mkubwa una kiasi kidogo cha madini ya zinki kwenye mwili wako.

Dawa hii inaweza kutumika na yoyote hata kama ni mwenye vidonda vya tumbo au hata mjamzito chini ya uangalizi wa Tabibu.

Ikiwa unahitaji dawa hii ya asili ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175