Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara 1

Hakuna kitu kinavutia zaidi kama kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Hata hivyo tatizo la kupotea kwa nywele au upara ni tatizo kubwa linalowapata watu wengi kila pembe ya dunia.

Nywele inawezekana ndiyo kitu cha kwanza hasa linapokuja suala la urembo hasa kwa wasichana, wadada na wamama kwa ujumla. Hii inamaanisha nywele zinaangaliwa zaidi na watu kuliko hata nguo, dhahabu au hata viatu.

Nywele ndiyo taji, fahari na kung’aa kwa utukufu wa mwanadamu katika ulinzi na kujiamini.

Ingawa katika zama hizi za vyombo vingi vya habari, wanawake wamekuwa wakishinikizwa na kupewa presha juu ya kuwa aina fulani ya muonekano wa nywele kwa maana ya urefu, rangi, ulaini wake au staili yake.

Namna nywele zako zinavyoonekana isitokee kuwa ni kizuizi cha wewe kutokujisikia vizuri bali unahitaji zaidi kujipenda, kujiamini na kujikubali hivyo ulivyo.

Nywele zako ni kitu pekee na cha thamani

Haijalishi ikiwa wewe ni mwafrika, ni mzungu, ni mchina au mhindi, vile Mungu amekuumba na kukupa hizo nywele wewe ni mrembo na ni wa pekee hivyo ulivyo.

Tofauti ya nywele mara nyingi ni matokeo ya asili ya ki-DNA. Nywele zinaweza kuwa ni kiwakilishi cha utamaduni, sanaa, siasa au namna ya kuwasilisha hisia.

Hakuna kiwango maalumu cha urembo au uzuri wa nywele kwa watu wa utamaduni wowote! Vyombo vya sasa vya habari vinatuchanganya tuwe bize na urembo wa nje ya mwili huku tukijisahau kushughurika na urembo wa ndani ya mwili.

1 Petro 3 : 3 – 4

3. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4. bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara 2
Upara

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupotea kwa nywele kama vile:

 • Sababu za kimazingira, 
 • Kuzeeka,
 • Msongo wa mawazo (stress),
 • Kuvuta sigara kupita kiasi,
 • Lishe duni,
 • Homoni kutokuwa sawa,
 • Kurithi
 • Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
 • Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
 • Baadhi ya dawa za hospitali
 • Matatizo katika kinga ya mwili
 • Upungufu wa madini chuma
 • Na magonjwa mengine sugu 

Uvumilivu unahitajika zaidi kwani ni tiba inayochukua muda mrefu kwa kawaida.

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara

Dozi hii ina dawa 2 na zinapaswa kutumika zote mbili kwa pamoja kwa matokeo mazuri ambapo moja utakuwa unakunywa na nyingine unapakaa kichwani moja kwa moja.

1. Mafuta ya habbat soda

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara 3
Mafuta ya Habbat soda

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele.

Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.

Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Sisi sote kwa pamoja kuna wakati kila mmoja amejishuhudia nywele zake zikipukutika na kukosa afya. Nywele kupungua au kudumaa au kuacha kuendelea kuota ni tatizo ambalo ni vigumu kuliepuka kutokana sababu nyingi zilizo nje ya uwezo wetu.

Kwa bahati mbaya kwa baadhi yetu tatizo linaweza lisiondoke kirahisi au lisiondoke lenyewe na ndiyo sababu ni mhimu kuanza sasa kuwa bize ukijali afya ya nywele zako mara tu unapoanza kuona dalili za mwanzo za upara kuanza kujitokeza.

Ni jambo la kawaida kupoteza nywele 50 mpaka 100 kila siku, lakini chochote kinachozidi hapa kinapaswa kuchukuliwa hatua za mapema ili kuzuia kujitokeza kwa upara.

Kushughulika na tatizo la upotevu wa nywele mapema siyo tu kunasaida kuzuia tatizo bali pia kunarahisisha ukuwaji mpya wa nywele zilizopotea.

Sehemu hii ya makala nitakueleza faida za mafuta ya habbat soda katika kukuza na kuotesha upya nywele zilizopotea.

Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.

Haya ni moja ya majina yake:

*Kalonji Oil
*Black Cumin Seed Oil
*Nigella Seeds
*Graine De Nigelle
*Black Onion Seeds
*Schwarzkummel

Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’.

Mbegu hizi hujulikana pia kwa jina la ‘MBEGU ZA BARAKA’ (The seeds of blessings).

Zimetumika katika tiba asili kwa maelfu ya miaka iliyopita kutibu aleji, maumivu ya kichwa, pumu, maumivu mbalimbali mwilini, kupandisha kinga ya mwili na kuondoa minyoo tumboni.

Kwa sasa mafuta yatokanayo na mbegu hizi yanatumika katika tiba za asili kwa bidhaa za vipodozi na urembo. Mafuta haya yana sifa kuu na uwezo wa kuondoa sumu na harara katika ngozi.

‘Thymoquinone’ ni kiondoa sumu na harara kinachopatikana kwenye mafuta ya habbat soda ambacho hupigana dhidi ya magonjwa ya ngozi yasababishwayo na bakteria na fangasi.

Hii thymoquinone iliyomo kwenye habbat soda ina protini, alikaloidi na king’arisha mwili cha asili kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘saponins’ ambavyo kwa pamoja huiimarisha afya ya ngozi ya kichwa na kuongeza uotaji wa nywele huku vikipunguza dalili za kuzeeka kwa seli zinazounda nywele.

Habbat soda hupunguza kupotea kwa nywele kunakosababishwa na harara kwenye vinyweleo vya nywele.

Mafuta ya habbat soda huweka sawa usawa usio sawa wa mzunguko wa ukuwaji wa nywele na kuviamsha vinyweleo vya nywele.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yanarutubisha nywele, yanang’arisha nywele na yanaongeza pia hali ya unyevunyevu kwenye ngozi ya kichwa.

Kwa kawaida mafuta haya huongezwa kwenye shampoo, mafuta, na kwenye vipodozi vya asili na vya kisasa kwakuwa huongeza uwingi na msokotano wa nywele na kupoteza upotevu wa nywele unaopelekea kipara.

Mafuta haya pia yanapotumika kuotesha na kukuza nywele huleta faida nyingine kwa upande wa nywele zifuatazo:

(A). Huimarisha afya ya ngozi ya kichwa

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yana uwezo wa kudhibiti harara, fangasi, bakteria, virusi na maumivu katika ngozi. Uwezo huu ndio unaoyafanya kuwa dawa nzuri ya kuilinda na kuimarisha afya ya ngozi ya kichwa.

Sifa hii ndiyo inayoyawezesha mafuta haya kuwa dawa bora kwa matatizo ya ngozi ya kichwa kama vile mba.

(B). Huhamasisha ukuwaji wa nywele

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yana vitu viwili vijulikanavyo kama ‘nigellone’ na ‘thymoquinone’ ambavyo vyote viwili ni mdhibiti mzuri wa asili wa histamini.

Dawa zinazodhibiti histamini mara nyingi hupewa watu wenye upara (androgenic alopecia) ambao ni matokeo ya matatizo ya kutokutulia kwa kinga ya mwili (autoimmune diseases).

Kutumia mafuta ya habbat soda ya nywele kama mafuta yako ya nywele kila siku ni njia salama ya kupata faida ya udhibiti wa histamini (antihistamines) kwa ajili ya kuotesha na kukuza upya nywele bila kuhitaji kutumia dawa za kizungu ambazo zinaweza kuwa na madhara mengine mabaya kiafya.

(C). Huzuia kupotea kwa nywele

Hii ndiyo faida kubwa inayojulikana zaidi ya mafutaya habbat soda linapokuja suala la afya ya nywele.

Habbat soda ya nywele ni moja kati ya viungo mhimu zaidi unavyoweza kutumia kutibu tatizo la kupotea kwa nywele. Mafuta haya yana viinilishe tofauti tofauti zaidi ya 100 ambavyo ni vyanzo vya virutubisho kwa vinyweleo vyako vya nywele na ngozi ya kichwa.

Urutubishaji huu wa ziada utasababisha uponyaji wa vinyweleo vyako vya nywele kurudi kwenye afya yake ya kawaida na hivyo kutibu tatizo la kupotea kwa nywele (hair loss).

(D). Huzuia mvi

Mafuta ya habbat soda hujulikana pia kwa uwezo wake wa kuzuia na kuondoa mvi kichwani. Yana ‘linoleic acid’ ambayo husaidia kuzuia kupotea kwa seli zinazounda rangi ya asili ya nywele kwenye vinyweleo vyako.

Ni dawa nzuri pia kwa watu ambao wana tatizo la ngozi lijulikanalo kama zeruzeru au vitiligo kwa kiingereza ambapo mtu anapoteza rangi yake ya asili na kuwa na mabaka mabaka meupe kwenye baadhi ya maeneo ya mwili.

(E). Yanasaidia ku-Condition nywele

Sebum ni mafuta ya asili ambayo huzalishwa kwenye ngozi yako ya kichwa ambayo husaidia kuziacha nywele zako na unyevunyevu na zenye afya.
Si kila mmoja wetu ana ngozi ya kichwa inao uwezo wa kuzalisha hii sebum na ndiyo sababu kuna wenye ngozi ya mafuta na kuna wengine wana ngozi kavu.

Mafuta ya habbat soda yanaweza sawa usawa wa uzalishaji wa sebum kwenye ngozi yako ya kichwa. Kazi hii ya habbat soda inazihakikishia nywele zako zinabaki kuwa na hali nzuri bila kuwa na mafuta mengi kupita kiasi au kuwa kavu kupita kiasi.

(F). Huzuia uharibifu wa ngozi ya nywele

Vijidudu nyemelezi (Free radicals) vinaweza kuleta madhara kwenye ngozi ya kichwa na nywele. Mafuta ya habbat soda yana viondoa sumu (antioxidants) ambavyo huondoa madhara ya vijidudu kwenye nywele zako.

Hii husaidia kuziacha nywele zako na ngozi ya kichwa vikiwa na afya nzuri na bila madhara yoyote.

(G). Huhamasisha mzunguko wa damu

Mafuta haya yana omega-3 na 6 vitu viwili ambavyo huhamasisha kuongezeka kwa mzunguko wa damu hasa katika eneo la ngozi ya kichwa.

Hii husaidia kuota na kukua nywele kwa haraka ndani ya wiki kadhaa tangu uanze kuyatumia kukuza, kuotesha au kama mafuta yako ya nywele ya kila siku.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa na huwa mazito kidogo.

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele.

Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.

Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa na huwa mazito kidogo.

2. Unga wa Majani ya Mlonge

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara 4

Ingawa katika mbio hizi za urembo wa nywele (na hakuna ubaya wowote katika hili) mti wa ajabu wa mlonge una umhimu mkubwa ambao hujawahi kuambiwa na mtu katika kutunza, kukuza na kuweka vema afya ya nywele kwa ujumla.

Unaweza kuniuliza KIVIPI?

Kabla ya yote ngoja tujifunze ni viinilishe vipi, vitamini zipi na madini yapi ambayo ni MHIMU kwa kuotesha, kukuza na kuboresha afya ya nywele kwa ujumla.

Vile vile yakupasa utambuwe kuwa ubora wa afya yako kwa ujumla unaweza kutambulika kwa kuangalia muonekano wa nywele zako tu! Nywele zako zinaonyesha afya yako ilivyo.

Kama mwili wako ni mzima, una viinilishe vyote mhimu na nywele zako zitaonekana kuwa zina furaha pia. Ikiwa kuna shida mahali popote kwenye mwili wako nywele zako zitatuonyesha hilo.

Utumiaji wa kila siku wa vitamini na madini mhimu na asidi amino ni mhimu katika kutunza nywele zetu zibaki na afya na zenye furaha. Baadhi ya vitamini, madini na asidi amino ni mhimu kwa ajili ya uundwaji wa ‘keratin’ ambayo hufahamika kama umeng’enywaji wa nywele ( hair metabolism).

Siri kubwa nyuma ya pazia la ukuwaji wa nywele …

Kwahiyo, kwa ubora kabisa wa kukua kwa nywele, vinyweleo vya nywele lazima viwe na kiasi cha kutosha cha viinilishe na oksijeni katika mfumo wa mwili ili kuotesha na kukuza nywele.

Kumbuka mti huu wa ajabu wa mlonge umebarikiwa kuwa na vitamini na madini kwa wingi kuliko mti au mmea wowote chini ya jua. Mlonge una viinilishe 92 vya madini na vitamini mbalimbali huku ukiwa na viondoa sumu mwilini 46!

Kama tunavyoweza kuona mlonge ni kitu maalumu mno na cha ajabu, una viinilishe vingi mno kwa ajili ya afya ambavyo siyo rahisi kuvieleza vyote katika makala hii lakini nitajaribu kuvigusia baadhi kati ya hivyo mhimu kwa ajili ya nywele.

Mlonge una vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye machungwa, una madini ya chuma mara 25 zaidi ya yale yaliyomo kwenye spinachi na mara 17 zaidi ya kalsiamu zaidi ya ile iliyomo kwenye maziwa na mara 4 zaidi ya vitamini A iliyomo kwenye karoti na vitu vingine vingi.

Vitamini A ndiyo vitamini mhimu zaidi katika kutengeneza afya bora ya tishu na seli mabalimbali katika mwili jambo linalopunguza kupotea au kunyonyoka kwa nywele. Mlonge ni mti tajiri wa vitamini A na utachangia kwa sehemu kubwa katika ukuwaji wa nywele zako.

Madini ya Zinki ambayo yanapatikana kwa wingi katika mlonge yanahamasisha ukuwaji wa nywele na kuimarisha kinga yako ya mwili.

Kiasi cha kutosha cha madini ya zinki na vitamini A pia kunazuia kuzibika kwa tezi mafuta ya nywele katika ngozi ya kichwa. Sababu namba 1 ya watu wengi kusumbuliwa na tatizo la kunyonyoka kwa nywele au upara ni matokeo ya kushuka kwa madini ya zinki mwilini.

Ikiwa una upungufu wa madini ya zinki mwilini kutatokea kupungua au udhaifu katika vinyweleo vya nywele ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja na usanisi na DNA ya nywele, wakati zinki ina ushawishi mkubwa katika uundwaji wa asidi nyukilia.

Kingine mhimu kilichomo kwenye mlonge kinachohusika na afya ya nywele ni uwepo wa viatmini nyingi za kundi B kama B1, B2, B3, B4, B6, B7, B12 ,B14, na B17. Hivyo afya mbovu ya nywele inaweza kutokea ikiwa lishe yako ina upungufu wa kiasi cha kutosha cha vitamini za kundi B hasa hasa vitamini B6 na folic asidi.

Vitamini E ambayo huondoa sumu mwilini ni mojawapo ya kiinilishe mhimu katika mlonge ambacho ni cha lazima katika ukuwaji wa nywele sababu huongeza msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa.

Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa (scalp) kunatengeneza upatikanajai wa viinilishe mhimu kwa ajili ya vinyweleo vya nywele jambo linaloleta afya bora ya nywele na nywele kuwa ndefu.

Kwa kuongezea vitamini C kwenye mlonge inaunda msukumo wa damu katika ngozi ya kichwa na vinyweleo vya nywele.

Madini ya Potasiamu madini mengine mhimu katika mlonge yanazipa nywele zako uwezo wa kuchukua viinilishe katika chakula vinavyohitajika ili kuwa na nywele nzito, nyingi na za kuvutia.

Kwenye mlonge pia kuna kiondoa sumu chenye nguvu sana kijulikanacho kitaalamu kama ‘Zeatin’. Tafiti za wazi zimethibitisha kwamba mlonge una kiasi kingi kisicho cha kawaida cha homoni za mimea zijulikanazo ‘cytokinins’ kama vile zeatin.

Katika kuangalia zaidi katika kemikali hii majaribio mbalimbali yamehitimisha kuwa cytokinins kama zeatin zina kazi kubwa katika kukuzuia usizeeke. Namna hili linatokea ni kuwa Zeatin inachelewesha mgawanyiko wa seli (cell division) na kuondoa sumu mwilini.

Madini, Mlonge na Ukuwaji wa nywele …

Salfa ya asili iliyomo kwenye mlonge ni madini mengine mhimu kwa ukuwaji wa nywele.

Sulfur ya asili ambayo ni tofauti na ile ya kutengenezwa ni kitu kilichopo karibu katika kila vyakula tunavyokula hasa matunda na mboga za majani.

Sulfur inashikilia jina la utani (a.k.a) la ‘madini urembo’ kwa sababu hii. Ndiyo madini yanayokuza nywele, kucha, kung’arisha ngozi na hivyo kukufanya uonekane kijana

Madini mengine yaliyomo kwenye mlonge kama vile manganizi, kalsiamu na shaba yanaweza kuhamasisha kukua na kuripea nywele.

Usisahau pia kupendelea kula vyakula vingi ambavyo havijapikwa (staili ya kachumbali nk). Vyakula vingi vya kwenye migahawa si salama kwa ukuwaji wa nywele zako.

Vyakula feki kama vile vyenye sukari nyingi kupitiliza, vinywaji baridi, keki, utumiaji uliozidi wa nyama nyekundu, nyama ya nguruwe (kitimoto) vinachangia kupotea kwa nywele.

Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara 5

Kama unahitaji dozi hii kamili kwa ajili ya kukuza nywele au kuotesha nywele kwa wenye vipara niachie ujumbe WhatsApp +255714800175. Natuma pia mikoani.

Naitwa Fadhili Paulo ni Tabibu wa Tiba Asili, Ofisi yangu inaitwa VICTORIA HOME REMEDY ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam karibu na ofisi ya Tanesco ya Yombo.

Kama utashea ujumbe huu na rafiki zako wengine uchukuwe kama ulivyo usibadili chochote.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine.

Imesomwa mara 1,181

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy Ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175. Pia kama una semina au kongamano lolote na unahitaji mzungumzaji hasa kwa upande wa afya hususani tiba asili, tuwasiliane napatikana.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp +255714800175