Dawa za kupevusha mayai ya uzazi

Kama mwanamke, afya nzuri ya mayai ya uzazi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi na kuwa na uwezo wa kushika ujauzito. Je ni dawa gani nzuri za asili kwa ajili ya kuongeza afya ya mayai yako ya uzazi? Makala hii inajadili hilo kwa kina.

Endelea kusoma ….

Pamoja na dawa, bado kutakuwa na mabadiliko utakayotakiwa kuyafanya hasa upande wa vyakula ili kuongeza uwezekano wa tatizo lako kuisha kwa haraka na kwa uhakika na hivyo kuongeza uwezekano wa wewe kupata ujauzito.

Hapo kabla iliaminika kwamba wanawake huzaliwa na mayai yote ya uzazi na kwamba mwili hauendelei kuyazalisha mengine. Miaka ya karibuni imegundulika katika tafiti mbalimbali kwamba seli ndani ya ovari za mwanamke zinaendelea kuzalisha mayai mengine mapya katika mzunguko wa miaka ya uzazi.

Umri unabaki kitu mhimu sababu ingawa mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mapya bado mji wako wa uzazi utaendelea kuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa afya bora ya mayai kadri umri wako unavyozidi kuongezeka

Kama umekuwa ukiambiwa uwezekano wako wa kupata ujauzito ni mdogo sababu mayai yako yamezeeka basi hilo lisikutishe sababu bado mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mengine mapya kila mara na hivyo bado kuna tumaini kwako.

Ni mhimu kula mlo sahihi na kufanya mabadiliko chanya ya kitabia ili kuvutia upevukaji mzuri wa mayai yako.

Inachukua siku 90 mpaka yai liwe limezalishwa na kuundwa tayari kwa kurutubishwa. Hii ndiyo sababu hatua zozote utakazochukua kuimarisha afya na kukomaa kwa mayai yako lazima zidumu kwa muda mrefu si chini ya miezi mitatu mpaka uone matokeo chanya na mazuri.

Wakati mayai yako yanajiandaa kwa ajili ya kurutubishwa yanaweza kuathiriwa ubora wake na mambo mengi yanayohusiana na hali ya afya yako ya sasa.

Hapa nimekuandikia na kukuelezea dawa asili 7 unazoweza kuzitumia ili kuboresha afya ya mayai yako na hivyo yapevuke vizuri tayari kwa kurutubishwa.

Dawa za kupevusha mayai ya uzazi

1. Mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi ni mhimu sana linapokuja suala la afya bora ya mayai ya uzazi. Ni mafuta ambayo ni lazima ule kila siku ili kuwa na afya nzuri ya mayai kwenye mfumo wako wa uzazi.

Ni mafuta mazuri kwa huboresha afya ya mayai yako ya uzazi kutokana na kuwa ni mafuta ambayo ni mazuri kwa afya.

Nimesema mafuta mazuri. Kuna mafuta ya aina mbili, mafuta mazuri (monounsaturated fats) na mafuta mabaya (saturated fats). Mwili unahitaji zaidi mafuta mazuri kuliko mafuta mabaya.

Ndiyo mwili unahitaji mafuta, usije ukakubali ule msemo kwamba mafuta yote ni mabaya na kwamba mwili wako hauhitaji kabisa mafuta!

Hapana mwili hauwezi kufanya kazi zake vema ikiwa unaunyima kila aina ya mafuta.

Tafiti zinazoonyesha kuwa wanawake ambao chakula chao kingi kinakuwa na mafuta mazuri wanazalisha mayai yenye afya na mazuri kwa uzazi.

2. Unga wa Mbegu za Maboga

Madini ya saliniamu yanahitajika kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa kromozoni katika mayai ya uzazi.

Saliniamu ni madini ambayo hupatikana kwa wingi katika mbegu za maboga na kazi yake hasa ni kuondoa sumu na kuulinda mwili dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa na hivyo kuruhusu uzalishwaji mzuri wa mayai.

Na watafiti wamegundua kuwa nguvu ya madini ya saliniamu inakuwa kubwa zaidi ikitumika sambamba na vitamini C, vitamini E na beta carotene!

Faida nyingine ya mbegu za maboga katika afya ya mayai ni pamoja na kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya chuma.

Madini ya chuma ni mhimu sana linapokuja suala la afya bora ya mayai ya uzazi. Kama mwili wako una upungufu wa madini ya chuma itakuwa vigumu wewe kupata ute wa uzazi.

3. Unga wa majani ya mlonge

Madini ya zinki yanahitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa homoni zinazohusika na afya bora ya mayai ya uzazi.

Unga wa majani ya mlonge ni chanzo kizuri cha madini ya zinki. Unga wa majani ya mlonge unatoa sumu mwilini, unaongeza kinga ya mwili na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla na hatimaye afya ya mayai ya uzazi.

Kile unachokula kina uhusiano wa moja kwa moja na afya yako ya uzazi na mayai kwa ujumla.

Unga wa majani ya mlonge una vitamini C mara 7 ZAIDI YA ILE INAYOPATIKANA KATIKA MACHUNGWA!

Na hivyo mlonge unabaki kuwa ndicho kitu pekee chenye nguvu ya kuondoa sumu mwilini kuwahi kutokea katika historia.

Vitamini C kama wote tujuavyo ni kitu mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili.

Zaidi sana vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.

Mtu mwenye tatizo la kupevusha mayai yake anahitaji lishe yenye viinilishe vingi mhimu kwa ajili ya afya ya mwili kwa ujumla.

Kwa kuongezea mlonge una lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu.

Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu (mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe), madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi. Mlonge una vitamini A mpaka Z.

Zote hizo ni vitamini mhimu toka katika chanzo cha asili kisicho na madhara yoyote mabaya hapo baadaye ambacho ni mti wa miujiza mti wa mlonge.

Kama umeambiwa mayai yako hayakomai au hayana afya ya kuweza kurutubishwa hakikisha unajumuisha unga wa majani ya mlonge katika orodha ya dawa utakazotumia kujitibu tatizo hili.

4. Mizizi ya Maca

Hii ni dawa nyingine ya asili kwa ajili ya kuimarisha afya ya mayai yako. Mtishamba huu una madini tofauti tofauti mhimu 31 na viinilishe vingine mhimu kwa ajili ya mwili zaidi ya 60.

Ni dawa imetumika kwa maelfu ya miaka katika tamaduni za kiarabu, kichina na kihindi kutibu maradhi mbalimbali mwilini ikiwemo kuongeza afya ya mayai ya uzazi.

Inaamika maca huongeza uwingi wa mbegu za kiume na kuimarisha afya ya mayai ya uzazi. Inaongeza pia hamu ya tendo la ndoa kwa wote mwanamke na mwanaume na kuweka sawa pia homini.

Unaweza kupata mizi ya maca katika mfumo wa vidonge au unga.

5. Asali yenye Mdalasini

Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana.

Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini.

Mchanganyiko huu wa asali na mdalasini unaweza kuimarisha afya ya mirija ya uzazi na hivyo kuleta uzalishaji mzuri wa mayai ya uzazi kwakuwa husaidia pia insulini kufanya kazi zake ipasavyo.

Asali yenye mdalasini inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi kwa wapenzi wa jinsia zote.

Asali yenye Mdalasini imetumika miaka mingi katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Hii ndiyo sababu wanawake wenye tatizo la vivimbe kwenye mfuko wa mayai ya uzazi (Polycystic Ovary Syndrome – PCOS) hushauriwa kuongeza mdalasini kwenye vyakula vyao.

6. Mafuta ya habbat soda

Ikiwa homoni zako hazipo sawa ni vigumu mayai yako ya uzazi kukomaa vizuri kwa ajili ya kurutubishwa. Pia itakuwa ni vigumu kupata ute wako wa uzazi ikiwa homoni hazipo sawa.

Mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya kuweka sawa homoni zako za uzazi na hivyo kuwa na mayai yenye afya. Ukiacha hili la kuweka sawa homoni, Mafuta ya habbbat soda ni dawa karibu kwa magonjwa yote isipokuwa kifo.

Mara nyingi usawa usio sawa wa homoni husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.

Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).

Vitu vingine vinavyopelekea mabadiliko ya homoni ni pamoja na kuongezeka umri, lishe duni, kutokujishughulisha na mazoezi, kupungua kwa ogani ya adreno, mfadhaiko au stress, kukosa usingizi, dawa za uzazi wa mpango, sumu na kemikali mbalimbali nk.

Mafuta ya habbat soda yana asidi amino 15 na 9 kati ya hizo ni asidi amino mhimu zinazohitajika zaidi na mwili, nazo ni leucine, valine, methionine, histidine, isoleucine, lysine, threonine, tryptophan, na phenylalanine.

Kuna tafiti nyingi zinazothibitisha kwamba mafuta ya habbat soda yana kazi sawa na zile za homoni ya estrogen na ni msaada mkubwa katika kuweka sawa homoni za mwili hata kwa wamama wanaokaribia au waliofika ukomo wao wa hedhi.

Mfadhaiko wa akili (Stress) unaathiri mwili wako kwa mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na afya ya mayai yako ya uzazi.

Unapokuwa umefadhaika kwa kipindi kirefu mwili wako huzalisha homoni za prolactin, cortisol na nyinginezo ambazo zinaweza kuzuia mayai yako kuwa na afya bora kwa ajili ya uzazi.

Unaweza kupunguza kiasi chako cha mfadhaiko (stress) kwa kutumia mafuta ya habbat soda

7. Maji ya Kunywa

Maji ni uhai. Kunywa maji mengi ya kutosha kila siku ni mhimu kwa afya bora kabisa ya mayai yako ya uzazi. Unahitaji maji lita 2 mpaka lita 3 kila siku iendayo kwa Mungu ili kuwa na afya bora kabisa ya uzazi.

Mayai yenye afya yanahitaji hewa safi ya oksijeni na mzunguko wa damu unaotiririka vizuri kwenda kila sehemu ya mwili wako. Msukumo wa damu unaweza kupungua ikiwa haunywi maji ya kutosha kila siku na hufanyi mazoezi yoyote ya viungo.

Maelezo ya matumizi ya dawa hizi:

Kwa matokeo ya uhakika kabisa utatakiwa kutumia dawa zote nilizoelezea kwenye somo hili kwa mtindo ufuatao:

1. Asubuhi ukiamka tu, Kunywa mafuta ya nazi kijiko kidogo kimoja cha chai
2. Kisha kula chakula cha asubuhi kunywa unga wa mbegu za maboga vijiko vikubwa viwili ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya parachichi na ndani yake ongeza asali yenye mdalasini kijiko kikubwa kimoja
3. Nusu saa kabla ya chakula cha mchana kunywa kijiko kidogo kimoja cha unga wa majani ya mlonge ukiongeza na kijiko kingine kidogo cha chai cha unga wa mizizi ya maca ndani ya kikombe kimoja cha maji ya uvuvuguvu ongeza asali yenye mdalasini kijiko kikubwa kimoja
4. Usiku wakati unakula chakula kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda wakati unaendelea kula chakula
5. Kunywa maji ya kunywa glasi 2 kila baada ya masaa matatu
6. Fanya hivi kwa miezi miwili mpaka mitatu na tatizo lako linatakiwa kuwa limeisha

Vyakula vinavyosaidia kupevusha mayai:

Vyakula vinavyosaidia kupevusha mayai ya uzazi ni pamoja na Maharage, Parachichi, Samaki, Dengu, Mayai ya kienyeji, Nyama ya kuku wa kienyeji, Ufuta, Korosho, Karanga, Viazi, Uyoga, Mafuta ya zeituni, Spinachi, Maini nk

VITU HIVI USIVITUMIE ILI KUBORESHA AFYA YAKO YA MAYAI:

1. Vyakula vya viwandani
2. Mafuta yatokanayo na wanyama
3. Soda
4. Kaffeina – chai ya rangi, kahawa
5. Vilevi
6. Sukari

Kama utahitaji dawa hizi zote kwa ajili ya kupevusha mayai ya uzazi niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama utanunua kutoka kwangu utakuwa unachangia kuendeleza kazi hii nzuri nimekuwa nikifanya na nitakuwa karibu na wewe kila siku mpaka nione umefanikiwa kutibu tatizo lako.

Napatikana live WhatsApp nyakati zote za mchana kila siku.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

(Visited 211 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp