kirusi cha corona

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Kirusi cha Korona

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Kirusi cha korona (Coronavirus), ni kimelea chenye gamba na kutunza vinasaba vyake katika malighafi za RNA.

Corona virus nikisababishi cha magonjwa mbalimbali na vimelea hivyo vina makabila mbalimbali.

COVID-19 Corona Virus Disease 2019 yaani; Ugonjwa utokanao na virusi vya korona vilivyogunduliwa mwaka 2019

Historia ya Virusi vya Corona

Kirusi cha korona (coronavirus) kimechukua jina lake ‘corona’ kutoka lugha ya kilatini kikimaanisha taji (crown) hii ni kutokana na muonekano wakirusi hicho katika hadubini hufanana na taji ya mfalme.

•Kirusi hicho hutoka katika kundi la vimelea vingi viletavyo homa za mfumo wa hewa mfano mafua.

Kundi hilo la kirusi cha korona lina makabila (strains) mengi ambayo mpaka sasa hayajagunduliwa yote.

•Moja ya kabila limegunduliwa mnamo mwezi wa kumi na mbili mwaka 2019 mjini Wuhan, China nalo hujulikana kama 2019–nCoV (Novelcoronavirus).–

Hili ni kabila hatarishi sana kati ya makabila yote ya korona yaliyogunduliwa. – Husababisha kifo.

•Kirusi cha korona husafilishwa kutoka kwa wanyama kwenda kwabinadamu (zoonoticdisease).

•Baadhi ya wanyama ambao hutunza virusi vya korona na kuleta maradhi ni;–Popo–Ngamia–N.k.

Nani hupatwa na korona?

•Watu wote (wa kike kwa kiume) waweza kudhurika na korona

•Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.

•Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupata korona kwani wana kinga mwili hafifu.

Ukubwa wa tatizo mpaka sasa

•Hili ni tatizo linalotishia kusambaa dunia nzima likianzia mjini Wuhan, China

Dalili za mgonjwa wa korona

Dalili zionekanazo mara kwa mara

•Homa •Kikohozi kibichi
•Uhemaji wa tabu
•Maumivu ya mwili
•Kuuma kwa koo mfano wa matonses (tonsillitis)
•Kukosa hamu ya kula

Dalili za mara chache

•Kuhara
•Kutapika
•Kichwa kuuma
•Kukohoa damu
•Maumivu ya kifua

Kirusi cha korona katika mwili wa binadamu

•Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation period)

•Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.

•Epuka kusalimiana kwa mikono

Wakati gani waweza kudhani ni COVID 19

•Mgonjwa mwenye dalili za homa ya mfumo wa hewa wa chini (LRTI) – tazama kipengele cha dalili na sio homa ya mfumo wa hewa wa juu (mfano: Kukohoa , pua kuwasha, chafya, koo kuuma) na endapo mgonjwa huyo ana historia za Kusafiri kutokea nchi zenye uwezekano mkubwa wa maambukizi ndani ya siku 14

Matibabu

•Dawa za kufifisha makali ya virusi huenda zinaweza kusaidia, lakini bado haijathibitishwa.

–Lopinavir
–Ritonavir
–Ganciclovir
–Oseltamivir
–Remdesivir
–Interferon alpha

Dalili hatari za ugonjwa wa korona

•Homa kali ya mapafu (severe pneumonia)
•Utindio wa ubongo
•Kuhema kwa shida na kutoa mlio wa kifilimbi mithili ya mgonjwa wa pumu.

Je, mgonjwa wa nje anaweza kupata tiba ya dawa za kufifisha virusi?

•Haishauliwi
•Mgonjwa aliyelazwa ndiye anaweza kupata dawa hizo.

Je, dawa za kuongeza kinga mwili (Ig) zinaweza kutibu?

•Hakuna shuhuda za dawa hizo kutibu.
•Dawa hizo zinaweza kusaidia tuu kwa kiasi fulani (immunomodulator) kwenye hali ya homa kali ya mafua (severe pneumonia)

Je, dawa ya Chloroquine hutibu korona?

•Chloroquine husaidia kutibu homa kali ya mapafu(SARS–Co-2)
•Kwa sasa, chloroquine haisaidii katika kutokomeza ugonjwa wa korona.

Je, siruhusiwi kuwapa tiba hewa(nebulization) wagonjwa?

•Ndiyo, ikiwa kuna visa vya korona vilivyothibitishwa katika eneo husika haishauriwi kumpa mgonjwa tibahewa.

•Tibahewa huongeza hatari ya usambaaji wa matone yenye maambukizi kwenda mbali Zaidi.

•Dawa za kuvuta (inhaler) huweza kutumika kama m’badala wa tibahewa.

Kipi ni bora Zaidi katika kumpa mgonjwa hewa ikiwa kuna ugonjwa wa korona?

•Mirijahewa (Oxygenprongs) ni salama Zaidi ukilinganisha na vifunika mdomo na uso (facemasks)

Mtu niliyesafiri naye kwenye ndege amegundulika kuwa ana virusi vya Korona!!!!!!

• Usihofu!

– Ikiwa ulikaa naye umbali wa Zaidi ya viti viwili nusu kipenyo kutoka kwake, hatari ya maambukizo kwako ni ndogo mno.

Je, kuwatenga washukiwa wa korona huongeza hatari ya kuambukizana?

• Ikiwa nafasi kati ya vitanda viwili katika eneo la kuwatenga ni chini ya futi 6, hatari ya kuambukizana ni kubwa!

Kinga

• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni

• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.

• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.

• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona

• Hakuna chanjo mpaka sasa

Maswali na majibu kuhusu virusi vya corona

1. Lini kuvaa mask

• Kwa watu mwenye afya vaa mask endapo unamuhudumia mshukiwa wa COVID – 19

• Vaa mask kama unakohoa au kupiga chafya

• Mask husaidia tuu endapo utazingatia usafi wa mikono kwa kutumia kitakasi (alcohol-based hand rub) cha kileo au sabuni na maji.

• Uvaapo mask unatakiwa kufahamu namna ya kuitumia na kuitupa pia.

2. Je, nCOV-2019 huambukiza kwa wakubwa au wadogo

• Watu wa umri wote huweza kuambukizwa nCOV-2019

• Wazee na watu wenye maradhi (mfano: Pumu, kisukari, maradhi ya moyo) wana hatari kubwa ya kupata COVID-2019 na pengine kupoteza uhai.

• WHO inashauri watu wote kufuata kanuni za ufya na usafi wa njia ya hewa.

3. Je, mifugo ya nyumbani inaweza kusambaza Ncov-2019?

• Kwa sasa hakuna shuhuda zinazoonesha kuwa wanyama wa nyumbani (pets) mfano mbwa au paka huweza kupata kupata maambukizo ya nCOV-2019.

– Hata hivyo, inashauriwa kuosha mikono kwa maji na sabuni mara baada ya kugusana na mbwa/paka.

4. Je, chanjo ya homa ya mapafu husaidia kukinga nCOV-2019?

• HAPANA! Chanjo za homa ya mapafu, kama pneumococcal vaccine na Haemophilus influenza type B (Hib) vaccine, haziwezi kukukinga dhidi ya nCOV-2019.

– Japo chanjo hizi hazisaidii kukinga Ncov-2019, chanjo hizi ni za muhimu na zinashauriwa ili kulinda afya yako.

5. Je, dawa za kuua vimelea (antibiotics) husaidia kukinga nCOV-2019?

• HAPANA! Viua vimelea haziuwi virusi, huua bakteria tuu.

• nCOV-2019 ni kirusi pia, hivyo viua vimelea (antibiotics) zisitumike katika kutibu au kukinga.

• Japo, kwa mgonjwa aliyelazwa kwa COVID-2019, mgonjwa anaweza kupewa dawa hizo kwani bakteria pia wanaweza kushambulia mwili.

6. Je, kusuuza pua kwa maji ya chumvi husaidia kukinga maradhi ya COVID-2019?

• HAPANA! Hakuna shuhuda zioneshazo kuwa kusuuza pua mara kwa mara kwa maji ya chumvi hukinga maambukizi ya nCOV-2019.

• kuna baadhi ya shuhuda zioneshazo kuwa kusuuza pua mara kwa mara kwa maji ya chumvi husaidia mtu kupona mafua ya kawaida tuu.

• Lakini tiba hii haiwezi kutibu maradhi ya mfumo wa hewa.

7. Je, vipimajoto husaidia kwa kiasi gani katika kutambua maambukizi ya nCOV-2019?

• Vipima joto husaidia kugundua kuongezeka kwa joto mwilini kwa watu wenye homa kutokana na maambukizi ya nCOV-2019.

• Vifaa hivi haviwezi kutambua maambukizi kwa mtu ambaye ameambukizwa virusi na hajaanza kupata dalili.

– Hii ni kwasababu huchukua siku 2 hadi 10 mpaka mtu aliyeambukizwa apate homa.

8. Je, kula vitunguu saumu husaidia kukinga maradhi ya nCOV-2019?

• Vitunguu saumu ni vyakula vya afya ambavyo huenda zina baadhi ya nguvu za kuua bakteria.

• Hata hivyo, hakuna shuhuda mpaka sasa zioneshazo kuwa kutafuna kitunguu saumu hukinga maradhi ya COVID-2019.

Soma hii pia > Vyakula 16 vinavyoongeza kinga ya mwili

9. Je, miale ya mwanga wa taa za ultraviolet huweza kuua nCOV-2019?

• Miale ya taa za ultraviolet (UV) isitumike kutakasa mikono au sehemu zingine za ngozi, kwani miale hiyo huweza kuleta madhara katika ngozi.

10. Je, vikausha mikono (hand dryers) husaidia kuua nCOV-2019?

• HAPANA! Vikausha mikono vya umeme haviwezi kuua nCOV-2019.

• Kujikinga na maambukizi unatakiwa usafishe mikono yako kwa kileo (alcohol-based hand rub) au osha mikono kwa maji safi na sabuni. Ukishaosha mikono yako ikaushe kwa kitambaa safi au vikausha mikono vya umeme.

11. Hali ya hewa baridi na barafu HAYAWEZI kuua nCOV-2019.

• Hakuna sababu ya kuamini kuwa hali ya hewa baridi huweza kuua mashambulio haya.

• Joto la kawaida la binadamu hubaki kati ya 36.50 na 370, hii haijalishi hali ya hewa ya nje ya mwili iko kwa kiasi gani.

• Njia ya kuaminika kuweza kujikinga na vimelea hivi ni kusafisha mikono yako mara kwa mara kwa kileo (alcohol-based handrubs) au maji na sabuni.

12. nCOV-2019 haiwezi kuambukizwa kwa njia ya kung’atwa na mbu.

• Mpaka sasa haijathibitika kuwa mbu huweza kusafirisha nCOV-2019 kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
• COVID-2019 ni kirusi kipya kinachovamia njia ya hewa ambavyo husafirishwa kwa njia ya matone

(droplets) yazalishwayo pindi mgonjwa anpokohoa au kupiga chafya, au mate au makamasi.

• Unashauriwa ufuate kanuni za afya za kunawa mikono pia kuepuka kugusana na mtu anayekohoa au kupiga chafya.

13. Kuoga maji ya moto hakuwezi kukukinga kupata nCOV-2019

• Joto la mwili huwa ni 36.50C na 370C, haijalishi umezungukwa kwa joto la kiasi gani. Kuoga maji ya moto kupita kiasi kutakusababishia kuunguza ngozi yako tuu.

• Kujikinga na maambukizi fuata kanuni za usafi wa mikono. Hii husaidia kuua virusi ambavyo vinaweza kuwa katika mikono yako.

• Epuka maambukizi yanayoweza kukupata kwa kugusagusa pua zako, mdomo na pua.

14. Virusi vya korona haviwezi kuambukizwa kutoka bidhaa zinazozalishwa China au nchi yoyote iliyothibitika kuwa na mashambulio ya nCOV-2019.

• Hata kama kirusi cha korona huweza kukaa kwa masaa au siku kadhaa (hutegemea na aina ya uso wa kitu), hakuna uwezekano kuwa kirusi cha korona kuendelea kuwepo katika uso wa kitu baada ya kuondoshwa, kusafirishwa na kupitia katika hali za hewa tofauti na joto tofauti.

• Kama unadhani uso wa kifaawaweza kuwa na vimelea, basi safisha uso huo kwa kutumia kiua wadudu.

• Baada ya kukigusa kifaa hicho safisha mikono yako.

15. Je, kujipulizia kileo (alcohol) au kemikali za klorini mwili mzima kwaweza kuua Ncov-2019?

• HAPANA! Kujipulizia kileo au kiua wadaudu hakuwezi kuua virusi vilivyo kushambulia.

• Kujipulizia vitu hivyo huweza kuwa hatari kwa nguo au sehemu laini za ngozi (macho, mdomo).

• Kuwa mwangalifu, kileo na kiua wadudu cha klorini huweza kuua wadudu walio katika nyuso za juu, lakini zinatakiwa kutumika kwa maagizo sahihi.

1• Kirusi cha korona ni kikubwa, kina ukubwa wa kipenyo cha maikro 400 – 500. Kwa sababu hii, mask yoyote ile huweza kuzuia kirusi hicho kisipenye.

2• Kirusi cha korona kikianguka katika uso wa chuma, huweza kuishi kwa masaa 12, hivyo ni lazima kusafisha mikono kwa sabuni na maji safi.

3• Ikiwa kirusi cha korona kikianguka katika uso wa pamba au nguo (fabric surface) hubaki hapo hai kwa masaa 9, hivyo yakupasa kusafisha nguo safi au anika juani kwa masaa mawili ili uweze kuviua au kuviondosha.

4• Ikiwa kirusi kitakutana na joto kati ya 226 – 270C, hufa, kwani kirusi hicho hakiwezi kuishi katika mazingira ya joto.

• Hivyo kuepuka vyakula vya baridi na ice-cream au kuishi mazingira ya joto husaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya korona.

5• Kirusi cha korona huishi kwenye mikono kwa takribani dakika 10, hivyo kuwa na kitakasishi cha kileo (alcohol sterilizer) mfukoni husaidia kukinga maambukizi ya korona.

6• Kirusi cha korona hakibaki hewani, kirusi hiki hutua chini, hivyo ni vigumu kuambukizwa kwa njia ya hewa.

Soma hii pia > Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

ASANTENI

VIRUSI VYA KORONA IMEANDALIWA NA Eusebius Joseph Mikongoti, M.D.Medical Officer The Aga Khan Polyclinic IRINGA

Ukubwa wa tatizo mpaka sasa

Mwenendo wa Virusi vya Corona dunia nzima (Corona Virus Daily Updates):

Takwimu za mwisho za kila siku kidunia na Tanzania

Global Total
Last update on:
Cases

Deaths

Recovered

Active

Cases Today

Deaths Today

Critical

Affected Countries

Total in Tanzania
Last update on:
Cases

Deaths

Recovered

Active

Cases Today

Deaths Today

Critical

Cases Per Million

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo:

Fahamu kuhusu kirusi cha korona Click To Tweet

Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 149

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *