faida za mafuta ya nazi

Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

FAIDA 39 ZITAKAZOKUSHANGAZA ZA MAFUTA YA NAZI KIAFYA

Zaidi ya tafiti 1500 zimethibitisha kuwa mafuta ya nazi ndiyo mafuta bora zaidi chini ya jua.

Hili halishangazi sababu karibu kila mtu anajua mafuta ya nazi ni dhahabu kwa afya ya mwili na ngozi kwa ujumla.

Bidhaa nyingi za vipodozi ukizichunguza utagundua huongezwa pia mafuta ya nazi ndani yake.

Ili upate faida hasa za mafuta haya ni lazima yawe ni ya asili na hayajachanganywa na kingine au kemikali yoyote, hayajapita kwenye moto wakati wa kuyatengeneza na yakiwa hivyo hujulikana kama mafuta bikra ya nazi (Virgin Coconut Oil).

Nyingi ya faida za mafuta ya nazi ni matokeo ya kuwa na asidi mafuta mhimu sana ijulikanayo kama ‘lauric’.

Lauric ni asidi mafuta mhimu ambayo ni mdhibiti mzuri dhidi ya bakteria, fangasi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi.

Ili kupata faida hizi nyingi za mafuta ya nazi unaweza kuyanywa au kupakaa juu ya ngozi.

Mafuta ya nazi ni moja ya chanzo cha viinilishe mhimu sana mhimu na hivyo kufanya moja ya dawa mbadala mhimu kuwa nayo.

Mafuta ya nazi yanaweza kutumika kuongeza kinga ya mwili, kuzuia matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji, kuponya matatizo katika figo, kutibu shinikizo la chini la damu, kupunguza hatari ya kisukari nk

Matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya nazi yanaweza kuongeza umeng’enywaji wa asidi amino, madini, vitamini mhimu na hivyo matumizi yake yanaweza kuboresha muonekano wako kwa ujumla.

Ndiyo maana siyo jambo la kushangaza kuona bidhaa nyingi kama vipodozi, sabuni na zile dawa za nywele ndani yake zikiongezwa mafuta ya nazi pia.

Kuna faida nyingi za kushangaza katika mafuta ya nazi kwa ajili ya afya na urembo ambazo ninapenda kukuonyesha kupitia makala hii.

Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

1. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’enywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama ‘ketones’.

Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.

Kwa bahati mbaya ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha.

Watu wanaosumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu wanatakiwa waongeze matumizi ya mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku.

Kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu ni moja ya kazi za mafuta ya nazi ambayo ninapenda kukufahamisha kupitia makala hii.

2. Huzuia uwezekano wa kupata kansa

Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa.

Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.

Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama “helicobacter pylori” ambaye husababisha vidonda vya tumbo.

3. Yanaongeza kinga ya mwili mara dufu

Kinga imara ya mwili ina umhimu mkubwa katika kupigana na aina mbalimbali za magonjwa.

Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.

Unaweza kupakaa moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.

4. Yanaongeza nguvu za ubongo

Utafiti mmoja uliofanywa mwaka 2004 unaonyesha mafuta ya nazi yana uwezo wa kuongeza nguvu za ubongo hata kwa watu wenye umri mkubwa na wazee.

Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.

5. Yanaongeza nguvu na uvumilivu

Mafuta ya nazi yana uwezo wa kukupa nguvu na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, moja ya kazi mhimu zaidi ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu.

Hii ndiyo sababu wakimbia mbio wengi hupendelea kutumia mafuta ya nazi.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya nazi na kijiko kidogo kingine cha asali mbichi na unywe pamoja mchanganyiko huu kila siku kutwa mara 1 kabla ya kwenda kwenye mazoezi au kwenye kazi yoyote ngumu.

6. Dawa nzuri kwa matatizo ya mifupa

Ugonjwa wa mifupa husababishwa na vijidudu nyemelezi na mfadhaiko wa mwili wa muda mrefu.

Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.

Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umeng’enywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.

Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako.

Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.

7. Husaidia kushusha uzito

Watu wengi wanaamini kwamba ili kupungua uzito basi hutakiwi kabisa kutumia mafuta.

Hata hivyo hili si jambo la kweli.

Kupunguza uzito ni moja ya kazi nyingine nzuri sana ya mafuta ya nazi.

Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.

Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.

8. Huondoa mfadhaiko (Stress)

Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu.

Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.

Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi.

Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.

Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.

Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.

Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.

Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi.

Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.

9. Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.

Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.

Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.

Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umeng’enywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimeng’enya vinavyohusiana na mmeng’enyo wa chakula.

10. Jitibu matatizo katika Kongosho na Kibofu cha mkojo

Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.

Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.

11. Yanatengeneza Misuli ya mwili

Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.

Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.

Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.

Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.

12. Zuia jino kuoza na magonjwa ya kwenye fizi

Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.

Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi.

Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.

Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).

13. Ongeza ufanisi wa Ini na Figo

Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.

Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.

Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.

Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.

14. Yanaondoa mawe katika figo na kibofu cha mkojo

Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa ‘Monooctanoin’ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.

Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.

Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.

15. Yanatibu baridi yabisi

Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.

Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.

16. Husaidia kazi za tezi koromeo (Thyroid gland)

Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.

Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.

17. Yanatibu kisukari aina ya kwanza

Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.

Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.

Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.

18. Hutibu maambukizi ya fangasi

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.

Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii.

Hii ni matokeo ya kuwa na ‘lauric acid’ na ‘capric acid’.

Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.

Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.

19. Yanaweka sawa homoni zako.

Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa.

Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.

Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama ‘lauric acid’.

Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama ‘estrogen’.

Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.

20. Yatakufanya usizeeke mapema

Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote.

Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.

Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.

Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.

21. Hupunguza maradhi ya ubongo

Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa ‘ketones’ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘amyloid beta peptides’.

Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Phenolic compounds’ ambacho hudhibiti ile kemikali ya ‘amyloid beta peptides’ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.

22. Hupunguza njaa

Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.

Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.

23. Yanapunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo

Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.

Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.

Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

24. Yanauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.

Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemeng’enywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.

Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.

25. Yanapigana kuondoa vijidudu nyemelezi

Maisha yetu ya kila siku yanapelekea kuundwa kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili bila sisi kupenda.

Kuzidi kujitokeza kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili ndiyo kunakopelekea mwili kuwa ni wa kuchokachoka kila mara na ni chanzo cha magonjwa mengine mengi.

Kuendelea kutumia mafuta ya nazi kutasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.

26. Yanaotesha nywele

Faida za mafuta ya nazi haziishii ndani ya mwili tu, bali yana faida nyingine nyingi yanapotumika nje ya mwili.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuzuia aina yoyote ya upotevu wa nywele.

Kupungua kwa protini kunaweza kuwa ni sababu nyingine ya kupotea kwa nywele zako kama hakutadhibitiwa kwa haraka.

Unachohitaji ni kuyafanya kuwa mafuta yako ya nywele na hutachelewa kuwa na nywele nzuri zinazopendeza.

Mafuta ya nazi ni mlinzi mzuri wa nywele zako.

27. Yanaondoa mba kichwani

Unasumbuliwa na mba kichwani?

Pakaa mafuta ya nazi na mba utapotea bila kupenda wenyewe.

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa mbadala zenye nguvu kutibu tatizo la mba.

Dawa nyingi na vipodozi vya kuondoa mba kichwani huongezwa mafuta ya nazi ndani yake.

Tuliona pia pale juu kuwa hutumika kuotesha nywele.

Unahohitaji ni kufanya ni kuamua mafuta ya nazi kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa kichwani na mba utapotea wenyewe kadri unavyoendelea kuyatumia.

28. Mafuta bora zaidi kwa ngozi yako

Mafuta pekee mazuri kwa ngozi yako ni mafuta ya nazi.

Hii ndiyo sababu dawa nyingi na vipodozi vya ngozi ndani yake huwa na mafuta ya nazi pia.

Kama una ngozi kavu au yenye mikunjokunjo basi pakaa mafuta ya nazi na ngozi yako itakuwa nzuri, nyororo, yenye rangi yake ya asili na ya kupendeza sana.

Waulize watu wa ukanda wa pwani hili wanalifahamu vizuri sana.

Kama utaamua kutumia mafuta ya nazi kama mafuta yako ya kupakaa magonjwa mengi ya ngozi utayasikia tu kwa jirani.

29. Yanalinda ngozi yako dhidi ya miale ya jua

Viinilishe vya asili kwenye mafuta ya nazi vinawezesha ngozi yako isiathirike na miale ya jua moja kwa moja.

Moja ya kazi nyingine ya kushangaza ya mafuta haya.Mafuta ya nazi ni miwani ya jua ya asili.

Kwa mjibu wa utafiti, mafuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.

Tafiti nyingi zimeonyesha miale ya jua kuwa ina athari nyingi ikitua moja kwa moja juu ya ngozi yako ikiwemo kufanya ngozi kuwa na makunyanzi, magonjwa ya ngozi na kansa ya ngozi.

30. Dawa nzuri ya kusugulia mwili (Scrub)

Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.

Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.

Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.

Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.

Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.

Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.

Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.

* Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini.

*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)

* Kausha uso wako kwa taulo safi.

* Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dakika kama 3 mpaka 5.

*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.

* Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.

* Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.

Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.

Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.

31. Yanatibu vidonda vya homa mdomoni

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nzuri kabisa kutibu vidonda vya homa ambavyo hujitokeza mdomoni.

Unahitaji kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.

Hili linawezekana kutokana na sifa ile ile ya mafuta haya katika kupigana dhidi ya bakteria na virusi na vijidudu nyemelezi.

32. Yanaimarisha kucha

Ukitumia mafuta ya nazi utakuwa na kucha nzuri na zenye kupendeza.

Wakati huo huo kunyunyiza mafuta ya nazi kwenye kucha zako kunaua wadudu wowote wanaoweza kuharibu kucha zako.

33. Hufukuza wadudu mbali

Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu.

Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.

Pakaa mchanganyiko huu mara kadhaa katika siku kwa matokeo mazuri zaidi.

34. Mafuta mazuri kwa ajili ya Lips

Wasichana na wamama wengi ni watumiaji wa bidhaa nyingi za lipstiki zenye kemikali kwa ajili tu ya kulainisha midomo yao ya nje (lips).

Kile wengi hawajuwi ni kuwa bidhaa hizi si salama sana kwa afya zao.

Bahati nzuri kwa wewe unayesoma makala hii mafuta ya nazi yanaweza kutumika kama lipstiki yako ya asili isiyo na madhara mabaya hapo baadaye.

Kwahiyo kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara..

35. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya.

Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.

Hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

36. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula.

Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

37. Mafuta mazuri kwa ajili ya masaji

Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.

Unaweza kuchanganya na mafuta mengine kama ya karafuu na kupata mchanganyiko wa mafuta maalumu kwa ajili ya masaji na ukiyatumia utaweza ku-relax kwa uzuri kabisa huku yakituliza mishipa, misuli, ubongo na mwili wako kwa ujumla.

38. Hutumika kulainisha uke mkavu

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu.

Kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake nyingine ikiwemo ya kutibu, fangasi na bakteria tena bila madhara yeyote mabaya.

39. Husaidia katika ugonjwa wa aleji

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza.

Moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji.

Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

UNAHITAJI MAFUTA YA NAZI?

Mafuta ya nazi nauza 10000 kwa robo lita, ni mafuta ya asili kwa 100% nayatengeneza mimi mwenyewe nyumbani na hayapiti kwenye moto hata dakika 1.

Kama unahitaji niachie ujumbe WhatsApp +255714800175, Kama upo Dar naweza pia kukuletea ulipo unanilipa nauli ya daladala na natuma pia mikoani.

Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100 na kama unataka ya kunywa hakikisha hayajapita kwenye moto wanayaita bikra (virgin coconut oil), ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani yake ile ya asili.

Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 132

2 thoughts on “Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

  1. George Manyama 10/12/2020 at 2:15 am

    I’ve interested with y’r article.

    1. Fadhili Paulo 10/14/2020 at 1:03 am

      You are most welcome George

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *