Fangasi ukeni na tiba yake

Published by Fadhili Paulo on

fangasi ukeni na tiba yake

Fangasi ukeni na tiba yake

Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.

Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:

• Kuwa na wapenzi wengi
• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
• Uchafu
• Uvutaji sigara
• Pombe
• Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili:

• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Maumivu makali chini ya kitovu
• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Fangasi ukeni na tiba yake

Matibabu

Dawa ya asili ya fangasi ukeni  > Palimaua
Ili kutibu aina yoyote ya maambukizi ya ndani ya mwili ambayo yanahusu bakteria, virusi au fangasi kunategemea sana na uimara na ubora wa kinga yako ya mwili.

Kinga yako ya mwili inajumuisha aina ya seli nyeupe maalumu ambazo hutafuta na kuua bakteria na vijidudu vingine nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa.

Kinga yako ya mwili inapokuwa ni dhaifu bakteria wabaya wanaweza kuongezeka na kujirundika mwilini na kusambaa mpaka kwenye via vya uzazi kwa njia ya damu.

Kwahiyo ili kutibu na kukinga P.I.D unahitaji kuwa na dawa ya uhakika ya kuboresha kinga yako ya mwili ifanye kazi kwa kiwango chake cha juu kabisa.

 • Palimaua ni mchanganyiko wa dawa kadhaa za asili maalumu kwa kuimarisha kinga ya mwili nzuri kuliko dawa nyingine yoyote unaifahamu au uliyowahi kutumia.
 • Ni dawa nzuri ya asili inayondoa sumu mwilini.
 • Ina Vitamini C. Vitamini C ni mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili.
 • Vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili
 • Ina Vitamini A ambayo ni moja ya vitamini zinazotajwa kuwa mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili.
 • Vitamini A ni mhimu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.
 • Palimaua husafisha mwili wako wote, inasafisha ini, figo, moyo, macho, inaimarisha meno, ngozi na nywele.
 • Ni dawa bora ya asili yenye nguvu dhidi ya bakteria (anti-bacteria), ni dawa dhidi ya virusi (anti-virus) na ni dawa pia dhidi ya fangasi (anti-fungus).
 • Pia ni dawa nzuri kwa mtu mwenye tatizo la kukosa usingizi.
 • Usingizi ni kitu mhimu katika kuongeza, kutunza na kuimarisha kinga ya mwili.
 • Kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku ni vigumu mwili wako kuwa na kinga nzuri ya mwili na hivyo utashambuliwa kirahisi na magonjwa ya bakteria, virusi na fangasi.
 • Ikiwa ni mjamzito usitumie dawa hii.
 • Inatibu pia vidonda vya tumbo
 • Mara zote pata ushauri toka kwa tabibu kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.

Mpaka hapo nimekupa hii Elimu BURE hujanilipa hata sh 100. Hela haitibu mtu ndiyo maana hata matajiri hufariki.

Je unahitaji dawa ya asili ya kutibu fangasi ukeni? Kama ndiyo nipigie simu 0714800175

MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:

Zingatia dawa peke yake haitofaa kitu bila kuzingatia ushauri au masharti mhimu yafuatayo:

1. Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
2. Tumia zaidi vyakula vyenye vitamini B, C, D na E
3. Tumia sana matunda hasa machungwa, limau, ndizi na vitunguu
4. Punguza vyakula vyenye wanga
5. Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
6. Epuka mapenzi kinyume na maumbile
7. Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
8. Usitumie chokoleti na vitu vingine vya namna hiyo
9. Kuwa na mpenzi mmoja tu
10. Pendelea kujiweka msafi muda wote
11. Oga maji ya moto
12. Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
13. Acha vilevi
14. Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko

MHIMU: Kama unahitaji USHAURI TU niandikie hapo kwenye comment nitakujibu, nipigie simu ikiwa tu unahitaji dawa toka kwangu moja kwa moja.

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Fangasi ukeni na tiba yake Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 150
Categories: P.I.D

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *