Hadithi 15 za uongo kuhusu kushika ujauzito

Published by Fadhili Paulo on

Hadithi 5 za uongo kuhusu kushika ujauzito

Huenda umesikia hadithi fulani kuhusu jinsi ya kupata mimba au jinsi ya kuhakikisha hupati mimba.

Kwa kweli, mbinu ya hakika ya kutopata mimba ni kutofanya mapenzi. Kutofanya mapenzi pia kutakuzuia kupata magonjwa ya zinaa.

Watoto hutengenezwa wakati mbegu za kiume zimekutana na yai la mwanamke. Wakati mume na mke wanafanya mapenzi, mbegu za kiume huogelea kutoka kwa mwili wake hadi kwa mwanamke.

Wanawake wengi na wasichana wana mahali maalum miilini mwao panapoitwa tumbo la uzazi. Mbegu zile za kiume huogelea hadi pale.

Kama kuna yai pale, basi mtoto anaweza kutengenezwa.

Linapokuja suala la kushika mimba au ujauzito, hapakosekani maneno mengi ya jinsi ya kupata mimba au namna za kuharakisha upatikanaji mimba.

Unaweza ukawa umesikia mengi sana, na wakati mwingine ukashindwa kujua lipi sahihi na lipi si sahihi. Mitazamo hii imesambaa sehemu mbalimbali duniani.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka

Sasa kwa vile unajua masuala ya kimsingi, hapa ni uongo kuhusu mimba ambao hufai kuamini kamwe.

Hadithi 15 za uongo kuhusu kushika ujauzito

1. Msichana hawezi kupata mimba kama ni mara yake ya kwanza kufanya mapenzi

Mradi msichana ameanza kupata hedhi zake, anaweza kupata mimba. Haijalishi kama ni mara yake ya kwanza au ya hamsini.

2. Msichana hawezi kupata mimba wakati wa hedhi

Mbegu za kiume zinaweza kukaa ndani ya mwili wa msichana hadi siku 5. Msichana akifanya mapenzi mwishoni wa hedhi yake, anaweza kupata mimba.

3. Msichana akioga punde tu baada ya kufanya mapenzi hatapata mimba

Mbegu za kiume huogelea hadi ndani ya mwili wa msichana. Hakuna idadi ya kuoga itakayoweza kuitoa.

4. Msichana akiruka juu baada ya kufanya mapenzi hatapata mimba

Punde mbegu za kiume ziko ndani ya mwili wa msichana, kuruka juu hakutafanya zitoke nje.

5. Wewe ni mchanga sana kupata mimba

Pindi msichana anapoanza hedhi zake, ana uwezo wa kupata mimba. Haijalishi ana umri wa miaka ngapi.

Kama una maswali zaidi au wasiwasi kuhusu kupata mimba, zungumza na mtu kwenye kliniki. Wanaweza kujadiliana nawe kuhusu mbinu mbalimbali za kupanga uzazi.

Uamuzi wa kufanya mapenzi unahitaji kufikiriwa kwa makini. Zuia kushinikizwa au kukimbilia uamuzi utakao jutia.

6. Kuna Mitindo ya Kufanya Mapenzi Inayosaidia Kupata Mimba Haraka.

Hapana, hakuna mitindo ambayo inaweza kusababisha kupata mimba haraka zaidi ya mingine. Mbegu za mwanaume hufikia mirija ya uzazi dakika chache baada ya kumwagwa billa kujali aina ya mtindo wa mapenzi mliokuwa mnafanya.

7. Ukifanya Mapenzi Kila Siku Unaweza Kupata Mimba Kirahisi.

Ingawa kufanya mapenzi kila siku kunadhaniwa huongeza uwezekano wa kupata ujauzito, ukweli ni kwamba kipindi ambacho yai la kike linatoka (ovulation) ndio jambo hili linawezekana pekee. Siku zingine hata kama ukifanya mara 10 kwa siku hauwezi kupata ujauzito.

8. Ukifanya mapenzi siku chache kabla au baada ya hedhi unaweza kupata ujauzito.

Unaweza kupata ujauzito siku ya 11 mpaka ya 17 kama mzunguko wako ni wa siku 28. Hizi ndio siku yai linakuwa linakaribia kutoka au limetoka (ovulation).

Hivyo mbegu za mwanaume zinaweza kukutana nalo na kulirutubisha ili ujauzito utungwe.

Uwezekano wa kupata ujauzito siku chache kabla au baada ya hedhi upo ila ni kwa kiasi kidogo sana.

9. Lazima Mwanamke Afike kileleni Ili Mimba Itunge

Sio lazima mwanamke afike kileleni (orgasm) ili mimba iweze kutungwa. Ingawa kitendo cha mwanamke kufikishwa kileleni husaidia kwa kiasi fulani mbegu za mwanaume kusafiri haraka kwenda kwenye mirija, lakini sio lazima hili litokee ili kutunga mimba.

10. Mtoto Atafanana na Mzazi Atakayekuwa Anampenda Sana Mwenzake Wakati wa Kufanya Mapenzi

Maumbile ya mtoto hurithiwa kutokana na vinasaba vinavyotokana na yai la mama na mbegu za baba. Mihemko ya kimapenzi huwa haiathiri muonekano wa mtoto.

11. Ukiwa Unanyonyesha Mtoto Haupati Mimba

Kunyonyesha mtoto hasa miezi 6 ya mwanzo kunaweza kuzuia usipate mimba. Lakini sio kwa asilimia 100. Tafiti zinaonesha kuna wanawake wanaopata mimba ingawa walikuwa wakinyonyesha watoto wao vizuri kila siku.

Vizuri uchukue tahadhari ya njia ya kuzuia mimba.

12. Kuinua Miguu Juu Baada ya Kufanya Mapenzi Husaidia Mimba Kutunga.

Sio kweli. Ukweli ni kwamba mbegu za mwanaume zinaweza kuogelea zenyewe kwenye via vya uzazi vya mwanamke kuelekea kwenye mirija ili kutunga mimba hata kama umesimama!

Hivyo usijichoshe kwa kuinua miguu baada ya mapenzi.

Hili pia linajibu swali ambalo baadhi huuliza eti mbona nikimaliza tendo la ndoa na mke wangu mbegu zinatoka nje ya uke wake je inaweza kuwa ndiyo sababu ya ujauzito kutotunga?.

Ni mbegu 1 tu inahitajika ili kutungisha ujauzito. Mbegu karibu zote hutoka nje ya uke wa mwanamke baada ya tendo wakati atakapoenda kuoga au kujisafisha baada ya tendo, hivyo ukiona mbegu zinatoka ukeni baada ya tendo hilo halizuii ujauzito usitungwe.

13. Kula Viazi au Soya Utapata Mimba ya Mapacha

Hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha madai haya. Kwa kifupi sio rahisi kabisa kupanga upate ujauzito wa mapacha au kuchagua jinsia ya mtoto.

14. Kunywa Dawa ya Kifua ya Maji (Cough Syrup) Inasaidia Kupata Mimba

Kwa muda mrefu watu wengine wamekuwa wakiamini mwanamke akinywa dawa ya kifua ya maji (cough syrup) inasaidia kutunga mimba. Hii ni kutokana na guaifenesin, kemikali inayopatikana katika dawa hizo, kudhaniwa kurahisisha shahawa zisafiri kwa urahisi katika shingo ya uzazi. Lakini hakuna tafiti ambazo zimeonesha kuwa hii ni kweli.

15. Kutumia Vidonge vya Majira (Kuzuia Mimba) kwa Muda Mrefu Husababisha Kuchelewa Kushika Mimba

Vidonge vya kuzuia mimba huwa vina homoni za kutengenezwa ambazo hufanya kazi kama homoni za kawaida mwilini.

Unapoacha kutumia dawa hizi uwezewako wa kupata mimba unapokuwa bado upo palepale lakini kwa uzoefu wangu wengi wanachelewa kubeba mimba kwa mda mrefu.

Nimepata kesi za wagonjwa ambao wanachukua zaidi ya miaka 6 kabla kuweza kushika mimba tena.

Naam naweza sema zinachelewesha mimba kutungwa kwa baadhi ya wanawake lakini hakuna utafiti wa kuthibitiisha ila kwa uzeofu wangu naona inachelewesha mimba kutunga kwa baadhi ya wanawake.

JE UMEJARIBU KWA MIAKA MINGI KUPATA MIMBA BILA MAFANIKIO?

DAWA YA ASILI KWAAJILI YA KUTUNGA MIMBA NA KUZUIA KUPOROMOKA KWA MIMBA (CONCEIVE & STOPPING MISCARRIAGE) INAPATIKANA SASA.

Dawa yangu kwa ajili ya uzazi itakusaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kufungua mirija iliyoziba au kuyeyusha uvimbe wowote utakaopatikana katika njia au mfuko wa uzazi kama (fibroid, cyst, endometriosis) na kukuondolea maumivu wakati wa hedhi, husaidia kuweka sawa vichocheo (hormone) pia husaidia kurutubisha mayai ya mwanamke na kupelekea kutunga mimba kirahisi na haraka, hukuondolea magonjwa ya uke kama chango, na kukuacha salama na dawa haina madhara yoyote mabaya.

Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Hadithi 15 za uongo kuhusu kushika ujauzito 1

Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto

Naitwa Fadhili Paulo ni Tabibu wa Tiba Asili. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 563

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *