Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kufunga kula?

Published by Fadhili Paulo on

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kufunga kula?

Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…

Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, mwenye neema nyingi kwa kuendelea kunipa afya njema na uhai mpaka leo.

Ni kwa neema tu tunaishi na kula.

Mwaka huu umeonekana kuwa ni mwaka wa tofauti ukilinganisha na miaka mingine hasa linapokuja suala la kufunga na ramadhani.

Sote tunashuhudia wakati wakristo wakiendelea na mfungo katikati ya mfungo huo na waislam nao wameingia kwenye mfungo wa ramadhani na hivyo kufanya wote kuwa kwenye kufunga kwa pamoja.

Wakati kwa upande wa wakristo kufunga kuna maana nyingi zaidi ya kuacha tu kula, kwa waislam kufunga ni kuacha kabisa kula na kunywa chochote.

Kwa wakristo siyo lazima kuacha kabisa kula na kunywa vyote, kwa mfano kama wewe ni mlevi unaweza kuamua kufunga ulevi tu na chakula ukala.

Sasa kama wewe ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo huenda ukawa unajiuliza ikiwa na wewe ufunge kula na kunywa vyote kama wafanyavyo wengine wenye afya zao nzuri au la.

Kwa bahati nzuri baada ya kusoma soma huko na huko nimeona kumbe hata uislam haulazimishi mgonjwa kufunga kula.

Kwahiyo kama unaumwa vidonda vya tumbo ni vema usifunge kula au kunywa.

Kwanini hasa usifunge kula ni kwa sababu kufunga kula kunaweza kuongeza zaidi maumivu ya vidonda vya tumbo na kufanya kupona kwako kuwa ni jambo gumu.

Unaweza kupunguza kidogo kiasi unachokula na utumie vile anavyokubariki Mungu kusaidia watu wengine wenye mahitaji maalumu kama yatima, walemavu, wazee wasiojiweza nk

Unaweza kujitolea kufanya kazi yoyote kwa ajili ya jamii kama kwenda kufanya usafi maeneo ya hospitali, kupeleka cement au madawati shuleni nk

Kumbuka kwa sehemu kubwa tunaokolewa kwa neema na siyo kwa matendo yetu au jambo fulani zuri tumefanya, ni Mungu tu ndiyo anatuhurumia, anaturehemu na kutusamehe.

Kwa hiyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo usifunge kula.

Na wakati huu tende zikiwa nyingi mitaani usisahau na wewe kula tende 2 kutwa mara 3 kila siku.

Tende (dates)

Na mhimu kuliko yote ni kuwa lengo langu ni ifike wakati upone kabisa vidonda vya tumbo na visiwe ni sehemu ya maisha yako kila siku kila mwaka.

Hakuna sababu ya kuendelea kuuguza vidonda vya tumbo mwaka hadi mwaka.

Huhitaji kuishi na vidonda vya tumbo miaka yote.

Kama unahitaji dawa ya asili ya uhakika inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kumbuka nimeandika tuwasiliane kwenye WhatsApp.

Share post hii na wengine uwapendao

(Visited 163 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175