Je mwanaume anaweza kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wake?

Je mwanaume anaweza kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wake?

Kama wewe ni mwanaume ambaye kwa miaka kadhaa umekuwa ukitafuta ujauzito bila mafanikio huenda ukawa unajiuliza kama tatizo hili limewahi kuwepo pia kwa wazazi wako.

Unaweza kuwa unawaza huenda wazazi wako hasa baba yako anahusika kwa namna moja au nyingine na wewe kuwa na tatizo la kushindwa kutungisha mimba.

Tafiti kadhaa zimewahi kufanyika kuona kama kuna uwezekano wa mwanaume kurithi hali ya kutokuwa na uwezo wa kutungisha ujauzito kutoka kwa wazazi wake.

Kwa nyakati tofauti tafiti zinasema kuna uhusiano mdogo sana wa mwanaume kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wake.

Kuna uwezekano wa kama asilimia 1 tu ya wewe mwanaume kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wako.

Sababu nyingi au vyanzo vingi vya ugumba kwa wanaume haviwezi kuwa ni vitu vya kurithi.

Hata hivyo utafiti mmoja uliofanyika nchini Denmark unasema vijana wa kiume ambao wazazi wao wamewahi kuwa na tatizo la kushindwa kutungisha mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja walionekana kuwa na tatizo la kuwa na mbegu chache (low sperm count) na mbegu chache zenye muonekano wa mbegu nzuri na zenye afya.

Lakini utafiti huo ulihusisha kundi dogo sana la watu na hivyo bado hakuna hitimisho la moja kwa moja kama mwanaume anaweza kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wake.

Utafiti mwingine uliowahi kufanyika nchini Ufaransa uliona kuwa kuna uwezekano fulani wa jeni (sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani) ya baba kurithiwa na mtoto.

Nao ni utafiti uliohusisha watu 300 tu.

Kwahiyo ni hali ya kawaida na ya asili kabisa kama wewe ni mwanaume ambaye unashindwa kutungisha ujauzito kuwaza kwamba labda unaweza kuwa umerithi tatizo hili kutoka kwa wazazi wako.

Na pengine unaweza kuwa unawaza kama na wewe unaweza kupata watoto wenye matatizo ya uzazi kama ilivyo kwako.

Lakini kama ulivyoona tangu mwanzo wa maelezo yangu kwamba uwezekano huo upo bali ni mdogo sana sawa na hakuna.

Huenda kuna aina fulani ya maisha (life style) waliyokuwa wakiishi wazazi wako umeirithi hasa kwenye kula, kunywa na maisha yao ya kila siku ambayo inaweza kupelekea mtu mgumba.

Lakini kwamba kuna namna ya kijenetiki ya moja kwa moja kutoka kwa wazazi wako kuja kwako inayoweza kuwa ndiyo sababu ya wewe kuwa mgumba bado hakuna hitimisho katika tafiti zilizofanyika tayari na zinazoendelea kufanyika.

Kwahiyo acha kuwa na wasiwasi kuhusu hali yako na uhusika wa wazazi wako, na mhimu kuliko yote ni kuwa wao kama wazazi walifanikiwa kukupata wewe na wakakulea mpaka sasa umekuwa mtu mzima.

Kama wewe ni mwanaume na umekuwa unapata wakati mgumu linapokuja suala la kutungisha ujauzito na unataka kujitibu kwa kutumia njia za asili niachie ujumbe wako kwenye WhatsApp +255714800175 ukinieleza namna hasa tatizo lilivyo, lina muda gani sasa, umri wako na mahali ulipo.

Share post hii na wengine uwapendao.

Je mwanaume anaweza kurithi ugumba kutoka kwa wazazi wake?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Scroll to top
WhatsApp WhatsApp +255714800175