Je punyeto inasababisha ugumba kwa wanaume?

Published by Fadhili Paulo on

Je punyeto inasababisha ugumba kwa wanaume?

Nimeshaandika mengi sana kuhusu punyeto au kujichua kwenye hii blog.

Mengi sana.

Nimeshaandika madhara ya punyeto kwa jinsia zote mbili.

Punyeto ni kitendo cha mtu akiwa peke yake kulazimisha hisia zake huku akitumia mkono na vifaa vingine kama sabuni, mafuta, picha, midori (toys) na video ili kufika kileleni.

Wakati ugumba ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo kabisa wa kuweza kumpa ujauzito mwanamke.

Kila mara mwanaume anapofanya punyeto mwisho wake mbegu humtoka na hivyo hujisikia vizuri kama vile ameshiriki tendo la ndoa na mwenza wake, lakini hapa anakuwa yupo peke yake.

Nguvu zaidi za kiakili na kimwili zinahitajika ili mtu atimize lengo hili.

Tambua kwamba punyeto ya mara moja au mara mbili kwa mwezi haina madhara yoyote mabaya kwa afya ya mwanaume.

Shida iliyopo ni kuwa punyeto ni kama kilevi na ina kawaida ya kumfanya mtu kuwa mtumwa wa jambo hilo.

Kwa sababu hii wapo wanaume ambao hawawezi kupitisha siku bila kujichua na wengine wanaweza kufanya hivyo mara mbili au hata mara tatu kwa siku.

Inajulikana wazi kwamba kitu chochote kikizidi huwa kinaleta madhara.

Kwa lugha ya watu wa pale Mbeya wanasema ‘too much of anything is harmful‘.

Kwahiyo kama umekuwa ukijiuliza ikiwa punyeto inaweza kukuletea shida ya wewe mwanaume kwenye kumpa ujauzito mwanamke, jibu la haraka la swali hili ni HAPANA.

Punyeto ya mara moja moja haina uwezo wa kukufanya kuwa mgumba.

Kumekuwa na mabishano juu ya jambo hili kwa miaka mingi na tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika hazijawahi kuwa na jibu moja linaloeleweka.

Hivyo kama wewe ni mpiga punyeto uliyepitiliza, yaani unapiga sana punyeto kupita kiasi basi tambua kwa namna moja au nyingine kitendo hicho kinaweza kuwa moja ya sababu zinazoweza kukupa ugumba.

Ili kuwa na mbegu bora na zenye afya mwanaume anashauriwa kutozitoa kwa siku mbili au tatu.

Kama una tabia ya kujichua kila siku kuna uwezekano mkubwa ukapata tatizo la kuwa na mbegu chache (low sperm count) la muda mfupi (temporary).

Hivyo punyeto inaweza kukuletea ugumba kama matokeo ya kuwa na mbegu chache tatizo ambalo siyo la kudumu kwani ukikaa bila kupiga punyeto kwa siku 3 baadaye wingi wa mbegu zako utarudi kama kawaida.

Kama hilo halitoshi ni kuwa unapojichua mwili wako unachoka sana mara mbili au hata mara tatu zaidi tofauti na vile ungeshiriki na mwanamke.

Kama wewe ni mtu wa uchovu mwingi kila siku itakuwa vigumu kumpa mwanamke ujauzito.

Kwa kumalizia kujibu swali ni kuwa punyeto kama punyeto haiwezi kukufanya wewe kuwa mgumba bali punyeto ya kuzidi inaweza kuleta shida ya muda mfupi ya mwanaume kushindwa kumpa ujauzito mwanamke kama matokeo ya mbegu kuwa chache.

Kama wewe na mkeo mmekuwa mkihangaika kwa muda mrefu kutafuta mtoto, ushauri wangu kwako ni kuwa usijihusishe na kupiga punyeto kwa namna yoyote ile.

Na ikiwa tatizo bado linaendelea hata baada ya miezi kadhaa ya wewe kuacha kujichua basi ni vema kufika hospitali wote wawili wewe na mkeo kwa vipimo na uchunguzi zaidi

Ikiwa unahitaji dawa ya asili inayosaidia kutibu matatizo ya uzazi kwa mwanaume niachie tu ujumbe WhatsApp 0714800175

Share post hii na wengine uwapendao

(Visited 251 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175