Je ukubwa wa uume una umhimu wowote kwenye mahusiano

Published by Fadhili Paulo on

kuongeza uume

Je ukubwa wa uume una umhimu wowote kwenye mahusiano?

Wanaume nao hufuatilia fuatilia kuhusu miili yao kama vile wafanyavyo pia wanawake.

Maswali kama je mimi ni mnene sana? ni mrefu? ni mwembamba? ni mfupi? je nikipita barabarani naonekana nimependeza na nadhifu? ni maswali ya kawaida kwa wanaume wengi.

Ndiyo; wanaume wanapenda pia waonekane wamependeza, ndiyo maana wananunua nguo nzuri, wananyoa nywele wengine wanaenda mbali mpaka wanasuka nywele na kuvaa heleni kama vile wanawake ili tu waonekane tofauti na wamependeza.

Hata hivyo kitu pekee wanaume wengi hupenda kufuatilia ni juu ya ukubwa na uimara wa mashine zao.

Hilo ndiyo namba moja linalokuja kichwani kwa mwanaume yoyote.

Wanaume wanapenda sana kufahamu kuhusu mheshimiwa wao (mashine), yaani mheshimiwa wake anaonekanaje mbele ya mwanamke?

Maswali kama uume wangu ni mkubwa? unatosha? naweza kuuongeza kidogo? ni maswali ya kawaida kwa wanaume karibu wote.

Sasa swali la leo ni hili > Je ukubwa wa uume una umhimu wowote kwenye mahusiano?

Jibu langu ni kuwa : ‘Ndiyo ukubwa wa uume wako una umhimu kwenye mahusiano yako’.

Lakini siyo kwa kiwango na kiasi kile wanaume wengi wanafikiri.

Ni kweli kabisa unahitaji kuwa na uume mkubwa na ambao ni imara ila siyo kwa kiwango kile wengi wenu mnafikiri.

Nitaeleza na utatakiwa kuwa makini ili kunielewa.

Kwenye utafiti mmoja uliowahi kufanyika nchi fulani huko Ulaya ambao ulikuwa unawahoji wauzaji wa uume wa kutengenezwa (toy, au uume bandia) ilibainika kwamba wateja wengi (ambao ni wanawake) wanaokwenda kununua hizo bidhaa wengi wao huagiza uume wenye urefu wa kati ya inch 5 mpaka 6 na inch 6 ndiyo ulikuwa unaongoza kupendwa na wateja wengi.

Kwa hapa kwetu Tanzania ni vigumu kuyaona wazi wazi haya maduka ingawa kuna uwezekano yapo!

Kwa mtu ambaye ni mgeni ni kuwa kuna uume wa kutengenezwa wengine huita sex toy na mara nyingi hutengenezwa kwa kutumia plastiki maalumu na unakuwa na muonekano sawa na ulivyo uume wa kawaida na yapo maduka yanayouza na kwa huko Ulaya ni jambo la kawaida.

Upo pia uke wa kutengenezwa (bandia).

Kuna watu hawataki uhusiano na mtu yoyote na huchagua kununua vitu kama hivyo ili kumaliza haja zao.

Ni kama vile kujipiga punyeto au kujichua lakini ukitumia kiungo cha siri cha kutengenezwa.

Vina faida na madhara yake lakini kwa leo hiyo siyo mada hasa ninayotaka kuizungumzia.

Kwa hiyo wauzaji wa mashine hizo bandia walipohojiwa wengi walikiri kuwa wanawake wengi wanaofika kwenye maduka hayo huagiza uume bandia wa inch tano mpaka sita na wengi zaidi wanapendelea wa inch 6.

Wapo wanaoagiza wa inch 7 au 8 wengine wa inch 4 au 5 lakini ilibainika wazi inch 6 ndiyo saizi inayopendwa na wengi zaidi.

Kama wewe ni mdadisi, kama wewe ni mtu usiye na aibu ukikaa na wanawake kadhaa kwa upole na taratibu ukawahoji kuhusu hili wengi watakupa jibu kuwa ndiyo wanapenda mwanaume mwenye uume mkubwa.

Ndiyo sababu wanawake wengi wanapenda kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume ambaye ni mrefu na ana afya yake nzuri.

Linapokuja suala la uzuri kwa mwanaume urefu ni sifa inayoongoza kutakwa na wanawake wengi.

Ukiacha imani yao ambayo haina uthibitisho kwamba mwanaume akiwa mrefu atakuwa na mashine ya kutosha pia wanawake wanasema mwanaume mrefu ana uwezo mkubwa wa kujiamini

Ndiyo; wanawake wanapenda mwanaume anayejiamini na anayeweza kuonyesha dalili ya kuwa mlinzi mzuri kwao.

Kama nilivyosema pale mwanzo kuwa ni kweli uume mkubwa una umhimu wake kwenye mahusiano lakini siyo kwa kiwango kile wengi mnafikiri na kutaka iwe.

Kuwa na uume mkubwa tu halafu hujuwi namna ya kuutumia vema ni shida kwa mke wako na pengine inaweza kuwa ndiyo sababu akaamua kuvunja hata uhusiano wenu.

Ndiyo, wanawake wanapenda uume mkubwa lakini siyo mkubwa sana kupitiliza kwani unaweza kuharibu kizazi chake iwapo mwanaume huyo hajuwi namna nzuri ya kutumia uume wake mkubwa.

Uume mkubwa sana maana yake unahitaji maandalizi ya kutosha kabla ya kumwingilia mwanamke, ni lazima awe amesisimka vya kutosha na ana unyevunyevu; tofauti na hapo ni maumivu makali, ni kero, ni shida, ni kama adhabu fulani hivi na ambayo inahatarisha usalama wa afya ya kizazi kwa mwanamke.

Kwahiyo kama unapanga kuwa na uume mkubwa basi malengo yako yawe ni kufikia inch 6 na ukizidi sana basi uwe si zaidi ya inch 7.

Pamoja na hayo yote bado wanawake wengi pia hawafurahii kuwa na mahusiano na mwanaume mwenye uume mdogo sana.

Hilo lipo wazi na hadi wametutungia majina wanaume wa namna hii wanatuita timu vibamia.

Uume ukiwa na udogo hasa urefu wa chini ya inch 4 ni kero kwa wanawake wengi.

Hawapendi na ukimpata chizi anaweza kukuambia kabisa wazi wazi kwamba hasikii chochote.

Kwa hiyo ukubwa wa uume wako una umhimu wake ingawa siyo kwa kiwango kile wanaume wengi wanafikiri.

Kabla ya kumaliza labda nitoe ushauri kidogo kwa wanawake ambao kwa bahati mbaya wanaolewa na wanaume wenye uume mdogo sana.

Ikitokea umeolewa na mwanaume mwenye uume mdogo sana kwanza kabisa kama unaweza jitahidi kutomuambia lolote kuhusu hilo.

Usijaribu.

Tena wanawake wajanja wa mjini yaani wale wenye akili zao hata uwe na uume mdogo yeye atakusifia tu una uume mzuri na unamfaa sana yeye.

Hana muda huo wa kukaa kupeleleza au kuwaza kuhusu ukubwa wa uume; ana mipango yake mingine ya mhimu na wewe zaidi ya uume wako.

Kwa hiyo ikitokea umepata mwanaume ana uume mdogo jaribu kuangalia kama ana vitu vingine mhimu zaidi kwako kuliko uume.

Mwangalie je ni mtu anayejali? ana upendo wa dhati? anakutimizia mahitaji yako mengine ya mhimu? ana hofu ya Mungu? anakudekeza kama mtoto mdogo?.

Ni hatari kuwa na mwanaume mwenye uume mkubwa halafu ana mdomo mchafu yaani anaropoka tu maneno ya hovyo, hakujali, anakuchukulia poa, hakupi chochote, anafanya fujo na nguvu nyingi unaposhiriki naye tendo la ndoa utadhani hana kazi zingine za mhimu hapa duniani.

Kama vile mara nyingi huwa napenda kusema hela ni kitu cha mhimu lakini hela siyo kila kitu katika maisha kadharika napenda kumaliza kwa kusema uume mkubwa na ambao ni imara ni wa mhimu kwenye mahusiano lakini uume tu peke yake siyo kila kitu kwenye mapenzi.

Kuna mengi kwenye maisha ya ndoa zaidi ya uume.

SHARE POST hii na wengine uwapendao

Je ukubwa wa uume una umhimu wowote kwenye mahusiano? Click To Tweet

Kabla hujaondoka soma pia na hii 👇

Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

(Visited 949 times, 1 visits today)

2 Comments

Lazaro · 21/07/2021 at 9:15 am

I have a weak penis(sina nguvu za kiume)

    Fadhili Paulo · 22/07/2021 at 7:04 am

    Tuwasiliane Lazaro

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175