Je wanawake huwa wanataka mwanaume adumu muda gani kitandani

Published by Fadhili Paulo on

Je wanawake huwa wanataka mwanaume adumu muda gani kitandani

Watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba mwanaume anapochelewa sana kufika kileleni basi ndiyo tendo la ndoa linakuwa tamu jambo ambalo si kweli.

Umekuja hapa ukitafuta jibu la swali hili na usijifikirie upo peke yako ambaye umekuwa ukitaka kujuwa jibu la swali hili – ni wengi wamekuwa wakiniuliza mara kwa mara na leo nimeona niwatolee uvivu niwajibu wote kwa kirefu

Nikuambie tu mapema huwezi kuipata elimu kama hii popote shuleni wala chuoni ila hapa kwa bahati nzuri umeipata na unaweza kunizawadia chochote ikiwa maelezo haya yatakusaidia kuboresha maisha yako kwa namna moja au nyingine.

Tafiti mbalimbali zinasema wastani wa karibu ya zaidi ya asilimia 90 ya wanaume kote duniani hufika kileleni ndani ya dakika 2 mpaka 3.

Wapo baadhi ya wanaume wao wanawahi sana kiasi huwezi kuamini.

Yaani ni sekunde kadhaa tu tayari wazungu hao.

Na wengine wanadai yaani kile kitendo cha kumkumbatia tu mwanamke na kuhisi joto lake tayari ameshakojoa na mbaya zaidi hawezi kusimama tena mpaka kesho!

Hapa tunazungumzia muda ule ambao tayari kitendo kimeanza kufanyika kama ni kifo cha mende basi tayari mzee yupo juu ya ulingo!

Hatuhesabu muda wa maandalizi (foreplay).

Wanawake wengi wanajali sana muda wa maandalizi kuliko muda wa tendo lenyewe.

Kama unaweza kutumia dakika 40 kumuandaa mwanamke na ukamwingilia kwa dakika 10 kwake hapo utakuwa umefanya jambo la maana zaidi kuliko ungemwandaa dakika 10 na kumwingilia kwa dakika 40.

Wanawake ni watu wa hisia na ni jukumu lako kuhakikisha hisia zake zipo sehemu sahihi.

Je wanawake huwa wanataka mwanaume atumie muda gani kitandani?

Jibu la haraka ni kuwa wanawake wanapenda mwanaume atumie muda usiopungua dakika 13 katika tendo la ndoa.

Unaweza ukashangaa kusikia hivi na ukisoma dakika 13 unaweza kufikiri ni chache lakini ni nyingi sana hizo katika ule mchezo.

Kwa kawaida mwanaume anapoanza uhusiano mpya na mwanamke mpya anakuwa na hamasa na nguvu na shauku nyingi ya kutaka kushiriki naye tendo la ndoa lakini kwa bahati mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda ndani ya huo uhusiano pole pole mwanaume huanza kupungua hiyo shauku na tamaa.

Ndiyo sababu watu wa jinsia zote mbili tunahimizwa ubunifu na kutafuta mbinu mpya kila mara katika uhusiano ili kuleta hamasa zaidi katika kitengo hiki cha kitandani.

Kwahiyo kinamama mliopo kwenye ndoa miaka mitano au kumi au zaidi msije mkafikiri mwanaume wa uchumba ndiyo mwanaume wa kwenye ndoa, hapana hapo utakuwa umechemka ndoa haiendi hivyo.

Kumbuka wakati wa uchumba hakuwa na majukumu kama aliyonayo sasa kwahiyo nguvu zake na vipaumbele vyake haviwezi kuwa sawa sasa na wakati ule wa uchumba au wakati mnaanza tu maisha ya ndoa.

Kuna uwezekano wakati wa uchumba mwanaume akawa na nguvu sana wakati wa tendo la ndoa na uwezo huo ukashuka hata zaidi ya nusu miaka kadhaa baadaye baada ya ndoa.

Miaka mitano au kumi baada ya ndoa kuna uwezekano mna mtoto au watoto tayari na ni jukumu kuu la baba kuhakikisha watoto wanakula vizuri, wanalala sehemu nzuri, wanaenda shule, wanaandaliwa pesa ya matibabu pembeni na kadharika.

Majukumu yote hayo humuondolea mwanaume hamasa, nguvu na uwezo wake wa awali wa kushiriki tendo la ndoa.

Kwahiyo ni jambo la kawaida kwa mwanaume kupungua uwezo wake wa awali wa kushiriki tendo la ndoa miaka kadhaa baada ya ndoa. Ni jambo la kawaida mwanamke mwenye akili tambua hilo na uishi kwa adabu na mmeo.

Ukiacha majukumu kuongezeka ni kwamba mwanaume anaona wewe mkewe upo hapo kila siku masaa 24 akikutaka anakupata muda wowote.

Sasa hiyo lazima itampungumzia hamasa tofauti na mwanzo mkiwa wachumba ulipokuwa unampa kwa nadra au mara chache tena kwa kuibana.

Kwa sasa anayo yote hapo hapo kwanini atumie nguvu nyingi wakati na baadaye na baadaye tena na baadaye tena na kesho ipo hapo hapo inamsubiri.

Kwahiyo wanaume wengi zaidi ya asilimia 90 wanafika kileleni ndani ya dakika 2 mpaka 3 dunia nzima siyo hapa Tanzania tu.

Utafiti mmoja uliofanywa na jarida liitwalo Journal of sexual medicine mwaka 2005 uliowahoji wataalamu wengi wa elimu ya tendo la ndoa (sex therapists) ulibaini kuwa wanawake wanachukulia muda mwanaume anaoweza kushiriki tendo la ndoa katika makundi yafuatayo:

a)Dakika 1 mpaka 3  > ni muda mchache mno. Lazima atakudharau

b)Dakika 3 mpaka 7 > muda wa wastani. Anakuona una afya

c)Dakika 7 mpaka 13 > Muda mzuri kwao. Anafurahi na kukuheshimu

d)Dakika 13 mpaka 25 > Muda MZURI SANA lazima atakuwa anakupa zawadi mara kwa mara

e)Dakika 25 kwenda juu > muda mrefu sana na ni kero kwao na anaweza kusitisha mahusiano na wewe.

Wanawake wengi wanaweza kuwa wamefika kileleni muda wowote kuanzia dakika ya 8 kwenda juu tangu uanze kumwingia (siyo kumuandaa).

Kwahiyo chochote chini ya dakika 7 kuna uwezekano mkubwa ukamuacha njiani na asifurahie chochote.

Kuna jamaa anataka kucommnet hapo chini kuwa huwa anaenda dakika 40 au 60 vizuri tu kwahiyo mimi niache uongo.

Ni kweli unaweza kuwa upo sahihi hasa kama unashiriki tendo la ndoa na wanawake wasiojitambuwa wala hawajuwi thamani yao.

Mwanamke anayejitambuwa na kujuwa thamani yake haweza kukubali uende dakika 40. Atakumabia tu hapana imetosha hapo basi. Ila yule asiyejitambua atakaa tu kimya kukusubiri wewe umalize kulima shamba muda wote huo utadhani huna kazi zingine za mhimu za kufanya.

Kuna wanawake wa aina mbili. Wanawake wanaojitambua na wasiojitambuwa.

Wasiojitambua ukimwambia geukia huku anageuka, pandisha kule anapandisha, zunguka hivi anazunguka yaani lolote utakalomwambia au kumfanya yeye sawa tu hata kama anaumia.

Wanaojitambuwa hawezi kukubali kila unachomwamuru. Vingine atakuambia mhhh hapana mzee hilo siwezi au hilo hapana.

Kwahiyo kama huwa unaenda dakika 40 au 60 au masaa mawili huenda huwa umekutana na wale aina ya pili – wasiojitambuwa wala kujuwa thamani yao.

Hata wale wanawake wanaojiuza ukizidisha sana muda anakuambia wazi utaongeza hela au kama inashindikana chukua hela yako ondoka usinipotezee mimi muda!

Wanaume mtambuwe kila goli moja unalopiga unatoa mbegu Zaidi ya milioni 200 toka mwilini mwako na tendo hilo linauchosha sana mwili wako kuliko mwili wa mwanamke.

Ndiyo sababu wanaume wengi hutangulia kufa kabla ya wanawake.

Goli moja ni sawa na kazi ya kutembea kwa miguu kilomita 27.

Kwahiyo utaona wazi ni jinsi gani ukiendekeza tendo hilo unavyoweza kujidhuru afya yako bila mwenyewe kujuwa.

Wanawake ni watu wa hisia, kuwa bize zaidi kujenga hisia zake na siyo kutaka kushiriki naye tendo la ndoa na mtu hayupo hapo kifikra.

Na baadhi ya wanaume wana akili ndogo sana eti huwa wanawaza wanaweza kumkomoa mwanamke wakati wa tendo la ndoa kwa kufanya muda mrefu na kwa nguvu utadhani ugomvi wakati ni starehe.

Tambua huwezi kumkomoa mwanamke. Unajikomoa mwenyewe.

Unakuta mwanaume anatumia vilevi vikali na vyenye kuharibu afya yake na mwingine yupo bize kumeza vidonge vya kizungu ili tu eti akamkomoe mwanamke kitandani!

Huwezi kumkomoa mwanamke, unajikomoa mwenyewe na wewe ndiyo utaharibikiwa afya yako ukiendelea na huo ujinga.

Kumbuka wewe mwenyewe umezaliwa na mwanamke sasa sijuwi una ukubwa gani wa kumshinda mtoto anayezaliwa!

Shida moja ya baadhi ya wanaume wanaposhiriki tendo la ndoa ni kuwa wanajiwaza wao, wao wanajiona ndiyo madereva na wake zao ni abiria.

Mapenzi ni two way systems. Mapenzi ni njia mbili, wewe na yeye.

Kaa karibu na mkeo, mshirikiane mnaposhiriki tendo la ndoa, kila mmoja awe tayari na aonyeshe uhitaji na uwepo.

Usishiriki na mwenza wako tendo la ndoa, bali MSHIRIKI na mwenza wako tendo la ndoa.

Unao uwezo wa kumwambia mapema kabisa mkitaka kuanza kushiriki kwamba; ndugu mwenzio leo najiona wazi nitawahi sana hivyo usishangae.

Hakuna mwanaume anayeweza kuchelewa kila siku au kila mara atakaposhiriki tendo la ndoa. Inawezekana ana uchovu mwingi muda huo au na mawazo fulani yanamtatiza au hajapata chakula muda mrefu na kadharika.

Mwanaume kadharika mwanamke muulize mwenzio anapendaje, anatakaje, kipi kinamwamsha zaidi na kipi hapendi kabisa. Mwanaume usijichukulie madaraka na ufahamu wote peke yako.

Je wewe ni mwanaume na umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la kuwahi sana kufika kileleni kwa muda mrefu? Kama jibu ni ndiyo pata suluhisho la tatizo lako kwa kubonyeza HAPA.

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Je wanawake huwa wanataka mwanaume adumu muda gani kitandani Click To Tweet

Share na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 1,520

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *