Jinsi kuchepuka kunavyoleta tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Published by Fadhili Paulo on

Jinsi kuchepuka kunavyoleta tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Leo nitazungumzia namna kuchepuka kunavyoleta upungufu wa nguvu za kiume.

Na hii ni pale mwanaume anapogundua mkewe anachepuka.

Hapa unakuwa umefahamu na una uhakika kabisa mkeo amechepuka au anaendelea kuchepuka.

Mke anauma sana asikuambie mtu.

Ndiyo sababu ni rahisi kwa ndoa kuendelea kuwepo ikiwa mke atamfumania mme lakini ni ngumu sana kuona ndoa ikiendelea baada ya mme kumfumania mke!

Ni kwa sababu wanawake wana nguvu zaidi za kuvumilia shida na wana roho kubwa ya kusamehe.

Kwahiyo wapo wanaume waliopungukiwa nguvu za kiume au kuishiwa nguvu na hamasa ya kutaka kushiriki tendo la ndoa kwa ufasaha kama matokeo ya wake zao kuchepuka.

Siyo kila mtu mwenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hafanyi mazoezi au ni mlevi, wengine wanakutana na tatizo hili kama matokeo ya kuvurugika kwa saikolojia zao.

Kama wewe ni mke wa mtu na una tabia mbovu ya kuchepuka tambua siku mmeo akifahamu unaweza kumharibia afya yake ya kitandani na pengine kuharibu hata maisha yake.

Kinachotokea hapa ni kuwa mwanaume anaanza kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaloletwa na kuvurugika kwa saikolojia yake.

Ubongo wake unakuwa kama vile umepigwa ganzi na itakuwa vigumu kwake kuhimili tena kwa usahihi tendo la ndoa na mke wake aliyemsaliti.

Ukweli ni kuwa itachukuwa muda kwa mwanaume huyu kurudi kwenye afya yake ya kawaida kama mwanzo na kwa wengine afya hiyo inaweza isirudi tena kama hatapata mshauri mzuri ili kuibadili akili na saikolojia yake.

Mwanaume kama huyu hata akipewa dawa ya kuongeza nguvu za kiume bado hawezi kupona kwa sababu tatizo lake ni la saikolojia zaidi na siyo viinilishe au vitamini zimepotea mwilini.

Yaani mwanaume anapogundua na kujihakikishia kuwa mkewe anachepuka hiyo huwa ni habari mbaya sana kwenye maisha yake na kama ndiyo mara yake ya kwanza kumtokea wapo ambao huona bora kufa kuliko kuendelea kuishi.

Mwanaume anaona kwamba amekuwa akijitahidi kumhudumia mkewe na kumjali kwa kila kitu lakini bado mke ameshindwa kuwa mwaminifu.

Kwa hiyo lipo tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanaume linaloletwa na kuchepuka kwa mwanamke.

Mwili wa mwanaume na akili na ubongo wake na saikolojia yake vinakuwa vimepatwa na mshtuko (shock) ambayo siyo rahisi mimi kuielezea ukaielewa labda mpaka likukute mwenyewe ndiyo siku hiyo utanikumbuka vizuri nini nimeandika hapa.

Mwanaume anaweza kuishiwa kabisa hisia za kutaka kushiriki tendo la ndoa na mke wake huyo.

Wanaume wengine huishia kuwa na tabia zifuatazo ;

1. Ulevi wa kupindukia
2. Kuacha kujijari
3. Kuwa na hasira muda mwingi
4. Kuacha kujali wengine
5. Kuwa na msongo wa mawazo
6. Akili kutokutulia
7. Kufanya maamuzi yenye majuto baadaye
8. Kukosa usingizi
9. Kukosa kabisa utulivu
10. Kuvurugika kihisia

Wapo Wanaume waliowahi kuchukuwa maamuzi magumu na mwisho kuishia gerezani au hata kufa.

Nini kifanyike sasa katika hali kama hii ili upone tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya kusalitiwa na mkeo?

Unaweza kufanya yafuatayo na ukabaki salama;

1. Omba rehema ya Mungu.

Omba nguvu ya kusamehe na kuachilia yaani kusahau hasa kama una lengo la kuendelea kuishi na mkeo.

Tafuta kujua sababu hasa ya mkeo kuchepuka.

Mara nyingi hakuna tatizo linalotokea bila sababu na huenda wewe mwenyewe ndiyo chanzo cha mkeo kuchepuka labda umekuwa humjali, hupo naye karibu muda mwingi, unamdharau na inawezekana pengine humpi huduma ya kitandani kama inavyostahili.

Kwahiyo kabla ya kuhukumu ruhusu Mungu akupe hekima na macho ya rohoni juu ya tatizo.

Kumbuka Mungu hutusamehe sisi bila kujali tumekosa nini lakini tunapotubu mara moja anatusamehe na kusahau.

Kama una moyo mkubwa na upo tayari kuendelea kuishi na mkeo, msamehe tu na ikiwa ameapa kwa maneno na vitendo kuwa hatarudia tena kosa hilo msamehe na umwachilie moyoni na safari hii jitahidi kuwa naye karibu zaidi.

2. Jali afya yako sasa kuliko wakati mwingine wowote.

Badala ya kugeuka na kuwa mlevi au usiyejali wala kujijalj, sasa ndiyo wakati wenyewe wa kujali afya yako na Kujipenda mwenyewe zaidi.

Kama unahitaji kusafiri kidogo nje ya mkoa fanya hivyo na ukae huko mpaka akili ikae sawa.

Usikurupuke kufanya maamuzi yoyote magumu kwa haraka.

Jipende mwenyewe zaidi wakati huu na uishi kama vile hakuna kilichotokea.

Haijalishi kimetokea nini, ukitulia na hilo nalo litapita.

Kwahiyo kama unahitaji muda wa kuwa peke yako kwanza fanya hivyo na umweleze pia mkeo kwamba unahitaji muda kufikiri kwa upya kuhusu maisha yako.

Kama hata baada ya muda kupita bado huna nguvu wala ujasiri wa kumsamehe mkeo ili muendelee na maisha yenu kwa amani kama mwanzo basi unaweza kuachana naye kwa siri, kimya kimya bila matangazo na bila mtu kufahamu.

Na siyo lazima ulipe visasi au utokee ugomvi.

Mathayo 1 : 19

 

19. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

Ni amani tu na upendo ili kuruhusu maisha mengine yaendelee.

Na usikae muda mrefu sana bila kuoa tena.

Tambua tatizo hilo haliwezi kupotea haraka haraka kichwani na kwa urahisi rahisi tu, lakini penye nia pana njia na hatimaye utakuwa huru tena

Jambo la mhimu hapa ni kama mkeo atakuwa tayari kukubali kosa lake, kuomba msamaha na kukubali kuacha tabia hiyo mbaya.

Kama mke hayupo tayari kubadilika itakuwa ngumu sana huu mgogoro kuisha bila madhara.

3. Omba msaada wa kimawazo

Tambua hilo siyo jambo la kwanza kukutokea wewe.

Ni jambo la kawaida na limeshawatokea wengine wengi bila kujali ni kina nani na wana nini.

Kuna wakati mambo hutokea tu maishani na unakuwa huna jinsi zaidi ya kulinda amani ya moyo wako.

Kwahiyo likikupata usione tabu kuomba ushauri na maelekezo mengine toka kwa watu wengine wakusaidie wenye umri mkubwa zaidi yako au hata kwa ndugu au wazazi wako.

Kumbuka kutotumia ushauri wowote unaopewa hasa na wazazi wako bila kuuchuja kwanza sababu wazazi lazima watakuwa na hasira sana hata kama wewe umeamua kusamehe.

Kama upo Dar Es Salaam au maeneo ya karibu na Dar Es Salaam unaweza kuja kuniona hata mimi na nitakusaidia mawili matatu juu ya kuendelea mbele.

Kama utapenda kuonana na mimi uso kwa uso kwa ushauri juu ya tatizo hili niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

4. Badili mtazamo wako kuhusu mapenzi

Mara nyingi mtazamo wetu kuhusu mapenzi ni tofauti kabisa na hali halisi ilivyo.

Kwa mfano mkiwa kwenye uchumba hakuna kiongozi wa dini, wazazi au marafiki wanaotueleza kwamba lazima tukawe tayari kwa lolote kwenye maisha hayo mapya ya ndoa.

Huwa tunasimuliwa kuhusu furaha tu za kwenye ndoa na hatuambiwi lolote juu ya upande wa pili wa shilingi.

Badili mtazamo wako kwamba lolote laweza kutokea na likitokea uweje na ufanye nini.

Wakati huo huo kinacholeta shida ya haya yote ni ile hali ya kumuamini sana mkeo kuliko hata kumpenda.

Jifunze kumpenda mkeo na siyo kumuamini.

Ukimpenda mtu siyo lazima umwamini kwa wakati mmoja.

Mpende sana mkeo, mpende sana lakini jiamini mwenyewe na Mungu wako.

Tambua hata mpendane vipi bado hamtazikwa kaburi moja au hamtakufa wote siku 1, vyovyote itakavyokuwa siku moja tu isiyo na jina lazima mtaachana hata kama ni kwa kifo.

Kwahiyo mpende sana mkeo kama unavyojipenda mwenyewe lakini jiamini mwenyewe wewe na Mungu wako.

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao.

(Visited 87 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175