Jinsi uchovu sugu unavyoleta upungufu wa nguvu za kiume

Published by Fadhili Paulo on

uchovu unaleta upungufu wa nguvu za kiume

Jinsi uchovu sugu unavyoleta upungufu wa nguvu za kiume

Uchovu unaotokana na kazi ni zaidi ya kuchoka kwa kawaida, na unazidi uchovu unaosababishwa na shughuli za kila siku.

Dalili za uchovu huo ni kuchoka kupita kiasi kwa muda mrefu na vilevile kuhisi umekata tamaa na kukosa nguvu.

Watu wanaokabiliana na uchovu huo hawafurahii kufanya kazi zao, yaani, wanakosa hamasa ya kufanya kazi na hivyo kuathiri ubora wa kazi.

Utafiti pia unaonyesha kwamba kuchoka kupita kiasi husababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.

Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Nguvu za kiume ni nguvu za mwili na siyo nguvu za uume.

Ni nini kinachosababisha uchovu mwingi?

Kwa kawaida kazi nyingi kupita kiasi ndicho chanzo kikuu.

Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, baadhi ya waajiri hutaka wafanyakazi wao wafanye kazi saa nyingi zaidi, na bila malipo ya kutosha.

Maendeleo ya teknolojia hufanya iwe vigumu kwa watu fulani kutenganisha shughuli za kikazi na maisha ya binafsi.

Kwa mfano mimi sehemu kubwa za kazi zangu huzifanya kwa kutumia WhatsApp na WhatsApp ipo kwenye simu, sasa kuna wakati najikuta naendelea kufanya kazi hata wakati wa mapumziko au hata baada ya muda wa kazi kuisha hivyo kuna siku najikuta nafanya kazi hata zaidi ya masaa 16 jambo ambalo ni hatari kwa afya yangu.

Nao wengine hupatwa na uchovu huo kwa sababu wanahofu kupoteza kazi zao, hawawezi kuzidhibiti, au wanahisi kwamba wanaonewa.

Vilevile kutojua majukumu yao kazini au migogoro kati yao na wafanyakazi wenzao huchangia kuchoka kupita kiasi.

Uchovu mwingi pia unaweza kusababishwa na mtu mwenyewe. Ili wafikie malengo yao na kupata pesa nyingi, baadhi ya watu hufanya kazi zaidi ya moja. Watu hao wana majukumu mengi na wanakabili hatari ya kuchoka kupita kiasi.

Ikiwa unakabili tatizo la kuchoka kupita kiasi kazini, unawezaje kushinda tatizo hilo?

Huenda ikaonekana vigumu kushinda tatizo hilo ikiwa kuna mambo yanayopita uwezo wako.

Mimi binafsi ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kukumbwa na mkasa huu wa kuwa na uchovu sugu.  Nilikuwa napenda sana kufanya kazi masaa mengi kwa kisingizio kile kile kwamba natafuta hela na maisha.

Kawaida ilikuwa naamka saa kumi au saa kumi na moja asubuhi mapema na ninaelekea ofisini ambako hakukuwa mbali na nyumbani na nilikuwa natembea tu kwa miguu. Na ningeweza kuwasha computer hiyo saa kumi na moja asubuhi na kuizima saa nne au tano usiku ndiyo narudi nyumbani nimechoka vibaya.

Anyway, ni kweli hela nilikuwa napata lakini hazikuweza kumaliza matatizo niliyokuwa nayo na zaidi nilipata tu matatizo mengine zaidi kwani sikuwa karibu sana na familia yangu na hata ndugu na marafiki.

Baadaye sana kwa neema tu ya Mungu nilifanikiwa kuachana na huo utumwa. Nimepunguza kazi na majukumu yangu zaidi ya nusu na ninajali muda wangu kuliko kitu kingine chochote.

Ninaridhika na chochote nipatacho mhimu niweze kula basi mengine ni majaliwa sina stress nayo kwani kuna siku moja yote nitayaacha hapa chini ya jua!

Hata wewe unaweza kupata suluhisho la tatizo lako kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 1. Chunguza ni jambo lipi unalipa kipaumbele sana

Ni nini muhimu zaidi kwako?

Watu wenye akili (smart people) wanasema kwamba uhusiano na familia zao na afya njema ndiyo mambo muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Hivyo, ukichoka kupita kiasi familia yako nayo itaathirika na afya yako itazorota.

Ukizingatia mambo muhimu, itakuwa rahisi kwako kufanya maamuzi magumu na kukataa majukumu fulani.

Kwa mfano, unaweza kugundua kwamba kazi yako inakusababishia uchovu unaopita kiasi.

Hata hivyo, huenda ukasema, ‘Siwezi kubadili kazi au kupunguza muda ninaofanya kazi; ninahitaji pesa!’ Ni kweli, kila mtu anahitaji pesa, lakini kazi yako inaathirije mambo unayothamini zaidi?

Uwe mwangalifu ili usitangulize mambo ambayo wengine wanaona kuwa siyo ya muhimu sana katika maisha.

Huenda mambo ambayo ni muhimu kwa mwajiri wako yakatofautiana na mambo yaliyo muhimu kwako.

Wengine wanaweza kutanguliza kazi kuliko mambo mengine maishani, lakini haimaanishi na wewe unapaswa kufanya hivyo.

2. Rahisisha maisha yako

Ili upunguze mkazo na upate muda wa kutimiza mambo unayothamini zaidi, huenda ukahitaji kufanya kazi kwa saa chache, kumwomba mwajiri wako akupunguzie majukumu, au ukahitaji kubadili kazi.

Vyovyote vile, inaelekea utahitaji kupunguza matumizi ya fedha na kubadili mtindo wako wa maisha.

Inawezekana kufanya marekebisho hayo, na huenda isiwe vigumu kama unavyowazia.

Katika nchi nyingi, wafanyabiashara wanashawishi watu wanunue bidhaa, na wengi wanafikiri kwamba furaha inatokana na kupata utajiri. Hata hivyo, si kweli.

Maisha rahisi yanaweza kukuletea uhuru mwingi na kufanya uridhike.

Ili ufanikiwe kufanya mabadiliko hayo, unahitaji kupunguza matumizi yako na kuweka akiba ya pesa.

Jitahidi kupunguza au kuepuka madeni.

Zungumza na familia yako kuhusu umuhimu wa mabadiliko hayo na uwaombe wakuunge mkono.

 3. Jifunze kusema HAPANA.

Ikiwa una kazi nyingi kupita kiasi au tatizo lenye kudumu kazini, zungumza na mwajiri wako.

Ikiwezekana, toa mapendekezo yanayofaa hali yako na pia mwajiri wako. Mhakikishie mwajiri wako kwamba unapenda kazi, na ufafanue yale ambayo uko tayari kufanya; lakini utaje waziwazi na kwa uthabiti mambo ambayo huwezi kufanya.

Uwe mwenye busara na uone mambo kihalisi.

Ikiwa unataka kufanya kazi kwa saa chache, huenda mwajiri wako akapunguza mshahara wako.

Fikiria pia uwezekano wa kufutwa kazi, na uwe tayari kukabiliana na hali hiyo.

Si lazima uache kazi ili utafute kazi nyingine, ni rahisi kupata kazi nyingine ukiwa bado kazini.

Hata kama mwajiri wako atakubali ufanye kazi kidogo ujue kwamba huenda baadaye akasisitiza ufanye kazi zaidi.

Ni nini kitakachokusaidia kudumisha msimamo wako? Jitahidi kudumisha makubaliano yenu ya awali. Kufanya hivyo kutakupa uhuru wa kumwomba mwajiri aendelee kufuata makubaliano hayo.

 4. Tenga muda wa kupumzika

Hata ukifaulu kupunguza kazi, huenda bado utapatwa na mkazo, utashughulika na watu wagumu, au hali zisizopendeza.

Uwe na muda wa kupumzika vya kutosha na uwe na burudani kwa kiasi.

Kumbuka kwamba si lazima utumie pesa nyingi ili ufurahie burudani pamoja na familia yako.

Mbali na kazi, uwe na mambo unayofurahia kufanya na pia uwe na marafiki, na uepuke kufikiria kazi tu kila wakati. Kwa nini? Kitabu Your Money or Your Life kinasema hivi: “Utu wako ni muhimu kuliko kazi unayofanya ili kupata pesa.”

Ikiwa unafikiri utambulisho wako au heshima yako inategemea kazi yako, huenda ukashindwa kuweka mpaka kati ya kazi na shughuli zako mwenyewe.

Je, unaweza kufanya mabadiliko ili ufanikiwe kukabiliana na kuchoka kupita kiasi?

Bila shaka, unaweza.

Tunza afya yako. Pumzika vya kutosha.

Hakuna faida kufanya kazi kupita kiasi na kupuuza mambo mengine yote kama afya yako, familia, na marafiki ili tu upate mafanikio.

Hela inaleta furaha ikiwa tu itakuongezea zaidi muda wa kupumzika na siyo kufanya kazi zaidi.

Kama una biashara au kazi yoyote inakuingizia hela lakini haikupi hata siku 20 kwa mwaka za kwenda kupumzika hata katika mbuga moja tu ya wanyama hapa Tanzania basi hiyo siyo kazi, ni utumwa.

Kama una hela tayari zifanye hela zako zifanye kazi badala yako. Sasa wewe una hela halafu unaweka bank badala ya kuzituma zifanye kazi wewe uwe mtu wa kukagua tu unafanya kinyume chake yaani unakuwa bize kutafuta hela mpaka unasahau afya yako na hata mkeo au marafiki zako.

Ulaya na Marekani kwa sasa utajiri siyo nyumba kubwa au gari kubwa, hapana. Kwa huko wenzetu kwa sasa utajiri ni uwezo wa wewe kuiacha kazi yako na kwenda sehemu fulani ukipumzika kwa muda fulani bila kufanya shughuli yoyote! huo ndiyo utajiri

Kumbuka vyote unavyohangaika navyo mpaka usiku wa manane ili upate hela zaidi au utajiri kuna siku tu utalazimika kuviacha na utapumzishwa kaburini.

If you can’t set time aside to rest, soon you will receive R.I.P from your friends. Kama huwezi kutenga muda pembeni wa kupumzika baada ya kazi, muda si mrefu utapata kauli ya upumzike kwa amani (R.I.P) kutoka kutoka kwa rafiki zako.

Kuna mtu unasoma ujumbe huu hapa na kwa mwezi kwenye biashara zako unao uwezo wa kuweka pembeni kama faida milioni 5 au hata zaidi lakini ulivyo upo bize huwezi hata kutumia weekend moja ukiogelea baharini na familia yako au marafiki zako. Kila siku wewe ni kazi kazi na wewe!

Ili uwe na nguvu za kiume kwanza unahitaji utulivu wa nafsi, usiwe na uchovu wowote, uwe na nguvu za mwili na akili na huwezi kupata hivi vyote kama wewe upo bize masaa 24

Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine

(Visited 549 times, 1 visits today)

2 Comments

Hilally Ayoub · 29/02/2020 at 11:47 pm

Good
Elimu nzuri doctor

    Fadhili Paulo · 03/03/2020 at 4:58 am

    Nafurahi kusikia hivyo Avat

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175