Jinsi ya kupunguza uzito huku unacheka

Published by Fadhili Paulo on

Last Updated on 22/05/2021 by Fadhili Paulo

Jinsi ya kupungua uzito huku unacheka

Ndiyo upungue uzito, unene kupita kiasi, kitambi na mafuta mwilini huku unatabasamu

Watu wengi wakitaka kupungua uzito wanawaza kuhusu mazoezi, kufunga kula, kuacha vyakula vyenye mafuta na kutumia dawa kila mara tena dawa chungu na zingine zinauzwa gharama sana

Hayo yote huhitaji ili kupungua uzito

Huhitaji huzuni au upoteze hela ili upungue uzito

Nitakueleza kwa lugha rahisi kabisa ya kiswahili inayoeleweka vizuri na kila mtu ni nini unatakiwa kufanya ili upungue uzito wako huku ukiwa na furaha tele usoni

Huku ukitabasamu na huku unacheka lakini wakati huo huo uzito wako unapungua

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa tiba asili na ni mtanzania

WhatsApp natumia namba +255714800175

Sasa namna yenyewe siyo jambo jipya sana au la kushangaza sana, hapana

Namna yenyewe ni kuwa bize kila siku kucheza muziki wa dansi dakika 40 mpaka 60 wakati wowote

Kama utafanya uchunguzi binafsi unaweza kubaini kuwa karibu watu wote ambao wapo kwenye fani hii ya kucheza muziki hasa muziki wa dansi ni watu wembamba

Kucheza tu muziki wa dansi kunaweza kukusaidia kupungua uzito wako bila kulazimika kufunga au kutumia dawa yenye gharama kubwa

Kama utamkuta mcheza muziki wa dansi ni mnene basi labda ni mmoja katika 100

Unapouchangamsha mwili wako wakati upo bize unacheza muziki basi siyo kwamba unajisikia kuwa na furaha tu (ambalo ni jambo la kawaida huwezi kucheza muziki kama huna furaha) bali pia mwili wako unakuwa unakata mafuta

Kwenye mwili wako Kuna homoni ya kuchoma mafuta inaitwa lipase, homoni hii haiamki kuchoma mafuta peke yake mpaka umeushughulisha mwili kwa mazoezi kama haya ya kucheza muziki

Inapoamshwa kuchoma mafuta baada ya wewe kuwa bize ukicheza muziki kwa dakika 40 au 60 mfululizo homoni hii huendelea kuchoma mafuta yenyewe pole pole kwa muda wa masaa 12 hata baada ya wewe kuacha kucheza

Sasa labda na wewe ni mwenzangu na mimi ambao hatuwezi kupata muda wa kwenda disko au kwenye kumbi za starehe au kwenye mabar huko kwenda kucheza muziki, je itakuwaje?

Usipate tabu juu ya kuwaza kwenda disko au bar ili uweze kucheza muziki

Hapo hapo nyumbani kwako Ukitumia redio yako au TV yako weka muziki wa dansi funga milango na madirisha cheza muziki mwenyewe mpaka uchoke

Na uendelee hivyo kila siku

Unaweza pia kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vinavyojihusisha na kudansi kama huna aibu au siyo mchungaji kama mimi na ukaendelea na kudansi huku unapungua uzito pole pole

Kudansi pia kunaondoa msongo wa mawazo na stress

Msongo wa mawazo unahusika pia kwenye moja ya vitu vinavyoongeza uzito na mwili kwa ujumla

Unaweza kuingia YouTube tafuta video na channel mbalimbali za muziki wa dansi, Tazama huku unacheza na matokeo yake ni wewe kupungua uzito bila gharama yoyote

Hiyo ni njia mojawapo ya kupungua uzito huku unacheka

Weka muziki kwenye redio au kwenye TV au ingia YouTube tafuta miziki ya dansi itazame au isikilize huku ukiwa bize unacheza dakika 40 mpaka 60 kila siku ndani ya wiki 2 mpaka mwezi mmoja uzito wako uliozidi utaondoka

Naam, njia ya pili ya kupungua uzito huku unacheka ni kushiriki tendo la ndoa

Ndiyo, tendo la ndoa tu linaweza kukusaidia kupungua uzito

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili.

Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Tendo la ndoa husaidia kupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)

Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini

Tendo la ndoa hupunguza mfadhaiko wa moyo

Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Usingizi mzuri na wa uhakika ni mhimu katika kudhibiti uzito wako wa mwili

Tendo la ndoa huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).

Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Tendo la ndoa pia husaidia mtu kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana

Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa. Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu.

Ahsanteni kwa muda wenu

Kama wewe ni mwanaume na unawahi sana kufika kileleni tuwasiliane WhatsApp 0714800175 ninayo pia dawa ya asili nzuri ya kuondoa kabisa Kitambi

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo
(Visited 118 times, 1 visits today)

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175 Nifuate kwenye > Twitter

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175