Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

Published by Fadhili Paulo on

Kitunguu swaumu

Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu.

Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili ni kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum.

Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita.

Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, virusi, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi.

Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.

Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi!

Hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na uniletee mrejesho

Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia.

Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).

Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya.

Hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.

Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake.

Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.

Unaweza kutumia kitunguu swaumu kwenye chakula chako kila siku, kuna kitunguu swaumu pia katika unga pia katika mfumo wa vidonge

Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu

Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja,
2. Kigawanyishe katika punje punje,
3. Chukua punje 6 menya punje moja baada ya nyingine.
4. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu,
5. Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au kila baada ya siku 1.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe.

Na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Unaweza kutumia mtindi uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani. Binafsi mara nyingi natumia mtindi wa Tanga freshi.

Dozi ni siku ngapi? Unaweza kutumia mpaka utakapochoka mwenyewe. Ni chakula tu kama vilivyo viazi. Unaweza kutumia hata kama huumwi chochote.

Watoto wadogo miaka miwili kwenda juu mpaka miaka 10 unaweza kuwapa punje 2 kwa siku.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo wa kuimarisha na kuongeza kinga ya mwili ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti.

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

1. Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

2. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

3. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, fangasi na virusi.

4. Huondoa sumu mwilini jambo ambalo ni mhimu sana ili uwe na kinga nzuri ya mwili

5. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi. Huwezi kuwa na kinga nzuri ya mwili kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

6. Kinaondoa msongo wa mawazo (stress) na kukufanya uishi miaka mingi. Ni vigumu au ni sawa na haiwezekani uwe na msongo wa mawazo (stress) halafu uwe na kinga nzuri ya mwili.

7. Hutibu kifua kikuu (TB). Ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu.

8. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine

9. Huzuia kuhara damu (Dysentery)

10. Huondoa Gesi tumboni

11. Hutibu msokoto wa tumbo

12. Hutibu Typhoid

13. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi

14. Hutibu mafua na malaria

15. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I

16. Hutibu kipindupindu

17. Hutibu upele

Kwa kutumia kitunguu swaumu tu unaweza kujitibu tatizo la ukurutu na hata upele.

Kitunguu swaumu kina nguvu dhdi ya bakteria na wadudu wengine wanaosababisha maambukizi kwenye ngozi.

Kitunguu swaumu kinaweza kufanya kazi hii kwa namna mbili. Kama utakunywa kitunguu swaumu kinaweza kusaidia kupunguza ukali wa maambukizi na hata kuyazuia kutojirudia. Njia ya pili kitunguu swaumu kinaweza kutengenezwa mafuta na kupakwa juu ya ngozi moja kwa moja.

Kitunguu swaumu kinadhibiti virusi, fangasi, bakteria na vijidudu vingine nyemelezi. Kazi hizi zote zinawezeshwa na kitu mhimu kilichopo kwenye kitunguu swaumu kijulikanacho kama ‘Alicin’.

Ukurutu, chunusi, miwasho, mba, upele na matatizo mengi ya ngozi yanaweza kutibiwa kwa kutunguu swaumu tu

18. Huvunjavunja mawe katika figo

19. Hutibu mba kichwani

20. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.

21. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu ya jino

22. Hutibu maumivu ya kichwa

23. Hutibu kizunguzungu

24. Hutibu shinikizo la juu la damu

25. Huzuia saratani mbalimbali

26. Hutibu maumivu ya jongo (gout)

27. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

28. Huongeza hamu ya kula

29. Huzuia damu kuganda

30. Husaidia kutibu kisukari

31. Husafisha tumbo

32. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)

Tafiti kadhaa zimeonyesha kitunguu swaumu kuwa na ufanisi mkubwa sana katika kutibu magonjwa kama shinikizo la juu la damu, kolesteroli na magonjwa ya mishipa ya moyo.

Kitunguu swaumu huzuia kujikaza au kuzibika kwa mishipa ya damu.

Kitunguu swaumu pia huongeza msukumo wa damu.

Kama umeambiwa moyo wako umekuwa mkubwa sana au una tatizo lolote kwenye moyo kitunguu swaumu kinaweza kuwa msaada mkubwa kwako

Mhimu : Kitunguu swaumu kinaweza kisipatane na aina nyingi ya dawa za hospitalini sababu ya baadhi ya dawa hizo hukaza mishipa ya damu. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza kutumia hii dawa

33. Kitunguu swaumu hutibu majipu

Unaweza kutumia kitunguu swaumu pekee au ukikichanganya na kitunguu maji ili kutibu majipu.

Wakati unataka kutibu jipu sehemu yoyote katika mwili wako unaweza kunywa kitunguu swaumu au hata kupakaa mafuta yake juu ya ngozi yenye jipu moja kwa moja.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kitunguu swaumu kina uwezo wa kudhibiti bakteria, uvimbe, na vijidudu mbalimbali nyemelezi katika mwili.

Ule uwezo wake wa kudhibiti uvimbe (anti-inflammatory properties) unakifanya kitunguu swaumu kuwa dawa bora mbadala ya kutibu jipu.

34. Kitunguu swaumu kinatibu korodani zinazovimba

Kuna wanaume wanapatwa na korodani zao kuongezeka ukubwa au zinavimba.

Inaweza kutokea korodani zote 2 zikavimba au korodani moja kati ya mbili ikaongezeka ukubwa na nyingine ikabaki ndogo vile vile.

Tatizo hili (enlarged prostate) linaweza kutibika kwa kutumia kitunguu swaumu tu.

35. Kitunguu swaumu kinatibu Pumu

Kitunguu swaumu kikichanganywa na maji ya moto au maziwa ya moto ni dawa nzuri sana ya kutibu pumu.

Kitunguu swaumu kinao uwezo wa kuondoa msongamano kwenye mapafu na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa mtu mwenye pumu.

Kitunguu swaumu kinatibu pumu na kuziondoa kabisa dalili zake haraka.

Angalizo kuhusu kitunguu swaumu:

1. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema usitumie kitunguu swaumu kwa namna hii mpaka umeongea na kukubaliana na daktari wako wa karibu. Pia watoto chini ya miaka miwili wasitumie kitunguu swaumu kwa namna hii.

2. Vile vile kama una presha ya kushuka usitumie kitunguu swaumu kwa namna hii.

3. Harufu mbaya mdomoni baada ya kutumia kitunguu swaumu hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide).

Harufu hii mbaya hata hivyo yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu.

Na nimeshuhudia nikinywa kitunguu swaumu kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji

4. Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)

5. Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha

6. Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.

7. Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.

8. Aidha vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa

9. Ukiona kichwa kinauma sana siku 3 au 5 baada ya kuanza kutumia kitunguu swaumu utatakiwa kuacha kukitumia kwa siku 2 au 3 mpaka kichwa kiache kukuuma ndipo uendelee tena na dozi. Na ndiyo sababu napenda utumie kila baada ya siku 1 na siyo kila siku ili kuepuka hili la kuumwa kichwa

Mhimu : Ukiwa na swali lolote kuhusu kitunguu swaumu naomba uulize hapa chini kwenye comment nitakujibu hapa hapa tena.

Soma hii pia 👇

Njia zingine mpya 8 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30 Click To Tweet

Share na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 818

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *