Mabadiliko matano yanayotokea kwenye uume wako kadri unavyozidi kuwa mzee

Published by Fadhili Paulo on

Mabadiliko matano yanayotokea kwenye uume wako kadri unavyozidi kuwa mzee

Kama vile ngozi yako inavyobadilika kadri unavyozidi kuwa mzee kadharika kuna mabadiliko pia yatatokea hata kwa upande wa mheshimiwa.

Najua ungependa mheshimiwa aendelee kubaki kama ulivyokuwa na miaka 25 lakini kwa bahati mbaya hilo haliwezekani.

Kwa hiyo, unavyoelekea kuwa mzee na ukishakuwa mzee basi hata uume wako lazima uzeeke pia.

Ni mabadiliko yanayotokea kidogo kidogo sana na pengine unaweza usiyahisi kabisa na unaweza ukashindwa kuona kama kuna badiliko linaendelea.

Kwenye makala hii ninaangazia juu ya mabadiliko matano yanayotokea kwenye uume wako kadri unavyozidi kuwa mzee.

1. Rangi

Hili ni tatizo la kawaida kwa wanaume wanaokaribia kuwa wazee.

Rangi hasa rangi ya kichwa chote cha uume hubadilika.

Kawaida rangi ya kichwa cha uume huanza kufifia na kuwa tofauti na ulivyokuwa mwanzo.

Hili mara nyingi ni matokeo ya msukumo wa damu kupungua kwenye ubongo, moyo na kwenye uume kama matokeo ya kuelekea kuzeeka.

Hili siyo jambo la kuwa na wasiwasi nalo hasa kama vipimo vya afya yako kwa ujumla vinasema upo salama.

Hata ukijichunguza tu ngozi yako ya mwili kwa ujumla baada ya miaka 50 utaona kuna mabadiliko fulani ya muonekano wake, kwahiyo siyo ajabu ukiona hata rangi ya uume hasa sehemu ya kichwa nayo imebadilika.

2. Kusinyaa na kupungua ukubwa

Hili ndilo jambo wanaume wengi hawapendi liwatokee!

Hata hivyo ukweli ni kuwa ukubwa wa uume wako utapungua kidogo kidogo kadri unavyozidi kuwa mtu mzima.

Kwa kawaida kuanzia miaka 45 kwenda juu uume wako utaanza kusinyaa kidogo kidogo kila mwaka na mpaka unafikisha miaka 60 uume wako unaweza kuwa umepungua mpaka nusu ya ukubwa wake wa asili.

Na kama mwanaume una kitambi basi unaweza kuanza kuona kupungua huku kwa uume wako mapema zaidi hata kabla ya miaka 50.

Kama utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kuondoa kitambi niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

3. Kupungua kwa uwezo wa hisia

Kadri unavyoelekea kuwa mzee ndivyo na uwezo wa kuhisi wa uume wako unavyopungua pia.

Kwenye uume kuna miishio mingi ya neva za fahamu na kwa kawaida uume unapoingia ukeni huwa unakuwa na hisia zake.

Sasa uwezo huu wa kuhisi labda kama ukeni kuna joto, kuna ubaridi, uke ni mtamu au siyo mtamu hupungua kadri mwanaume unavyozidi kuwa mzee.

Hisia kwenye uume kwa kiingereza ‘Sensitivity’ inapungua kama matokeo pia ya kupungua au kushuka kwa kiwango cha homoni ya ‘Testosterone’.

Kadri unavyoelekea kuwa mzee ndivyo na usawa wa testosterone unavyopungua na ndivyo itakavyokuwa inakuwia vigumu kufika kileleni na kusikia raha yake.

Vile vile kusimama kwa uume kutakuwa ni kwa ulegelege na uchovu.

Na kama hushiriki tendo la ndoa walau mara 1 kwa wiki baada ya miaka 50 hali hizi zinaweza kukutokea mapema zaidi.

Kadri unavyokuwa mtu wa kushiriki tendo la ndoa hapa na pale ndivyo unavyoweza kupunguza madhara haya hapo uzeeni tofauti na yule ambaye hashiriki kabisa au anashiriki mara chache sana kwa mwaka.

Uuume ni msuli kama ilivyo misuli mingine mwilini, hivyo kadri unavyofanyishwa mazoezi (unaposhiriki tendo la ndoa mara kwa mara) ndivyo na wenyewe unavyozidi kuwa na afya nzuri hata uzeeni.

4. Kushuka kwa ufanisi wa mfumo wa mkojo

Matatizo mbalimbali kwenye mfumo wa mkojo ni ya kawaida kwa wanaume watu wazima wanaoelekea kuwa wazee na wale ambao tayari ni wazee.

Hili kwa kawaida huanzia kwenye tezi dume.

Hapa utaona uwezo wako wa kushikilia mkojo usitoke au kuuamuru utoke unapungua.

Unaweza kujikuta tu tayari umeshajikojolea pasipo kujua wala kuhisi hitaji la kutaka kukojoa kabla.

Hili huathiri karibu asilimia 20 ya wanaume wote kuanzia miaka 60 na kuendelea.

Unachoweza kufanya ili kuzuia madhara haya ya namba 4 ni pamoja na;

*Kuwa na uzito sahihi
*Kupenda kuwa mtu wa kutembea tembea na siyo kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi
*Tumia kwa wingi vyakula vyenye madini ya zinki na seleniamu
*Punguza kunywa pombe au acha kabisa

Soma pia hii > Siri 5 za watu wanaofanikiwa kuishi miaka mingi

Sababu za uume kusinyaa

5. Kushuka kwa nguvu za kiume

Kushuka kwa nguvu za kiume na ufanisi wa uume kwa ujumla ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi kuanzia miaka 45 na kuendelea.

Hili haliepukiki na halina mbinu zozote za kulizuia.

Baada ya miaka 55 ni kawaida kabisa kwa mwanaume kuwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tena tendo la ndoa.

Baada ya miaka 55 mwanaume unaomba tu uume uwe na uwezo wa kusimama ili uweze kuingia lakini huna mawazo yoyote ya kukesha hapo au kumfikisha mtu kileleni.

Ni jambo la kawaida na unatakiwa ulipokee kama lilivyo kwani ukitaka kupambana nalo sana unaweza kufa kabla miaka yako ya kufa haijafika.

Kama uume hausimami kabisa au unasimama kwa ulege lege sana unaweza kutafuta suluhisho kwa kutumia dawa za asili zisizo na madhara mabaya.

Na ni mhimu kutibu magonjwa yanayoweza kuwa ndiyo chanzo cha tatizo kama vile presha, kisukari, saratani ya tezidume nk kuliko kwenda kutibu nguvu za kiume moja kwa moja.

Lakini usijitese wala kutaka uonekane wewe ni rijali. Afya yako na uzima wako ni mhimu zaidi kuliko kumfikisha mtu kileleni.

Mabadiliko matano yanayotokea kwenye uume wako kadri unavyozidi kuwa mzee Click To Tweet

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175