Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili

Published by Fadhili Paulo on

Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili

Kupenda vitu vitamu hususani jamii ya sukari huwa ni tamu sana kwenye ulimi lakini changamoto inakuja kule inakoelekea kwa ajili ya kutunzwa na kutumika, hapo ndo husababisha changamoto mbalimbali mwilini hasa kwenye baadhi ya viungo vya mwili.

Madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari huanza taratibu, kadiri unavyo kuwa na sukari na unavyo shindwa kuchukua hatua juu ya sukari hiyo ndivyo hatari ya kupata madhara makubwa huongezeka.

Pia ikumbukwe madhara yatoka nayo na kisukari huweza kuhatarisha maisha ya mtu.

Yafuatayo ni madhara ya sukari inapozidi mwili na kiwango sahihi cha sukari inayotakiwa mwili pale unapokuwa umekula chakula:

Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili

1. Vidonda vya miguuni

Ugonjwa wa kisukari huathiri miguuni hasa pale unapopata ganzi inapelekea kushindwa kuhisi maumivu hivyo hata ukipata jeraha au mchubuko unakuwa huhisi maumivu ya aina yoyote.

Unakuwa hauna tofauti na aliechomwa sindano ya ganzi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Vidonda vya mtu mwenye kisukari ni vigumu sana kupona kwa sababu damu inakuwa haifiki ya kutosha kwenye kidonda na asilimia kubwa bakteria wabaya huanza kukishambulia kwa kasi kwa sababu kinakuwa ni kitamu 

Kwa kuwa kidonda kina bakteria na kinaonekana kuwa na malengelenge ya mafuta na hao bakteria hushambulia kwa kasi hivyo kusababisha kuongezeka kwa kidonda na mwishowe kukatwa endapo hutawahi huduma mapema ya kujikinga. ·        

2. Kutokuona vizuri au mtoto wa jicho

Mishipa ya kwenye macho huwa ni midogo midogo sana na iko laini sana ukiliganisha na mishipa ya sehemu zingine za mwili hivyo inapoingiliwa na sukari damu hushidwa kupita ya kutosha sehemu za macho na kumfanya mtu awe anaona ukungu ukungu au kutokuona kabisa. ·        

3. Madhara ya figo

Figo inapokuwa imezidiwa na kiwago kingi cha sukari hulazimika kupunguza maji ya ziada na utengenezaji wa calcium kwa ajili ya kulinda mifupa hivyo sukari nyingi kukimbilia kwenye damu na baadaye huwa sumu mwilini. ·        

4. Kiharusi (stroke)

Kwa kuwa madhara ya sukari mojawapo ni kudhoofisha mishipa kwenye mwili hivyo mtu wa kisukari ana hatari kubwa ya kupata stroke kwa sababu baadhi ya mishipa kwenye ubongo huathiriwa na kukosa uwezo wa kupitisha damu ya kutosha na mwishoe kupasuka na kusababisha kiharusi. ·        

5. Maradhi ya moyo

Vyanzo vya mishipa huanzia kwenye moyo na kusambaa pande zingine za mwili, moyo huathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa sababu sukari hudhoofisha mishipa na kumfanya mtu kuwa dhaifu hivyo kama damu haipiti ya kutosha kwenye mishipa inakuwa ni kirahisi kupata magonjwa ya moyo kama vile moyo kupanuka, moyo kuwa na tundo pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. ·        

6. Kwa wanaume kuishiwa nguvu za kiume

Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume kwa sababu mfumo wa uzazi wa mwanaume umeundwa kwa mishipa na misuli, kama patakuwa hakupati ujazo mzuri wa damu inakuwa ni rahisi sana kushidwa kushiriki tendo ndoa na wengi wao wanapopatwa na hali kama hii huigiwa na presha au msongo wa mawazo na kuibua matatizo mengine tena.  

Hayo ni baadhi ya madhara anayopatwa mtu mwenye kisukari japo anaweza kupatwa na changamoto zingine nyingi kwenye mwili wake na kumpelekea kupata shida awe mtoto au mtu mzima, lakini kwa kukosa uelewa na umakini zaidi kundi la watu wengi huishia kukatwa baadhi ya viungo na mwishowe kifo.

7. Kuvurugika kwa vichocheo vya mwili

8. Hatari ya kupata maambukizi kutokana na kushindwa kufanya kazi vizuri kwa seli nyeupe za damu

9. Kwa wamama wenye kisukari kinacho tokana na ujauzito kupata  aina ya pili ya kisukari

10. Kifafa Cha mimba

11. Matatizo ya ganzi na kupooza endapo kisukari kitaathiri mishipa ya fahamu

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Makala hii inaendelea kuboreshwa kwa kuongeza picha na maelezo zaidi, endelea kuja …

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao.

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175