Magonjwa 10 yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

Published by Fadhili Paulo on

Magonjwa 10 yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

Kushuka kwa nguvu za kiume hakutokani tu na punyeto au vilevi au kutokushiriki mazoezi ya viungo kila mara

Pia siyo jambo la kushindwa kufahamu ule nini au usile nini

Wakati mwingine nguvu za kiume hushuka kama matokeo ya magonjwa mbalimbali yanayomkabili mwanaume

Kwenye makala hii nitajadili kueleza kwa kirefu juu ya magonjwa yanayoweza kuleta kushuka au kupungua kwa nguvu za kiume

Magonjwa 10 yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

1. Shambulio la moyo (heart attack)

Upungufu wa nguvu za kiume ni moja ya dalili za mwanzo za mishipa ya ateri kuziba.

Ateri zinapoziba au kubana zinatengeneza njia ya kutokea kwa ugonjwa wa shambulio la moyo

Ukweli ni kuwa mpaka asilimia 15 ya wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wanaweza kupata ugonjwa wa shambulio la moyo au matatizo yoyote kwenye moyo ndani ya miaka 7 tangu kushuka kusikotibika kwa nguvu zao za kiume

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tafiti mbalimbali zinazoonyesha uhusiano uliopo kati ya upungufu wa nguvu za kiume na ugonjwa wa moyo

Ateri (mishipa ya damu) inapoziba unaanza kupata madhara kwenye ogani zinazohitaji kupelekewa maji, oksijeni na viinilishe vingine mhimu.

Kwa kawaida ateri za kwenye uume ndizo zinazoanza kuziba sababu ni nyembamba kuliko za sehemu nyingine ya mwili

Asilimia 20 mpaka 30 ya wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wana aina fulani ya tatizo lililojificha linalohusiana na afya ya moyo

Kwa hiyo kama wewe ni mvuta sigara au bangi na kwa kipindi kirefu umekuwa na upungufu wa nguvu za kiume usioisha ni vizuri uwahi hospitali uonane na daktari kwa uchunguzi zaidi juu ya afya ya moyo wako

2. Saratani ya tezi dume

Saratani ya tezi dume yenyewe haileti upungufu wa nguvu za kiume moja kwa moja bali dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu ndizo zinazosemwa kuleta upungufu wa nguvu za kiume

Mionzi na upasuaji kwa mgonjwa wa saratani ya tezi dume ndivyo vitu vinavyoweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume

Upasuaji unaofanyika katika harakati za kumtibu mgonjwa wa saratani ya tezi dume ndiyo unaohusika sana na kushuka kwa nguvu za kiume

Wakati tezi dume inaondolewa (upasuaji) neva zinaweza kudhurika na kuleta upungufu wa nguvu za kiume

Neva zilizodhurika wakati wa upasuaji na mishipa damu iliyodhurika kama matokeo ya mionzi ndivyo vinavyohusiana na kushuka kwa nguvu za kiume

3. Shinikizo la juu la damu

Unaweza ukawa na shinikizo la juu la damu na bado ukaendelea kufurahia tendo la ndoa hasa kama utakuwa karibu na daktari wako na kumueleza ukweli bila kificho hali yako ilivyo

Wakati huo huo tendo la ndoa linaweza kukusaidia kupunguza kiwango cha shinikizo la juu la damu ulilonalo tayari

Wakati mwingine unaweza kuwa au unaweza kuishi na shinikizo la juu la damu na usijitambue au usionyeshe dalili zozote

Hata hivyo bado kuna uhusiano wa karibu kati ya shinikizo la juu la damu na upungufu wa nguvu za kiume

Hakuna tatizo la moja kwa moja la kufahamika kati ya shinikizo la juu la damu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa upande wa wanawake

Baada ya muda mrefu wa kuishi na shinikizo la juu la damu matokeo yake hujionyesha wazi kwa kushuka kwa uwezo wa mwanaume kuhimili tendo la ndoa

Kama ilivyo kwa kisukari au kwa shambulio la moyo (ambalo nalo ni matokeo ya mwisho mwisho ya shinikizo la juu la damu), shinikizo la juu la damu nalo ni matokeo ya kujibana na kupungua kwa vipenyo vya mishipa inayosafirisha damu kuanzia kwenye moyo mpaka sehemu mbalimbali za mwili

Kujibana, kuzibika au kupungua kwa vipenyo vya mishipa ya damu kama matokeo ya shinikizo la juu la damu ndiko kunakoleta upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya shinikizo la juu la damu

Shinikizo la juu la damu pia linaweza kuleta matatizo kwenye kufika mshindo na kushusha hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa

Wasiliana na daktari wako wa karibu kuhusiana na shinikizo lako la damu na afya yako ya kitandani

4. Kisukari

Inakadiriwa kuwa asilimia 35 mpaka 75 ya wanaume wenye kisukari watasumbuliwa na aina fulani ya usumbufu kuhusiana na tendo la ndoa katika maisha yao

Wanaume wenye kisukari wana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume mapema zaidi miaka 10 mpaka 15 kabla ya wanaume wengine wasio na kisukari

Kadri mwanaume mwenye kisukari anavyozidi kuwa mtu mzima au mzee ndivyo na uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa unavyozidi kushuka

Mwanaume mwenye kisukari mwenye miaka 50 kwenda juu ana uwezekano wa kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume mpaka asilimia 60 zaidi tofauti na asiye na kisukari

Sababu za kupungua kwa nguvu za kiume kwa wanaume wenye kisukari ni nyingi zikihusisha mabadiliko kwenye neva, mishipa ya damu na mabadiliko ya utendaji kazi wa misuli

Ili kupata msisimko na uume usimame kwa ufasaha mwanaume anahitaji afya nzuri ya mishipa ya damu, misuli imara na neva ili kudhibiti usimamaji imara na wa kudumu wa uume.

Kwa bahati mbaya kisukari kinasababisha madhara kwenye mishipa ya damu na neva zinazohusika na usimamaji wa uume.

Hivyo hata kama homoni zako zipo sawa na unapata hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa bado hutaweza kuwa na uume imara na unaoweza kusimama dakika nyingi.

Kisukari pia kina uhusiano wa karibu na ugonjwa wa moyo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Kisukari maana yake mfumo wako wa kutengeneza nguvu mwilini haupo sawa kwakuwa sukari ni moja ya chanzo kikuu cha nguvu za mwili

Mwili una vyanzo vikuu vitatu vya nguvu ambavyo ni sukari (vyakula tunavyokula hubadilishwa kuwa glukozi au damu sukari) ili kutengeneza nguvu ya mwili, chanzo cha pili ni maji na chumvi na chanzo cha tatu ni mafuta (kama utakuwa ni mtu wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara).

Kisukari maana yake mwili hauna uwezo wa kuunda na kuitumia ipasavyo sukari inayotengenezwa na mwili kupitia vyakula unavyokula na mwisho wake ni mwanaume kukosa au kuishiwa kabisa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa

5. Vidonda vya tumbo

Wanaume wengi wanaougua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu hutokewa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwahiyo ikiwa mwanaume una tatizo la kushindwa kuhimili tendo la ndoa na unaumwa vidonda vya tumbo basi cha kwanza utatakiwa ujitibu kwanza vidonda vya tumbo.

Hili linakuwa kweli hasa tukiziangalia baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo kama zifuatazo;

Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo zinazopelekea pia upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na zifuatazo:

1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
2. Kuumwa mgongo au kiuno
3. Kizunguzungu
4. Kukosa usingizi
5. Kiungulia
6. Tumbo kujaa gesi
7. Tumbo kuwaka moto
8. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
9. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
10. Kusahahu sahau na
11. Hasira bila sababu.

Dalili au matatizo yote hayo hapo juu yanayompata mgonjwa wa vidonda vya tumbo ndizo ambazo kwa namna nyingine kama matokeo yake zinapelekea tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi.

Mwanaume anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo pia anaweza kupatwa na kupungukiwa nguvu za kiume kama matokeo hasi ya baadhi ya dawa za kemikali zinazotumika kutibu vidonda vya tumbo.

Ingawa madaktari huangalia zaidi matokeo chanya ya dawa kuliko matokeo hasi hasa inapobidi upone ugonjwa mwingine hatari zaidi hata kama moja ya matokeo yake hasi yaweza kuwa ni kupatwa na ugonjwa mwingine.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya vidonda vya tumbo na msongo wa mawazo au huzuni. Na msongo wa mawazo au stress moja kwa moja husababisha kushuka kwa nguvu za kiume!

Kwa kifupi Mwanaume fanya kila uwezalo usiuguwe vidonda vya tumbo au fanya kila njia kuhakikisha unajitibia vidonda vya tumbo hadi unapona ikiwa unataka kuendelea kulinda heshima yako nyumbani.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Magonjwa mengine yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na;

6. Msongo wa mawazo

7. Bawasiri

8. Magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji

9. Uchovu sugu

10. Uzito kupita kiasi

Kama wewe ni mwanaume na unahitaji dawa ya asili ya uhakika na isiyo na madhara mabaya kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kumbuka nimeandika nitafute WhatsApp

Share makala hii na wengine uwapendao kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii

Magonjwa 10 yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume Click To Tweet
(Visited 370 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175