Makala

Nimepata mtoto wa kiume jana

Nimepata mtoto wa kiume jana

Jana saa tatu usiku Mungu amenipa mtoto mwingine tena wa kiume.

MGENI mpya hapa nyumbani!

Ni miujiza mitupu

Nina furaha hapa ambayo haielezeki

Furaha niliyonayo leo siwezi kuieleza mtu akanielewa

Nabubujikwa tu na machozi ya furaha na siamini kile kinaendelea

Amezaliwa jana tarehe 23 mwezi wa nne

Cha kushangaza hapa hata mwanangu mwingine kabla ya huyu (ni wa kiume pia) naye alizaliwa tarehe 23 mwezi wa 7

Kama kawaida wakati wote wa ujauzito sikutaka kufahamu jinsia ya mtoto, nilimwambia mke wangu hakuna kufanya kipimo kufahamu jinsia ya mtoto ili ije iwe kama surprise na ndicho kilichotokea na watoto wangu wote ni hivi hivi huwa sipendi kufuatilia jinsia kabla ya kuzaliwa na huwa nipo tayari kwa mtoto wa jinsia yoyote!

Tofauti na safari zingine, safari hii roho mtakatifu kwa ishara kadhaa alikuwa akiniambia nitapata wa kiume tena na ndicho kilichotokea, kama wiki 1 kabla nilikuwa kariakoo nikanunua viatu vimeandikwa HB nikajua tu hapa handsome boy yupo njiani anakuja na kweli imekuwa hivyo!!!

Mungu ni mwema sana nashindwa hata niseme nini

Lakini cha ajabu zaidi ni kuwa hata mimi baba yao pia nilizaliwa tarehe 23 ila mwezi na mwaka nimesahau kidogo!

Ahsante sana Mungu

Ngoja nikanunue kuku mkubwa wa kienyeji nichinje nile leo.

Sasa nina jumla ya watoto watano, wa kiume watatu na wa kike wawili na nafikiri wanatosha sasa kwa sasa!

Ahsante sana Mungu

Fadhili Paulo

WhatsApp +255714800175

(more…)