Makosa wafanyayo wanaume wengi wakiwa kitandani

1.Kosa la kwanza : KUWA MBALI NA MWILI WA MWANAMKE

Wakati unashiriki tendo la ndoa mwanamke anapata Raha zaidi Ikiwa mwanaume utamlalia mwili wako wote juu yake

Wanaume wengi hawajuwi hili. Usiweke mikono yako Kama stendi na kubaki juu juu tu huku uko bize na shughuli yako. Mlalie kabisa mwili wako wote ausikie na utaona mwenyewe atakavyokuzungushia kinu huko chini kwa raha zote

Hii ndiyo sababu mwanaume makini hutakiwi kuwa na kitambi. Kitambi ni ugonjwa na unatakiwa ukikatae kwa gharama yoyote

Wakati huo huo hii haitafaa kwa mwanamke mwenye ujauzito kuanzia miezi minne hivi hivyo uwe makini

Wakati huo huo pamoja na mambo ya digitali kuenea na watu kupenda usasa bado tafiti kote duniani zinaonyesha wanawake wengi bado wanafurahia zaidi staili ya Kifo cha mende yaani Ile iliyozoeleka zaidi ya mwanaume kuwa juu mwanamke chini

Wakati huo huo tumia wakati fulani kumtazama mkeo machoni na yeye akuangalie wakati mnaendelea na mechi yenu

Kama ulikuwa hujuwi mimi leo nimekujuza bure

2.Kosa la pili : KUTAKA KUFANYA KILA WALIONALO KWENYE PICHA ZA X

Wanaume wengi hawafahamu kama movie zile za kikubwa ni mpango maalumu wa shetani kuharibu hiki kizazi cha sasa.

Watu hudhani kuna elimu fulani wanaweza kuipata kuhusu tendo la ndoa kwa kutazama hizo picha au video chafu. Hakuna elimu yoyote ya maana unaweza kupata kupitia hizo video zaidi ya ushetani.

Ikumbukwe hizo picha nyingi kati ya hizo zaidi ya asilimia 98 hazina ukweli wala uhalisia wa mambo. Wale ni waigizaji, ni watu walijuwa wanaenda kurekodiwa na watatazamwa na watu wengine wengi.

Hivyo hatuwezi kujua Yule mwanaume kwenye hiyo video alifanya nini nusu saa au lisaa limoja kabla ya kuanza mchezo huo. Kama alikunywa viagra kabla je wewe unajua? Kama alitumia midawa ya kuongeza nguvu je unajuwa? Kama alikunywa mizinga kadhaa ya konyagi unajuwa?

Huwezi kutatzama hizo picha halafu ukataka yale uyaonayo humo ndiyo na mkeo akufanyie huo utakuwa ni utahira.

Moja ya madhara makubwa kwa mwanaume kutazama picha hizo kwanza inamuondolea hisia au hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Mwanzoni unapoanza kuzitazama utaona kama hamu yako kwa tendo inaongezeka au unasisimka zaidi lakini kadri unavyokuwa bingwa wa kutazama ujinga huo ndivyo na hamu yako na uwezo wa kuhimili tendo la ndoa unavyopungua. Hili watu wengi hawajuwi

Miaka ya karibuni baada ya kuenea kwa digitali kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kuishiwa au kupungukiwa sana hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wengi wanajiuliza chanzo ni nini na hawapati majibu lakini jichunguze binafsi kama umekuwa na ujinga huu wa kuangalia hizi picha basi hiyo ndiyo sababu kuu ya tatizo lako

Shida ya pili ya kutazama picha hizo ni kuwa mwanaume unaanza kujiona hufai, unajiona hutoshi, unajiona kama siyo vile ni mwanaume wa kweli jambo ambalo halina ukweli wowote ni matokeo ya kutazama ujinga huo.

Shida ya tatu ya kutazama mipicha hiyo ni kuwa inaweza kukuhamasisha kwenda kupiga punyeto jambo ambalo ni hatari kwa afya yako kuliko hata sigara!

Madhara ya punyeto nikianza kueleza hapa nahitaji post nyingine mpya inayojitegemea maana ni mengi ikiwemo kuishiwa nguvu za kiume, kuwa na uume mlegevu, kupoteza kumbukumbu kirahisi, uchovu mwingi, kukosa umakini, kuishiwa kujiamini na kuwa muoga kwa vitu hata vya kitoto na unaweza ukaishiwa kabisa uwezo wa kujiamini kumtongoza mwanamke.

Kosa moja kubwa sana wanalofanya wanaume wengi bila wao kujua ni kutazama video hizi chafu wakiwa na wake zao! Yaani kama kuna kitu kitaharibu mahusiano yako haraka bila wewe kujua sababu ni kutazama picha hizi na mkeo. Hata kama itakutokea kwa bahati mbaya kamwe usije hata siku moja kuangalia ujinga mkiwa wawili na mkeo. Kwa sasa unaweza usinielewe ila kadri siku zinavyoenda utakuja kunikubali.

Kwahiyo usije hata siku moja kutaka kutekeleza kila unaloliona kwenye picha hizo kwa mkeo au kwenye ndoa yako. Asilimia 90 ya unayoyaona kwenye hizo picha mkeo hatakuwa tayari kuyatekeleza wakati ukishiriki naye tendo la ndoa na ujifunze kuyakubali yale ambayo mkeo au mchumba wako anayosema hayawezi au ni kinyume na mila na desturi yake!

Kama una picha au video hizi kwenye simu au computer yako zifute sasa dakika hii hii umalizapo kusoma ujumbe huu, kama kuna magroup upo huko WhatsApp au hata hapa facebook kuna watu wanapost mipicha hiyo ya kijinga jitowe (left) sasa hivi na usigeuke nyuma na ikitokea yoyote amekuweka tena jitowe haraka na umwambie asirudie ujinga huo utamchukulia hatua za kisheria haraka bila yeye kujua. Kama kuna blogs au tovuti huwa unatembelea futa anuani zake na historia zake na jitahidi uzisahau huku ukimuomba Mungu akusamehe na kukubadilisha.

Nini cha kufanya; kwanza acha hiyo tabia chafu ya kuangalia hiyo mipicha isiyompendeza hata Mungu. Unaharibu afya yako ya mwili na akili bila kujua. Pili pamoja na kupotoka huko kwako kwa kutazama mipicha hiyo tambua kuanzia leo kuwa kutaka kuyafanya yote uyaonayo kwenye hizo picha kitandani kwako ni kosa kubwa linaloweza kugharimu mahusiano yako kama hutakuwa mwangalifu.

Soma pia hii > Madhara ya punyeto kwa wanaume

3.Kosa la tatu : KUMPALAMIA MWENZA WAKO BILA MAANDALIZI

Kama kuna kosa kubwa wanaume mnalitenda dhidi ya wenza wenu basi ni hili.

Yaani kuna wanaume wakifika tu chumbani utasikia mama nanihii sogea hapa nikulenge. Hakuna kumbusu, hakuna kumshika wala kumchezeachezea dada wa watu wewe ukifika tu sogea hapa nikulenge!

Nikupe siri moja leo. Kwenye tendo la ndoa mwanamke kile kitendo cha wewe kuingiza uume kwake ni cha mwisho kabisa yaani cha mwisho kabisa linapokuja suala la tendo la ndoa kwake.

Sasa mpo wanaume baadhi yenu ukitoka kazini unapitia bar unalewa weee huko mpaka saa tano usiku halafu unakimbia kurudi nyumbani na ukifika tu hata salamu tu hakuna tayari unataka huduma. Kuweni siriasi kidogo na wenza wenu jamani.

Mwanamke wa umri wowote anahitaji kuandaliwa kwanza kisaikolojia juu ya hilo tukio. Siku hizi kuna simu unaweza kuanza kumtumia sms za kumwamsha tangu ukiwa barabarani unarudi nyumbani.

Kila mara tumia japo dakika 20 kumuandaa tu mwenzio kabla ya kumvua nguo ya ndani. Kama ni mkeo na unamwamini hana magonjwa muandae kwa vyovyote utakavyoweza mhimu tu asiwe na magonjwa au mhuni mhuni maana kuna magonjwa ya kansa ya koo kama usipokuwa makini.

Vile vile hii isiwe kama vile sala ya baba yetu kwamba lazima kila siku na kila wakati iwe hivi, mara moja moja sana unaweza kumuambia tu njoo nikulenge lakini isiwe ndiyo desturi yako ya siku zote atakuchoka!

Mbembeleze ndiyo mkeo na ndiyo huyo ukiumwa saa nane za usiku wa kwanza kukusaidia, ni ubavu wako tafadhali mbembeleze na tumia muda mwingi kumuandaa kabla ya mechi yenu

Ukiwa mjanja wapo wanawake anaweza kufika hadi kileleni wakati tu ule akiandaliwa kiasi kwamba ukianza kumlenga unakuwa umebaki wewe huhitaji hata kutumia dakika nyingi kubaki hapo unalima ili kumfikisha kwani anakuwa alishafika zamani.

Wanawake ni watu wa hisia sana.

Hakikisha hana mawazo mawazo au stress ya aina yoyote maana kama ana stress kama vile wanawake wengine yupo chumbani anawaza madeni ya vicoba sasa huyu unaweza kukesha ukimuandaa na asiandalike. Kuwa karibu naye kumsoma nini kinamsibu na nini unaweza kufanya kumsaidia aondokane na hali hiyo ili arudi kwenye hali yake ya kawaida

Wanaume naomba tubadilike maandalizi kabla ya tendo la ndoa ni lazima kuanzia leo kama ulikuwa unakwepa hii hatua na unafanya mambo kijeshijeshi tu naomba ubadilike kuanzia leo.

4.Kosa la nne : Kutohakikisha ikiwa wenza wao wamefika kileleni au la

Tendo la ndoa ni mawasiliano ya pande mbili. Kila upande kuna njaa fulani lazima iondolewe.

Tafiti zinasema asilimia 70 ya wanawake wote duniani hawajawahi kufikishwa kileleni na wengine hata hawajuwi hivi kufika kileleni ndiyo kitu gani hasa.

Kwa kawaida hata iweje mwanaume lazima atafika kileleni iwe kwa kuwahi au hata kwa kuchelewa ila lazima atafika kileleni. Tafiti zinaonyesha wanaume wengi wanawahi sana kufika kileleni. Sababu za wanaume wengi kupatwa na tatizo hili ni nyingi ila hilo siyo somo la leo.

Sasa kwa sababu tu wewe mwanaume umefika kileleleni haina maana kuwa na mwenzi wako naye atakuwa amefika kileleni. Na hii ni shida.

Kama mwanaume lazima uhakikishe kwanza kwamba kabla wewe hujafika kileleni basi mke wako naye pia awe amefika kileleni!

Kwahiyo kosa la nne ambalo leo nataka uliache ni hii tabia ya kutokuhakikisha ikiwa mwenza wako naye amefika kileleni au la kabla hujageukia upande wa pili ujifunike shuka ulale.

Ndiyo najuwa wapo baadhi ya wanawake ambao hata ufanye nini bado hawezi kufika kileleni. Kwahiyo ni mhimu kuhakikisha pia kuwa mwenza wako ana akili yenye utulivu na hana mawazo mawazo (stress) yoyote.

Shida kubwa ya kosa hili kwa wanaume ni kuwa wanaume wenyewe asilimia kubwa huwa hawajuwi ikiwa wapenzi wao wamefika kileleni au bado. Ukijua ishara na dalili anazozionyesha mwanamke anapofika kileleni au anapokuwa amefikishwa kileleleni itakusaidia sana kuepuka kosa hili.

Ndiyo mapenzi hayana kanuni maalumu kwa watu wote, pia inategmea na umri na muda gani tayari mmeishi kama mke na mme. Kuna wakati mwanamke anaweza kukubali kushiriki tendo la ndoa ila kwa ajili yako tu mwanaume yeye muda huo hisia zake zinakuwa hazipo kwa ajili hiyo. Ikitokea hivyo pia itakuwa ni vigumu wewe mwanaume kumfikisha kileleni.

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume

UTAJUWAJE MKE AU MPENZI WAKO AMEFIKA KILELENI

Wanawake wengi wanatabia ya kudanganya kuwa wamefika kileleni kumbe hata kileleni kwenyewe hajuwi ni wapi.

Mara nyingi wanatumia mbinu ya kudanganya kama wanafika kileleni kwa kupiga kelele za kimahaba na wapo ambao huongea kabisa, utawasikia “ooh bebi I’m coming”. Hapo mwanaume utajiona dume la mbegu kumbe “hutoshi”. Wakati mwingine wanaume wanapata taabu sana kujua kama ni kweli wamewaridhisha na kuwafikisha wake zao au la.

Dalili 5 zitakazokuonyesha sasa anafika kileleni:

1. UTAONA MISULI YA UKE WAKE INAKAZA NA KUACHIA:

Mwanamke anapokaribia kutaka kufika kileleni utaona misuli kuzunguka uke kama inakaza na kuachia hivyo hivyo kwa sekunde kadhaa na utaona wazi mheshimiwa akibanwa na kuachiwa hivi. Ni wakati huu mwanaume hatakiwi afike kileleni kwani atamwacha mwenza wake pabaya sana.

Kadri mwanamke anavyokaribia kufika kileleni ndivyo na kasi ya kukaza na kuachia kwa misuli ya uke kutakavyokuwa wake kunaongezeka.

Kitendo hiki cha uke kumbana na kumwachia mzee kitaendelea kwa kujirudia rudia mpaka mwanamke amefika kileleni.

2. UKE UTAZIDI KULOA MAJI:

Hapa sasa unaweza kuwa na uhakika kwamba ameshafika mlimani kabisa. Haya maji maji au utelezi kidogo unatokea hapa ndiyo tunaweza ni kukojoa kwa mwanamke na hapo ndiyo na yeye anakuwa amefika kilelelni kama vile manii yanavyomtoka mwanaume anapofika kileleni. Kwahiyo wanawake nao huwa wanakojoa katika tendo la ndoa na ndiyo wakati huo yeye huhisi raha ambayo ni vigumu kuielezea.

G-spot inapopata msuguano wa kutosha hapo mwanamke ataweza kukojoa. G-Spot ni sehemu ipo sehemu ya juu ya uke wa mwanamke inch 2 kutoka juu kwenye mlango wa uke. Hamu hii ya kutaka kukojoa wanawake wengi huipata katikati ya tendo la ndoa, wengine wanaweza kuipata wakati wa maandalizi kama mwanaume anajuwa kuichezea vizuri G-spot ya mwanamke.

G-spot inapopata msisimko wa kutosha, inatoa taarifa kwa homoni ya kike kutengeneza hayo majimaji yakiwa tayari. Mwanamke utajisikia kutaka kukojoa na ukijiachia ili yatoke yatapitia kwenye urethra kama mkojo lakini sio mkojo bali ni majimaji ya kufika kileleni.

Wanawake wengi wakati wa kupeana raha na utamu kuna muda huwa wanajisikia kama kukojoa na wanaomba wakakojoe lakini kumbe ni majimaji ya kufika kileleni. Unashauriwa wakati mwingine kabla ya kushiriki tendo la ndoa ukojoe kabisa ili kibofu chako cha mkojo kiwe kitupu ili katikati ya tendo ukisikia kukojoa ujue unakaribia kufika kileleni. Kwahiyo jiachie na uwe huru lii uweze kupata raha na utamu wa kufika kileleni.

Si wanawake wote wanaweza kutoa majimaji mengi, kama ikitokea hujatokewa na hali hii usijisikie vibaya bali ujuwe kuwa upo katika kundi la wale wanawake ambao wakifika kileleni uke wao huwa unazidi kuloa badala ya kutoa maji kama mkojo kabisa.

3. MIGUNO NA MAKELELE YA KIMAHABA VITAONGEZEKA:

Hapa uwe makini kidogo. Wapo wanawake wao huwa na kelele wakai wote tangu mnaanza mpaka mnamaliza, mwanamke wa namana hii anaweza kumchanganya mwanaume asiye mjanja kutambua hizi ni kelele za kufika kileleni au ni kelele za kawaida tu.

Wanawake wengi wamedanganya waume zao kwa kutumia mtindo huu na mwisho wa siku huwa hata hawajafika kileleni. Utaweza kujua kuwa anadanganya pale kelele au miguno yake ikiwa katika mpangilio unaoeleweka kwa mfano (oooh yeah,oooh yeah,ooh yes kama cd iliyorekodiwa, hapo ujuwe unadanganywa).

Kelele za kufika kileleni mara nyingi huwa hazieleweki na wala huwa hazina mpangilio maalumu. Kwa kawaida kelele huwa za undani kidogo zikiambatana na lugha ya mwili inayoendana na makelele au miguno anayoitoa. Kinyume na hapo ujue anakudanganya.

4. CHUCHU HUANZA KUWA NGUMU:

Kwa kawaida mwanamke anapokuwa anazidi kupata hamu ya tendo la ndoa matiti yake huvimba kutokana na ongezeko la kasi ya mzunguko wa damu katika mwili wake, lakini chuchu zake huwa zinakuwa za kawaida. Hata hivyo kuna baadhi ya wanawake chuchu zao zinakuwa ngumu pale matiti yakivimba (hawa ni wachache sana).

Hivyo ni mhimu ujue mapema kabla hata tendo la kupeana raha na utamu halijakolea. Pale mwanzoni tu unapokuwa unapashana nae joto, jaribu kuzigusa au kuziminya chuchu zake taratibu kama ukiona ni laini halafu baadae katikati ya tendo zikabadilika zikawa ngumu, basi ujue upo uwezekano ama ulifanikiwa kumfikisha kileleni au alikaribia kufika lakini hakufanikiwa. Ikiwa umezikuta ngumu tokea mwanzoni basi huwezi tena kuzitumia chuchu kama dalili ya kukujulisha kuwa amefika kileleni au bado.

5. LUGHA YA MWILI:

Hapa anaweza kuwa anahema haraka haraka kwa sababu ogani zake za ndani na mishipa yake vitakuwa vinahitaji oksijeni zaidi ili aweze kufika kileleni salama.

Hivyo hivyo atazidisha kujikunjakunja, kujinyonganyonga au kujisogeza kwako. Kama atakuwa ametulia tu ujue bado hivyo ongeza bidii.

Unaweza kuona pia mikono yake anaikunjakunja hata kufinya shuka.

Kama mpo kwenye staili ile ya kizamani wengine hupenda kuiita ‘kifo cha mende’ utashangaa ghafla anaanza kukumbatia na kukushikilia kwa nguvu, heee kama kucha zake ndefu anaweza kukuachia alama kadhaa mgongoni au kifuani wakati mwingine anaweza akashindwa kujizuia akakung’ata kabisa!!!

Soma pia hii > Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

Kama wewe ni mwanaume na unawahi sana kufika kileleni kila siku tuwasiliane dawa ninayo kwa ajili hiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 (Usipige simu, usitume sms ya kawaida). Ninayo pia dawa nzuri ya asili ya kuondoa kitambi moja kwa moja, tuwasiliane.

Pokea dondoo na makala nyingine mhimu kuhusu nguvu za kiume kupitia WhatsApp bure, ili kujiunga tuma neno > Afya ya wanaume likifuatiwa na jina lako na mahali ulipo kwenye WhatsApp +255714800175

Usiku mwema kwako

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imesomwa mara 378

Imehaririwa


Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp Bonyeza HAPA tuchat WhatsApp