Maswali ninayoulizwa mara kwa mara na wanaume

Published by Fadhili Paulo on

Maswali ninayoulizwa mara kwa mara na wanaume

Leo nimependa kuchukua nafasi na muda huu kujibu kwa kina baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wanaume huko WhatsApp.

Aidha yapo pia maswali mengine ambayo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wavulana.

Wavulana ni watu wa jinsia ya kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 mpaka 23 hivi.

Wavulana bado wanaishi kwa wazazi wao hawajuwi lolote kuhusu kodi ya nyumba au gharama ya chakula, kila kitu bado wanapewa na wazazi wao na hivyo bado wanafikiri kila kitu unaweza kupata bure.

Unaweza kukuta mvulana anakutumia ujumbe WhatsApp usiku saa sita halafu usiku huo huo saa tisa anakuuliza mbona unachelewa kunijibu?

Kwa vile yeye muda huo alikuwa hapa kwenye blog anasoma basi anafikiri na mimi muda huo nipo macho, yaani hajuwi kama kuna muda na mimi huwa nalala au kuna siku na mimi nakuwa nimepumzika!

Basi ngoja niache hizo habari za wavulana na niendelee na kile hasa nimekusudia kuandika kwenye makala hii.

Maswali ninayoulizwa mara kwa mara na wanaume

1. Nina uume wa ukubwa huu, je ni ukubwa sahihi?

Hofu namba moja ya wanaume wengi ni juu ya ukubwa wa uume wao.

Nafikiri haya ni matokeo ya video mbaya wamekuwa wakiziangalia kwenye simu zao miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo mara kadhaa nimeshaandika juu ya ukubwa sahihi wa uume, ukubwa wa kawaida wa uume na uume mdogo kabisa unakuwaje.

Na nimeshaeleza pia kuwa ukubwa wa uume peke yake siyo jambo la mhimu sana kuliko yote linapokuja suala la mahusiano na ndoa kwa ujumla.

Unaweza kusoma kwa kina zaidi kwa kusoma makala zifuatazo;

> Je ukubwa wa uume una umhimu wowote kwenye mahusiano?

> Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

2. Je nirudie mara ngapi tendo la ndoa ili mchumba au mke wangu aone kuwa nina nguvu za kiume za kutosha?

Hili ni swali lingine nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wanaume.

Ni swali gumu na si matabibu wote wanapenda kuulizwa maswali ya namna hii.

Na ndiyo maana matabibu wengi hawapendi kuandika au kuzungumza juu ya mada zinazohusu tendo la ndoa au nguvu za kiume kwa ujumla.

Wanaona bora wakae na kuzungumza kuhusu vidonda vya tumbo au kisukari au presha za kupanda na kushuka lakini siyo nguvu za kiume.

Ni kazi ngumu kukaa unazungumza nguvu za kiume na ni moja ya kazi za aibu na inamhitaji mtu shujaa na shupavu kufanya hivyo.

Ndiyo maana nilikuambia pale mwanzo kwamba yale maswali wanayouliza wavulana sitayazungumzia kwa leo kwa sababu mengi ya hayo yanakera ila mimi nawavumilia na wakati mwingine nakaa tu kimya siwajibu chochote maana nina majukumu mengine mhimu kwangu na kwa familia yangu.

Maadui zetu bado ni UJINGA, MARADHI NA UMASKINI.

Kurudia tu tendo la ndoa mara mbili au mara tatu au hata mara nne siyo kigezo au ishara kwamba una nguvu za kiume.

Unaweza kurudia hata mara 7 kama utaweza na bado ukaonekana huna nguvu za kiume.

Hata matangazo mengi ninayosoma kwenye magazeti, kusikia kwenye redio au hata hapa kwenye mitandao wengi wanasisitiza wana dawa ya kumsaidia mwanaume arudie tena mzunguko mwingine kwenye tendo la ndoa.

Kwamba kwa mjibu wa wao kurudia tena ndiyo nguvu za kiume.

Hii ndiyo sababu nakutana na wazee hata wa miaka 60 wanalalamika eti hawana nguvu za kiume!

Baada ya miaka 50 kama mwanaume huhitaji tena kuwa bize sana juu ya nguvu za kiume.

Kwa asili kabisa ya binadamu mwanaume baada ya miaka 40 nguvu zake za mwili, za kiume na uwezo wake wa jumla wa kushiriki tendo la ndoa huanza kupungua pole pole na taratibu.

Ukiwa na miaka 55 hivi kwenda juu hapa unatakiwa uwe na hofu endapo tu uume wako hauwezi kabisa kusimama hata kama utamuona mama hapo hana nguo zote au hata baada ya mama kukushikashika sana na bado husimami hapo ndiyo unaweza kuwa na hofu.

Lakini kama unasimama na unaweza kwenda hapo dakika 5 au 7 au 8 basi wewe una afya nzuri na hupaswi kuhofu kuhusu nguvu za kiume.

Nguvu za kiume hasa ni suala linalowahusu watu wa miaka 20 mpaka 45 hivi hapo.

Baada ya miaka 45 unatakiwa upunguze baadhi ya vitu ili kulinda afya yako zaidi.

Miaka 45 kwenda juu lazima ujuwe pia hata baadhi ya mazoezi ya viungo si sahihi kwako na wala huwezi kufanya tena yale mazoezi ulikuwa ukiyafanya ulipokuwa na miaka 20 mpaka 35.

Pamoja na hayo yote bado kurudia tendo la ndoa mara mbili au tatu au hata mara nne siyo kigezo kwamba una nguvu za kiume.

Nguvu za kiume ni muda uliotumia kubaki hapo kwenye mchezo ndicho kinachoangaliwa siyo idadi ya mizunguko.

Kama unaenda dakika 4 halafu umemaliza kisha unapumzika dakika 15 au 30 unaenda mara ya pili nayo inachukua dakika 5 tayari umemaliza bado huna nguvu za kiume.

Lakini kama unaweza kwenda dakika 15 au 20 au 25 kwa mzunguko mmoja bila kuchoka wewe una nguvu za kiume hata kama hutarudia mara ya pili au ya tatu.

Kwa sababu mwisho wa siku ni lazima uhakikishe mchumba au mkeo amefika kileleni!

Basi hilo ndilo la mhimu siyo idadi ya magoli.

Kwa sababu wanawake wengi wanaweza kufika kileleni kuanzia dakika ya 7 tangu muanze mechi yenu.

Chini ya dakika 7 ni vigumu kwa mwanamke kufika kileleni.

Kwa hiyo tunaposema una nguvu za kiume tunaangalia vitu vikuu viwili, kwanza uwezo wa kudumu kwenye tendo la ndoa kwa dakika nyingi kuanzia dakika 7 kwenda juu na uwezo wako wa kuhakikisha mchumba au mke wako amefika kileleleni.

Ni hivyo tu na siyo kurudia mara ya pili au mara ya tatu.

Kwa maelezo zaidi soma makala zifuatazo;

> Nguvu za kiume siyo idadi ya mabao

> Dalili zitakazokuonyesha mkeo au mpenzi wako amefika kileleni

> Je wanawake huwa wanataka mwanaume adumu muda gani kitandani?

3. Je nikiwa sina nguvu za kiume naweza kumpa mke wangu ujauzito?

Hakuna uhusiano wa nguvu za kiume na uwezo wa mwanaume kumpa mimba mwanamke.

Na kama ingekuwa kwamba ni lazima uwe na nguvu za kiume ndiyo uwe na uwezo wa kutungisha mimba basi maisha yangekuwa ni magumu sana na kungekuwa na watu wachache sana duniani.

Ni jambo la kawaida kwa mwanaume kuwa na nguvu chini ya kiwango mara mbili hata mara tatu kwa mwezi. Ni jambo la kawaida linalowatokea wanaume mara kwa mara kwenye safari yao ya kuishi hapa duniani.

Hakuna mwanaume ambaye yeye kuanzia januari hadi disemba kila akishiriki tendo la ndoa anakuwa na nguvu za kiume.

Kwa hiyo ni kawaida kwa mwanaume kutokuwa na nguvu za kiume na bado akawa na uwezo wa kutungisha mimba na akazaa hata watoto kumi.

Kama unapata shida kutungisha mimba mkeo ni vema mkafanya vipimo kwanza wote wawili wewe pamoja na mkeo ijulikane ni nini kinazuia msipate mtoto.

Mwanaume fanya kipimo cha mbegu zako kuona kama zina ubora na uwezo wa kutungisha mimba.

Pima pia kuhusu homoni zako.

Ukipata muda soma na hii makala ifuatayo;

Dawa ya kuongeza mbegu za kiume

4. Je nikiwa na nguvu za kiume ndoa yangu haitavunjika?

Zipo sababu nyingi zinazoweza kuvunja ndoa yako na siyo lazima iwe ni nguvu za kiume.

Wamama wengi wanaishi na waume zao ambao hawana nguvu za kiume na maisha yanaenda miaka hadi miaka.

Kuna mambo mengine mengi yanayoweza kuvunja ndoa yako na mengine yapo nje ya uwezo wako.

Pamoja na hayo ukumbuke huyu mkeo pamoja na mambo mengine tendo la ndoa ni moja ya vitu alivyovikosa kwao hata akaamua kuondoka kwao na kuja kuishi na wewe.

Kama ni chakula hata kwao alikuwa anakula chakula.

Kama ni hela anaweza kuzipata kwa kufanya biashara au kulima mashamba au kuwa mfugaji na akapata hela bila hata kuhitaji kuwa na mwanaume au kuolewa.

Kwahiyo kama mwanaume unawajibika kuona kwamba unao uwezo wa kumtimizia haja yake hiyo ya kitandani.

Hivyo ni mhimu mwanaume uwe na nguvu za kiume kwani zinaweza kusaidia kupunguza migogoro isiyo ya lazima kwenye ndoa yako, lakini nguvu za kiume peke yake haziwezi kuzuia ndoa yako isivunjike kwa sababu kuna mengine mengi kwenye ndoa zaidi ya tendo la ndoa.

Kwa leo imetosha.

Kabla hujaondoka bonyeza na usome pia hii makala ifuatayo;

Dawa ya kuongeza nguvu za kiume, kuimarisha mbegu za kiume na kutibu saratani ya tezi dume

Share post hii na wengine uwapendao

Maswali ninayoulizwa mara kwa mara na wanaume Click To Tweet

Kama wewe ni mwanaume na una swali lingine zaidi ya haya niulize hapa chini kwenye comment nitakujibu na wala huhitaji kuandika jina lako kamili ili kuuliza swali lako.

(Visited 313 times, 1 visits today)

2 Comments

Robert · 07/10/2021 at 7:32 am

Kikawaida kw mwanaume asiye na tatizo lolote la nguvu za kiume, je kwenye kufanya mapenzi bao la kwanza linapaswa kuchukua muda gani Hadi kulimaliza.

    Fadhili Paulo · 13/10/2021 at 3:00 pm

    Bonyeza HAPA

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175