Mimba kuharibika maswali na majibu

Published by Fadhili Paulo on

Mimba kuharibika maswali na majibu

MIMBA KUHARIBIKA MASWALI NA MAJIBU

Hapo kabla tulisoma kuhusu dawa ya kuzuia mimba kuharibika, tuliona nini husababisha hali hiyo, dalili zake na vitu vinavyosababisha tatizo hili.

Leo tutaangalia baadhi ya maswali na majibu kuhusiana na mimba kuharibika na ikiwa unalo swali lingine tofauti na haya liulize tu hapo chini.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka

Uchunguzi wa kuharibika mimba hufanyikaje na kutibiwaje?

Uchunguzi wa mimba kuharibika hufanyika hospitalini. Hii inahusisha uchunguzi wa mfupanyonga na kipimo cha ‘ultrasound’ kinaweza kutumika pia kuthibitisha kuharibika huko kwa mimba.

Ikiwa mimba imeharibika kwa asilimia 100 na taka zote zimetoka, basi hakuna matibabu zaidi utakayopaswa kuyafanya.

Ikiwa haikuthibitishwa kuwa umepatwa na kuharibika mimba bali ulipatwa na dalili tu, utashauriwa kupata muda wa kutosha kujipumzisha.

Nitajuwaje kama nimepatwa na mimba kuharibika?

Unaweza ukapatwa kutokujisikia vizuri, unaweza kutokwa na damu nzito kidogo, homa, au maumivu ya mwili mara baada ya kupatwa na mimba kuharibika.

Unapopatwa na hayo wahi kuonana na daktari mapema. Na hayo yanaweza pia kuwa ni ishara ya kuwa una maambukizi (infection).

Naweza kupata ujauzito tena baada ya mimba kuharibika?

Ndiyo. Hadi asilimia 85 ya wanawake waliowahi kupatwa na kuharibika kwa mimba hupata ujauzito mwingine na kujifungua salama. Kupatwa na mimba kuharibika hakumaanishi kuwa una tatizo la ugumba.

Kwa upande mwingine wastani wa asilimia 1 ya wanawake wanaopatwa na mimba kuharibika hupatwa tena na tatizo hilo mara mbili hadi tatu zaidi na watafiti wanadai hii hutokana na kutikiswa kwa kinga ya mwili (autoimmune response).

Ikiwa umepatwa na mimba kuharibika mara 2 mfululizo unashauriwa kusimama kwa muda kuendelea kutafuta mtoto mwingine kwa miezi kadhaa huku ukipata vipimo na ushauri toka kwa daktari kubaini nini chanzo hasa cha tatizo hili kwa upande wako.

Lini nitafute ujauzito mwingine baada ya kuharibika uliopita?

Jadili jambo hili na daktari wako. Ikiwa umepatwa na mimba kuharibika mara 2 mfululizo unashauriwa kusimama kwa muda kuendelea kutafuta mtoto mwingine kwa miezi kadhaa walau isiwe chini ya miezi mitatu IKIWEZEKANA SUBIRI MIEZI SITA IPITE huku ukipata vipimo na ushauri toka kwa daktari kubaini nini chanzo hasa cha tatizo hili kwa upande wako.

Daktari wako pia anaweza kukushauri juu ya kutibu au kuiongezea nguvu homoni mhimu sana katika uzazi ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘progesterone’

Ni mhimu kujipa muda kujiponya kiakili na kimwili kutokana na kuharibika kwa mimba kulikotokea. Na mhimu kuliko yote usikae kujilaumu mwenyewe, hilo ni jambo linalowatokea watu wengi na ni jambo la kawaida kabisa.

Je kuharibika kwa mimba kunaweza kuzuiwa?

Kwa kawaida mimba kuharibika hakuwezi kuzuiwa na mara nyingi hutokea kwa sababu ujauzito wenyewe haupo sawa.

Ingawa ikiwa kuharibika kwa mimba kunahusiana na mlango wa uzazi kuwa na uwezo mdogo basi upasuaji unaweza kusaidia katika hilo.

Kile unaweza kufanya ukiona dalili za kuharibika mimba ni pamoja na kuacha kutumia sukari, soda yoyote, vilevi, chai ya rangi, kahawa, tangawizi, papai na vyakula vigumu.

Pendelea kutumia juisi ya parachichi, kunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima, tumia unga wa mbegu za maboga na vitu vyenye vitamini C ingawa vitamini C isitumike kwa wingi kwani nayo ikizidi hupelekea mimba kuharibika.

Wakati huo pata muda wa kutosha wa kupumzika na uwe unafanya maombi kwa Mungu muda wote.

Kuwa karibu na nesi au daktari wako wakati huu wote.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kuzuia mimba kuharibika

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

(Visited 923 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175