Mwezi uliozaliwa na aina ya magonjwa yanayoweza kuwa yanakusumbua mara kwa mara

Published by Fadhili Paulo on

Mwezi uliozaliwa na aina ya magonjwa yanayoweza kuwa yanakusumbua mara kwa mara 

Hakuna mtu anafahamu kwa hakika ya asilimia 100 ataumwa ugonjwa gani na ataumwa lini.

Hiyo bado ni siri ya Mungu.

Na kwa bahati mbaya ni kuwa kila mtu ataumwa kitu fulani wakati fulani kwenye maisha yake.

Siyo watu wote wanakufa kwa kuumwa, wengine hufa kwa ajali, wengine kwa vita, wengine kwa kukosa chakula nk.

Kila mtu ataumwa.

Ndiyo, hata kama wewe ni daktari au mganga na unatibu watu na wanapona bado na wewe siku moja utaumwa na utakufa pia kama wanavyokufa watu wengine wote!

Hata kama unaishi na daktari nyumba moja, bado na wewe kuna siku utaumwa na unaweza pia kufa kama watu wengine wote.

Na ndiyo maana wengine huamua kukata Bima ya afya kabisa ili siku akiumwa awe na uhakika wa kufika hospitali na kuonana na daktari.

Wengine hutenga kabisa kiasi cha fedha kama dharura ya matibabu siku wakiumwa.

Hii yote ni kwa sababu hakuna anayejua kwa hakika ataumwa nini na ataumwa lini.

Na vile vile hakuna mtu yoyote anayependa kuumwa chochote, huwa inakuwa imetokea tu na hatuna jinsi.

Sasa kuna jambo kwenye tiba ya asili nalo ni hili la uhusiano wa mwezi uliozaliwa na aina ya magonjwa yanayoweza kuwa yanakusumbua mara kwa mara.

Tiba ya asili ni jumla ya mambo mengi sana. 

Hakuna uthibitisho wa kisayansi wa jambo hili, lakini wanasayansi wenyewe kwenye utafiti mmoja wa kisayansi wa Chama cha Habari za Matibabu cha Marekani kwa kuangalia takwimu (data) za wagonjwa milioni 1 na laki 7 kati ya 1985 hadi 2013 waliweza kuona uhusiano huu wa mwezi uliozaliwa na aina ya magonjwa yanayoweza kuwa yanakusumbua mara kwa mara wa mpaka asilimia 55, lakini bado tafiti zaidi zinahitajika ili kupata hitimisho.

Unaweza kufanya na wewe uchunguzi binafsi wa jambo hili kama utapata muda.

Sasa tuone mwezi uliozaliwa na aina ya magonjwa yanayoweza kuwa yanakusumbua mara kwa mara ;

1. Januari > Shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo

2. Februari > matatizo kwenye mapafu

3. Machi > Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, magonjwa ya moyo na matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji

4. Aprili > Maumivu kifuani, matatizo ya moyo

5. Mei > Hakuna ugonjwa wowote

6. Juni > Maumivu ya kifua na pumu

7. Julai > Hakuna ugonjwa wowote

8. Agosti > Maambukizi kwenye macho

9. Septemba > Maambukizi kwenye mfumo wa upumuwaji, maambukizi kwenye masikio, homa na kutapika, pumu, matatizo yanayohusiana na uzazi na kuzaliwa

10. Oktoba > Matatizo kwenye mapafu, matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji, vidonda kooni, magonjwa yanayohusiana na virusi, udhaifu kwa wadudu kama vile mbu, matatizo yanayohusiana na uwezo wa macho kuona, kupata hedhi nzito na nyingi, matatizo kwenye uke au uume, matatizo ya tumbo na msongo wa mawazo

11. Novemba > Magonjwa yanayohusiana na virusi, kukosa umakini, matatizo ya uzazi, utegemezi kwa dawa za kutuliza maumivu, matatizo kwenye uke au uume, kuharisha, vidonda kooni, matatizo kwenye kujifunza

12. Disemba > Matatizo ya ngozi

Watafiti wanasema huenda hili linatokea kama matokeo ya hali ya hewa ya mazingira na nyakati ya wakati mama anapata ujauzito, wakati wote akilea ujauzito na wakati anapojifungua.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha Kinga yako ya mwili niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

(Visited 465 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175