Namna msongo wa mawazo unavyoleta tatizo la kuwahi kufika kileleni

Published by Fadhili Paulo on

Namna msongo wa mawazo unavyoleta tatizo la kuwahi kufika kileleni

Hali ya mfadhaiko inasemwa kutokea wakati ubongo unapokabiliana na tatizo la mvurugiko wa akili na kujikuta ukishindwa kuendana na hali zingine zinazohitaji umakini kwa wakati mmoja. Jambo hili linaweza kuuteka ubongo na kudhoofisha uwezo wake.

Hatimaye hali hii ya ufadhaikaji katika ubongo inaweza kutengeneza dalili tofauti ambazo zimepachikwa majina mengi kwa mjibu wa sampuli tabia za nje anazozionesha mtu.

Idadi kubwa zaidi ya watu wanazidi kupatwa au wanategemewa kupatwa na aina fulani fulani za mifadhaiko. Baadhi ya aina za mifadhaiko ni hali za asili katika hatua za maendeleo na kukua kwa mtu.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu uwezo wao ni mdogo kushughurika na woga, wasiwasi na hamaki zinazohusiana na mifadhaiko. Kwa bahati mbaya tena wanapotafuta msaada wa kitaaluma, wanapewa aina fulani za madawa.

Jina langu naitwa Fadhili Paulo. Endelea kusoma …

Kuna uhusiano wa moja kwa moja wa tatizo la kuwahi kufika kileleni au upungufu wa nguv za kiume na msongo wa mawazo (stress).

Hili ni jambo ambalo wanaume wengi huwa hawawazi sana kama linaweza kuwa ni chanzo cha tatizo la kuwahi kufika kileleni.

Tunapozungumzia nguvu za kiume kwanza kabisa hatuzungumzii nguvu za uume kama uume bali tunazungumzia nguvu za mwili. Nguvu za mwili zimegawanyika mara 2 ambazo ni nguvu za mwili kama mwili (physical energy) na nguvu za ubongo (Psycological energy).

Namna msongo wa mawazo unavyoleta tatizo la kuwahi kufika kileleni 1

Kwa sehemu kubwa tatizo la kuwahi kufika kileleni na udhibiti wake linategemea sana kiasi cha nguvu kilichopo kwenye ubongo na akili yako kwa ujumla. Kwa zaidi ya asilimia 80 ya nguvu zako kitandani zinategemea ubora wa akili yako ilivyo kwa wakati husika.

Ni ngumu au ni sawa na haiwezekani kwa mwanaume mwenye mawazo mawazo (stress) kuwa na nguvu kitandani. Hilo haliwezekani.

Kwahiyo unapokuwa bize kuepuka vilevi, kula vizuri na kufanya mazoezi ili kuwa na afya nzuri ya kiume ni mhimu sana kuangalia afya yako ya akili ikiwa ina utulivu wa kutosha au la.

Tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi hasa kama stress ya mwanaume husika inasababishwa na mwanamke mwenyewe anayeshiriki naye, hapa shida huwa kubwa mara tatu zaidi.

Tendo la ndoa ni hisia na linahitaji utulivu wa kutosha wa akili na ushirikiano kutoka pande zote mbili.

Msongo wa mawazo unaharibu nguvu zako kitandani kwa namna nyingi ambazo hujawahi hata kufikiri.

Unapokuwa na msongo wa mawazo (stress) mwili wako huzalisha homoni mbili zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘coritsol’ na ‘adrenalin’. Kutokea kwa hizi homoni mbili kunaleta pia mabadiliko mengi mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.

Stress inapelekea mwanaume kukosa kujiamini na kuishiwa kabisa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.

Tendo lenyewe ni tendo la furaha, sasa ukiwa una huzuni huzuni rohoni utawezaje kushiriki kwenye sherehe kwa amani na ubora unaotakiwa?.

Asilimia 80 za vyakula na vinywaji tunavyotumia inatumika na ubongo. Na ni ubongo ndiyo unaanza kuhisi kushuka kwa nguvu mwilini na hukuletea hisia za njaa ili ule chakula.

Ni mhimu sana kwa mwanaume kuwa na akili iliyotulia na utulivu wa nafsi kwa ujumla ndipo atakapokuwa na nguvu za kutosha kumwezesha kushiriki tendo la ndoa kwa ubora unaotakiwa.

Kama upo mwanamke unasoma ujumbe huu tambua kuwa unahitaji kumwacha mmeo katika hali ya kutulia na usimpe shida nyingi kila mara kiasi cha yeye kukosa amani kwenye nyumba yenu kwani hilo litaharibu pia afya yake ya kitandani.

Hili linaenda sambamba na mwanaume kuhakikisha anapata usingizi wa kutosha na wenye utulivu. Kwa kawaida nguvu za kiume kwa mwanaume zinatengenezwa kati ya saa tisa na saa kumi na moja usiku kama aliwahi kulala na amepata usingizi wenye utulivu.

Kama mwanaume hupati usingizi mzuri na wa kutosha hasa nyakati za usiku ni vigumu sana kwako kuwa na uwezo wa kuhimili tendo la ndoa kwa ufasaha zaidi. Mwanaume alale masaa saba mpaka nane kila siku na upate usingizi wenye utulivu.

Usingizi ni mhimu siyo kwa nguvu za kiume tu bali pia kwa kulinda na kuimarisha kinga ya mwili. Kama hupati usingizi vizuri ni rahisi kuwa na msongo wa mawazo na ni vigumu uwe na nguvu za kuweza kushiriki tendo la ndoa.

Kwahiyo kuanzia leo mwanaume unayepata tatizo la kuwahi sana kufika kileleni na unashindwa kurudia tena tendo kwa mara ya pili au tatu jikaguwe mwenyewe afya yako ya akili ina ubora wa kiasi gani.

Kama wewe ni mtu wa mawazo mawazo au huzuni huzuni tu muda mwingi pengine nikushauri uachane kwanza na mapenzi mpaka hapo utakapokuwa na utulivu wa kutosha wa akili na nafsi yako.

Unahitaji hali ya utulivu wa kutosha wa akili na nafsi ili uweze kushiriki kwa ufanisi wa juu wa tendo la ndoa.

Ili kuondoa msongo wa mawazo (stress) hatua ya kwanza ni kujikagua na kujua nini chanzo hasa cha tatizo. Hii ndiyo dawa ya kwanza ya stress. Bila kufahamu chanzo cha stress yako hakuna dawa itakayokutibu hilo, ni mpaka utakapofahamu chanzo cha stress yako ukiondoe hicho ndiyo utakuwa na uhakika wa kupona hili janga.

Stress nyingi ukiangalia sisi wanaume huwa tunajitakia wenyewe kuwa nazo. Wanaume wengi pamoja na mibaraka mingi ambayo Mungu amewapa kwenye maisha yao bado hawana roho ya kuridhika na vile walivyonavyo tayari.

Jitahidi uishi maisha simpo ya kawaida kabisa ambayo unayamudu. Kama una uwezo wa kuendesha baiskeli wewe endesha baiskeli na usikae kunung’unika mbona sina gari. Amini Mungu amekupa baiskeli na anafahamu inakutosha kwa wakati uliopo na muda ukifika atakupa pia gari.

Kwahiyo ridhika na hali yako, usitake mambo makubwa sana yaliyo nje ya uwezo wako. Na mhimu zaidi kumbuka hata uwe na nini, hata ununuwe ndege ipo siku utakufa na vyote utaviacha hapa hapa duniani hivyo visikupe homa na kukukosesha amani ya moyo.

Kama stress yako chanzo chake ni mkeo basi jaribu kuona namna mnaweza kuzimaliza tofauti zenu na mwenza wako na muendelee kuishi kwa furaha na amani.

Kama stress yako ni magonjwa basi muombe Mungu akukutanishe na daktari ambaye ataweza kulitatua tatizo lako. Kumbuka hakuna ugonjwa usio na dawa hata kama umeshatumia dawa nyingi bila mafanikio bado usikate tamaa tiba kwa ajili yako bado ipo ni vile tu hujakutana nayo.

Namna nyingine ya kudhibiti msongo wa mawazo ni kuwa bize na mazoezi ya viungo kila mara, kukaa karibu na watu mbalimbali, kutembelea sehemu zenye utulivu kama baharini, kwenye mbuga za wanyama nk

Nguvu za kiume ni nguvu za mwili. Nguvu za mwili zimegawanyika mara mbili, nguvu za mwili kama mwili na nguvu za ubongo wako ama akili yako kwa ujumla.

Stress ama msongo wa mawazo ndicho kitu kikuu kinachoharibu ubora nguvu zako za ubongo na nguvu za ubongo ndizo hasa zinahitajika ili uwe na nguvu za kutosha kitandani.

Kazi inabaki kuwa kwako mpaka hapo.

Utajuwaje kama una mfadhaiko wa akili? Soma dalili na ishara 50 za stress hizi hapa chini;

Zifuatazo ni dalili na ishara 50 za kuongezeka kwa mfadhaiko au stress katika mwili wako;

1. Kuumwa kichwa kila mara

2. Kusagika meno

3. Kushikwa na kigugumizi

4. Kuhamanika, Kutetemeka kwa mdomo na mikono

5. Maumivu ya shingo, Maumivu nyuma ya mgongo, Misuli kujikaza

6. Kuwa na mashakamashaka , kizunguzungu na wasiwasi usioisha

7. Kusikia sauti au mvumo katika masikio

8. Fadhaa na hasira za mara kwa mara, kutokwa na jasho bila kazi

9. Homa au jasho katika mikono na miguu

10. Mdomo kuwa mkavu na kupata shida katika kumeza chakula

11. Homa za mara kwa mara na maambukizi,

12. Upele, muwasho wa ngozi na mabaka mabaka katika ngozi

13. Shambulio la mzio/aleji lisiloweza kuelezewa la mara kwa mara

14. Kiungulia, maumivu ya tumbo na kujisikia uvivu

15. Hasira kupita kiasi na gesi kujaa tumboni

16. Kufunga choo, kuharisha na kupoteza uwezo wa kujidhibiti

17. Kupata shida katika kupumua na kupiga miayo mara kwa mara

18. Kupaniki kwa ghafla

19. Maumivu katika kifua, na moyo kwenda mbio

20. Kukojoa mara kwa mara

21. Kupungua hamu ya tendo la ndoa na ufanisi hafifu

22. Wasiwasi uliozidi, mashaka, kujiona na hatia na kutokutulia kwa neva

23. Kuongezeka kwa hamaki au pupa na kuchanganyikiwa

24. Majonzi na huzuni kuu

25. Kuongezeka au kupungua kwa hamu ya kula

26. Kukosa usingizi, kuota ndoto za kutisha na kukosa utulivu katika usingizi

27. Kukosa utulivu katika mawazo na maamuzi

28. Mgumu au mzito katika kujifunza jambo jipya

29. Kupoteza kumbukumbu au kusahausahau, kukosa mpangilio katika mambo yako mengi na kujisikia umevulugwa

30. Kuwa mgumu katika kufanya maamuzi

31. Kujisikia umezidiwa na kazi au mawazo

32. Kulia mara kwa mara ikiwemo mawazo ya kutaka kujiuwa

33. Kujisikia mpweke na usiye na thamani

34. Kupungua kujipenda na kuwa mchelewaji

35. Kuongezeka kwa fadhaa na mahangaiko ya akili

36. Kuzidi kukata tamaa

37. Kuhamaki na kujibu kwa nguvu nyingi hata katika maudhi madogo madogo tu

38. Kuongezeka kwa idadi ya ajali ndogo ndogo katika shughuli zako za kila siku (bahati mbaya nyingi)

39. Kuwa na tabia ya hofu iliyozidi

40. Kupungua kwa ufanisi au uzarishaji katika kazi zako

41. Kuongopa au kuomba msamaha kufunika kazi zako duni

42. Kuongea haraka haraka au kumumunya maneno

43. Kujitetea au kujilinda binafsi kulikozidi

44. Matatizo katika mawasiliano au kushirikiana na wengine

45. Kujitenga na jamii na kukaa peke yako

46. Kuendelea kujisikia uchovu na udhaifu

47. Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kutuliza maumivu

48. Kuongezeka uzito au kupungua uzito bila kupunguza chakula

49. Kuongezeka kwa uvutaji wa sigara, unywaji pombe au matumizi ya madawa ya kulevya

50. Kupenda vitu vya kubahatishabahatisha au kamari

Katika kujidhibiti au kujitibu na mfadhaiko au stress jambo la kwanza ni kutambua nini chanzo cha huo mfadhaiko wako, ukishapata kujuwa chanzo ni rahisi kupata suluhisho kwa haraka.

Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kusababisha maradhi mengi mwilini bila idadi.

Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa utaweza kujidhibiti kupatwa na mfadhaiko.

Mengine unayoweza kuyafanya ni pamoja na kunywa maji ya kutosha kila siku, kuacha kabisa vilevi vya aina yote mara tu unapojihisi umefadhaishwa au una stress nyingi, usikae mpweke hata mara moja, shiriki tendo la ndoa, fanya mazoezi kila siku, mazoezi ni dawa au tiba mhimu sana kwa mfadhaiko na mhimu kuliko yote ni kutokukaa kimya juu ya tatizo linalokusibu.

Kuna watu wakipatwa na matatizo huyaficha kimya na kuendelea kuumia ndani kwa ndani peke yao, hii ni tabia mbaya sana kiafya, unapopatwa na tatizo jaribu kutafuta mtu au watu unaowaamini na uwaeleze tatizo lako hata kama hawatakusaidia moja kwa moja lakini mawazo na ushauri wao tu vinaweza kuwa ni dawa tosha ya mfadhaiko au stress yako.

Namna msongo wa mawazo unavyoleta tatizo la kuwahi kufika kileleni 2

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 842

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *