Sababu kuu 10 za uume kusinyaa na kuwa mdogo

Published by Fadhili Paulo on

uume kusinyaa na kurudi ndani

Sababu kuu 10 za uume kusinyaa na kuwa mdogo

Kadri anavyoendelea kuishi kuna wakati utafika mwanaume ataanza kugundua uume wake umeanza kupungua na kuwa mdogo tofauti na alivyokuwa na miaka 20 mpaka 35 hivi..

Kusinyaa kwa uume ni jambo la kawaida ambalo hutokea katika umri mkubwa yaani kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea, lakini ikitokea katika umri chini ya miaka 50 basi hilo ni tatizo linalohitaji kutibiwa.

Miaka ya karibuni tunashuhudia tatizo hili likijitokeza hata kwa vijana.

Sababu kuu 4 za uume kusinyaa na kuwa mdogo kwa wanaume chini ya miaka 50

Kusinyaa kwa uume hutokana na;

 1. Kuwepo kwa msukumo hafifu wa damu sehemu kwenye uume,
 2. Maambukizi sehemu za siri ya muda mrefu hasa magonjwa ya zinaa
 3. Hitilafu katika misuli ya sehemu za siri za mwanaume inayoathiriwa na magonjwa ya zinaa
 4. Msongo wa mawazo (stress)
 5. Ugonjwa wa kifua kikuu (TB)
 6. Baadhi ya magonjwa sugu ya ngozi
 7. Ugonjwa wa kisukari
 8. Kupiga punyeto (kujichua)
 9. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
 10. Uvutaji sigara, bangi kupita kiasi, pombe kupita kiasi na matumizi ya dawa za kulevya ya muda mrefu

Dalili za uume kuanza kusinyaa:

Mwanaume mwenye tatizo hili hasa kijana yaani aliye chini ya miaka 50, huanza kuona;

 • Mfuko wa tezi dume umelegea na kushuka sana,
 • Mfuko wa tezi dume unasinyaa na kujikunja kunja,
 • Kokwa (tezi dume) huonekana ndogo na mishipa mikubwa ya damu huanza kujitokeza 
 • Mishipa ya mbegu toka katika kende (tezi dume) huonekana wazi.

Uume huwa kama wa mtoto mdogo na mishipa ya damu huchomoza wazi. Nguvu za kiume hupungua sana na endapo ukiweza tendo la ndoa la kwanza unawahi kumaliza na kushindwa kabisa kupata tendo la pili.

Mara kwa mara maandalizi kabla ya tendo la ndoa kwa mwanaume mwenye tatizo hili ni kuchezea sana uume kwa kuurusharusha au kuupiga piga kidogo kidogo ili kuamsha au kuhamasisha msukumo wa damu.

Baada ya hapo uume huanza kusimama taratibu na endapo utasimama basi inabidi uwahi tendo na kama utachelewa, basi uume utalala na kushindwa tena kufanya tendo kwa siku hiyo.

Tatizo la uume kusinyaa wakati wa tendo la ndoa

Uchunguzi wa tatizo;

Tatizo hili kama tulivyoona husababishwa na magonjwa mbalimbali, pia yapo matatizo na magonjwa mengine yanyochangia hali hii, magonjwa kama ya kisukari, kama ugonjwa utadumu kwa muda mrefu unaweza kuathiri hali hii.

Tabia ya kujichua ni moja ya sababu kuu ya uume kusinyaa hasa kama mtu atakuwa amejichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani msukumo wa damu sehemu za viungo vya uzazi utakuwa umeathiriwa.

Uume unaweza kupooza na kusinyaa kutokana na hitilafu katika mishipa ya fahamu.

Mishipa ya fahamu inapoathirika hasa kama matokeo ya kupiga punyeto au msongo wa mawazo wa muda mrefu viungo hupooza na mwanaume hushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa na ukeni hakuna kabisa mawasiliano yanayoleta msisimko.

Ukipata muda soma na hii > Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

Share makala hii na rafiki zako wengine uwapendao

Sababu kuu 10 za uume kusinyaa na kuwa mdogo Click To Tweet

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175