Sababu kuu 7 kwanini wanawake wanachepuka

Published by Fadhili Paulo on

kwanini wanawake wanachepuka

Sababu kuu 7 kwanini wanawake wanachepuka

Asilimia mpaka 45 ya wanawake waliopo kwenye ndoa wanachepuka.

Kumbuka sababu za mwanamke kuchepuka ni nyingi na hakuna namna wewe kama mwanaume unaweza kufanya ili kumzuia mkeo asichepuke.

Haijalishi wewe mwanaume ni nani na una nini.

Mkeo akiamua kuchepuka atachepuka tu, huwezi kumzuia.

Kuna vitu unaweza kufanya kama mme ili kuzuia uwezekano wa mkeo kuchepuka na vinaweza kusaidia hilo.

Lakini mwisho wa siku ni uamuzi wake BINAFSI yeye mwenyewe mkeo kuamua kwamba hataki kuchepuka kwa sababu yoyote ili kukuheshimu wewe na ndoa yenu.

Wanawake wanakutana na vishawishi vingi karibu kila siku.

Tofauti na mwanaume kwamba mpaka uamue au upange kwamba nataka nimtongoze mwanamke fulani, mwanamke yeye hapangi, akitoka tu nje kuna mwanaume fulani lazima atamtaka.

Wanasema mwanamke mzuri wa kawaida anaweza kutongozwa walau na wanaume tofauti 180 kwa mwaka.

Bila kupoteza muda hizi ni Sababu kuu 7 kwanini wanawake wanachepuka :

1. Ikiwa mmewe ni mtu asiyejiamini

Wanawake wana akili sana tofauti na wanaume wengi wanavyofikiri na kuwaona.

Mwanamke akikusoma na akakuhitimisha kwamba hujiamini na kuwa umekufa kwake mazima basi hiyo inaweza kuwa ni sababu ya yeye kuchepuka.

Unaambiwa dume lenye uhakika halimchungulii mkewe.

Mwanaume ukiona kila mara upo bize unamwambia mkeo asichepuke, asikusariti basi tegemea atafanya hayo bila wasiwasi wowote.

Ni kama mtoto anapokua kama mzazi upo bize kila siku kumwambia usifanye hiki usifanye kile kila siku hayo ndiyo mahubiri yako kwake amini kuna siku lazima atafanya hayo hayo unayomkataza kila siku.

Atataka kujua kuna nini hasa?

Mbona baba yupo bize sana na kunikataza hili kwani kuna nini hasa huko?

Na atataka ajaribu aone matokeo.

Hata mkeo unao uwezo wa kumwambia mara moja moja mke wangu naomba usichepuke, naomba unilindie penzi langu kwako.

Mara moja moja.

Lakini akiona kila siku wimbo wako ndiyo huo huo, mara uwe bize kupekua simu yake, mara kila mara utake kujua yupo wapi!

Atajuwa wazi hujiamini, atajuwa umekufa na kuoza kwake na atatumia huo huo udhaifu wako kuchepuka.

2. Ni mwanamke mpenda hela sana

Je ni kweli amekupenda kutoka moyoni na amekupenda wewe kama ulivyo au amekupenda sababu una pesa?

Kuna baadhi ya wanawake mawazo yao yote masaa yote yapo kwenye hela tu.

Mwanamke wa aina hii yeye yupo bize zaidi na pesa ulizonazo na bata unazoweza kumfanyia kuliko hata kukuwaza au kukujali wewe.

Kwa hiyo mara utakapoishiwa pesa au mara tu maisha yako yatakapoyumba basi uwe na uhakika mwanamke huyo lazima atachepuka.

Kwa sababu hitaji lake kubwa siyo mahusiano au uwepo wako, hitaji lake kubwa muda wote ni pesa.

Tabia ya kupenda pesa kupita kiasi ndiyo sababu kubwa na sababu ya kwanza ya wanawake wengi waliopo kwenye ndoa kuchepuka.

Kwa mwanaume ni kupoteza muda wako bure kuishi na mwanamke wa aina hii.

Mwanamke huyu kuishi naye itakulazimu uwe na uhakika na pesa wakati wote.

Na shida kubwa hapa ni kuwa mara zote kutakuwa na mwanaume mwingine mwenye pesa nyingi kuzidi wewe sasa sijuwi utafanyaje kumdhibiti mwanamke wa aina hii.

Hawa mara nyingi unaweza kukuta unaishi naye ndani lakini ukasikia amenunua kiwanja au amejenga nyumba kwao au sehemu fulani bila hata kukujulisha wala kukushirikisha wewe.

Anakuwa pia na tabia fulani za kutaka kushindana au hata kukuzidi wewe.

Hela ni kitu mhimu hakuna asiyefahamu hilo lakini maisha siyo hela tu.

Kuna mengi kwenye maisha zaidi ya hela.

3. Ikiwa mwanamke anapitia magumu kwenye ndoa yake

Watu wengi huwa wanafikiri ndoa ni sherehe na furaha tu kila siku jambo ambalo si kweli.

Ndoa ina misimu na vipindi vingi.

Kuna wakati wa furaha tu, pia kuna wakati wa kugombana au kutofautiana.

Kila ndoa ina shida zake.

Kila ndoa ni ya pekee.

Kila wawili uwaonao kuna muda fulani wananuniana na kugombana.

Ndivyo maisha yalivyo.

Badala ya kutoka nje ya ndoa na kutafuta faraja na tulizo ni vizuri ukikaa na mmeo na kuyatatua matatizo yenu ikiwa yanaweza kutatulika.

Changamoto zipo kwa ajili ya binadamu na unapozivuka na kuzishinda ndiyo maana hasa ya kuishi.

Sasa kuna mwanamke mwingine badala ya kupambana na tatizo uso kwa uso anaanza kutafuta njia rahisi za kulikimbia tatizo na kuchepuka.

4. Ikiwa mwanamke hafikishwi kileleni

Hili siyo kosa la mwanamke moja kwa moja.

Shida kubwa ya maisha ya ndoa ni kuwa mara nyingi mnafundishwa namna ya kusali pamoja, namna ya kupendana na kujaliana lakini hakuna wakati wowote mtafundishwa namna ya kutoshelezana kitandani.

Wazazi, viongozi wa dini na walezi wenu wengine wote hakuna hata mmoja atakayewaeleza tendo la ndoa linafanyika hivi na hivi.

Wanawake nao kwa asili wanategemea mwanaume utakuwa unafahamu namna ya kumfikisha kileleni na kumtosheleza mkiwa kitandani.

Kwa bahati mbaya zaidi ya asilimia 80 ya wanaume wengi wanapoingia kwenye maisha ya ndoa huwa hawajuwi namna nzuri na sahihi ya kushiriki tendo la ndoa.

Wanaume wengi hawajuwi namna ya kumfikisha mwanamke kileleni, wengi wana tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.

Wanaume wengi wameathirika na punyeto tangu wakiwa mashuleni.

Kwa kifupi tu niseme hili ni SHIDA sana hasa kwa kizazi hiki cha sasa cha smartphone na youtube.

Wengi hawajuwi hata ishara tu za mwanamke anayefika kileleleni.

Kwa hiyo kama mwanamke hafikishwi kileleni na hatimiziwi hitaji lake hilo mhimu la kitandani kuna uwezekano mkubwa akachepuka.

Shida huwa kubwa zaidi iwapo mwanamke huyo kabla ya kuolewa na wewe amewahi kushiriki na mwanaume mwingine na alifikishwa kileleni na anaifahamu raha hiyo ya kufika kileleni.

Kuna mwanamke kama hutaweza kumfikisha kileleni hata umpe nini lazima atachepuka.

Wanawake wengine wanaweza kuumwa hadi kichwa ukadhani ni mgonjwa kumbe tu ana tatizo hajafikishwa kileleni muda mrefu.

WAPO WANAWAKE WA NAMNA HIYO KAMA ULIKUWA HUJUWI BADO.

Kama unapenda kujifunza mengi kuhusu nguvu za kiume bonyeza hapa.

5. Ikiwa mwanamke anahisi unamdharau

Wapo baadhi ya wanaume hawawajali na kuwaheshimu wake zao.

Mwanaume yupo bize na kazi masaa 24, muda wote yupo ofisini au kwenye biashara zake na kutwa nzima inaweza kupita hajampigia simu wala kumtumia hata sms mke wake.

Mwanaume anafanya mambo yake binafsi bila hata kumshirikisha mkewe.

Mwanamke akihisi tu unamdharau inaweza kuwa ni moja ya sababu ya kuchepuka.

Wanawake hawapendi kudharauliwa.

Hawapendi uwaone kama vile hana maana au faida kwako.

Mwanamke anahitaji zaidi muda wako na support yako kuliko hata hela au kufikishwa kileleni.

Wapo baadhi ya wanaume ni wajinga sana kisa tu ana hela basi anaweza kuchepuka na wasichana au wanawake wengine mtaa huo huo mmoja wanapoishi na mkewe hadi majirani na mkewe mwenyewe wanasikia na kuona.

Hakuna mwanamke mwenye akili zake timamu anaweza kuvumilia ujinga huo siku zote.

Kuna baadhi ya wanaume wanafikiri kuchepuka ndiyo uanaume au urijali na hufanya hivyo mpaka wanagundulika na wake zao.

Kumbuka na yeye ni binadamu na ana damu na moyo kama wako.

Yakimzidi atataka tu kulipa kisasi na ndiyo mwisho wake ni kuchepuka.

Hata kama mkeo ni masikini, wapo ambao wapo tayari kuwa maskini kuliko kuishi kwa kudharauliwa.

6. Ikiwa mwanamke hatimiziwi mahitaji yake ya msingi

Mahusiano yanahitaji muda, nguvu na pesa.

Sasa kama baba hata kodi tu ya nyumba kwako ni shida kwanini mkeo asichepuke?

Yaani unakuta mwanaume hata uwezo wa kununua tu chakula kwa ajili ya familia yake hana.

Kama mwanamke naye ana mahitaji yake fulani ya msingi.

Huyu siyo mwanamke mpenda pesa sana bali amekukubali kwa jinsi ulivyo lakini shida ni kuwa wewe mwenzangu mwanaume hata kumnunulia tu kitenge kimoja au gauni moja kwa mwaka huwezi.

Hata kama ana kazi yake au biashara yake, bado huyo ni kama mwanao.

Kuna mahitaji fulani madogo madogo anahitaji umsaidie.

Hata yeye ana wazazi, ana ndugu wanaomtegemea pia.

Kumbukeni hapa nazungumzia mahitaji ya msingi.

Isije kutokea mwanamke anakulazimisha umnunulie gari mwambie hilo siyo hitaji la msingi hasa ikiwa ni kweli huna uwezo huo.

Soma pia hii 👇

Nguvu za kiume siyo idadi ya mabao

7. Ikiwa ana marafiki ambao wanachepuka

Marafiki wa mkeo ni watu mhimu sana wanaoweza kumbadilisha tabia mkeo bila wewe kujua.

Kama ana marafiki ambao wanachepuka na wanamwambia hilo ni jambo la kawaida basi ni rahisi sana hata mkeo kuchepuka.

Ni mhimu sana kuwa na marafiki wazuri ambao mnaweza kuwa kwenye ukurasa mmoja.

Marafiki wabaya wa mkeo ni hatari kwa ndoa yenu.

Kama mwanaume kuwa na busara na hekima unapojadili jambo hili na mkeo sababu siyo jambo rahisi kama unavyoweza kufikiri.

Nenda naye pole pole hadi akuelewe.

Usimlazimishe kwa nguvu au kwa fujo na kwa haraka haraka abadili marafiki zake.

8. Ikiwa mwanamke amekuchoka au amekukinai

Hii ni moja ya sababu inayoweza kumfanya mwanamke achepuke.

Kama amekuchoka au amekukinai anaweza kuchepuka.

Wanawake wanapenda vitu vipya na vinavyosisimua kila mara.

Kama mmekaa pamoja miaka mingi na huna jipya wala maajabu mengine basi ni rahisi sana mkeo kuchepuka.

Kuepuka hili mwanume jaribu kuwa mbunifu, jaribuni mambo mengine mapya.

Siku nyingine nendeni mkalale nyumba ya wageni (guest house) siyo kila siku nyumbani tena chumbani na kitanda hicho hicho kimoja.

Ina-boa.

Nendeni likizo nje ya mji, kasalimieni ndugu na jamaa mikoa mingine.

Safirini.

Ikiwezekana muachane kidogo huyu aende huko na huyo aende huko baada ya mwezi au muda fulani tena muonane.

Inasaidia kuamsha upendo na hamasa upya.

Mhimu kufahamu ni kuwa hali ya kumchoka mwenzako huwakuta watu wa jinsia zote mbili tena wanaume ndiyo wanaongoza kuwahi kuwakinai wake zao.

Ni jambo la kawaida na la asili kabisa kwa mwanadamu, usiwe na hofu.

Hakuna mtu asiyependa vitu vipya.

Jaribu au fanya utafiti zaidi na wewe.

Share post hii na wengine uwapendao

Sababu kuu 7 kwanini wanawake wanachepuka Click To Tweet

Kabla hujaondoka soma pia na hii 👇

Mkeo akikupenda SANA anaweza kuchepuka

(Visited 1,109 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175