Shinikizo la juu la damu chanzo na tiba yake

Published by Fadhili Paulo on

Shinikizo la juu la damu chanzo na tiba yake

Nini maana ya shinikizo la juu la damu?

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la juu la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la juu la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

1. Uvutaji sigara
2. Unene na uzito kupita kiasi
3. Unywaji wa pombe
4. Upungufu wa madini ya potassium
5. Upungufu wa vitamin D
6. Umri mkubwa
7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Uanishaji wa shinikizo la damu

Presha ya kawaida <120 <80
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 =180 =110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini.

Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu.

Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes)

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za shinikizo la damu:

*Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
*Kuchanganyikiwa,
*Kizunguzungu,
*Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
*Kutoweza kuona vizuri au
*Matukio ya kuzirai.
*Uchovu/kujisikia kuchokachoka
*Mapigo ya moyo kwenda haraka
*Kutokuweza kuona vizuri
*Damu kutoka puani

Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

Kutokulielewa shinikizo la juu la damu na kuendelea kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

*Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
*Shambulio la moyo (heart attack)
*Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
*Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
*Kiharusi
*Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
*Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; “Salt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo.

Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea.

Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Soma hii pia > Ukweli kuhusu Chumvi na Maajabu yake

Dawa ya asili inayotibu shinikizo la juu la damu > Banaba Mix

BanaBa Mix

 

Banaba Mix ni dawa ya asili ya mitishamba ambayo;

>Ina madini ya kutosha ya potasiam ambayo ni mhimu ili kuweka sawa usawa wa shinikizo la damu mwilini
>Banaba mix ina madini, vitamini na viinilishe vingine mhimu kwa ajili ya kudhibiti shinikizo la juu la damu vikiwemo vitamini C, kalsiam, magensaimu, folate, phosphorus na potasiam
>Potasiamu ni madini mhimu sana linapokuja suala la kudhibiti shinikizo la juu la damu
>Banaba mix inasaidia kupunguza uzito wa mwili, uzito uliozidi ni sabbau kuu ya kutokea kwa shinikizo la juu la damu
>Banaba Mix inaondoa pia kolesto na kutibu kisukari aina ya pili

Mambo mengine 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la juu la damu:

*Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
*Kula nyama isiyo na mafuta mengi
*Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
*Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
*Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
*Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
*Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
*Acha kunywa pombe
*Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
*Punguza mfadhaiko au stress
*Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.

Ikiwa utahitaji Banaba Mix kwa ajili ya shinikizo la juu la damu, niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175.

Soma pia hii > Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Shinikizo la juu la damu chanzo na tiba yake Click To Tweet

Tafadhari share post hii na wengine uwapendao.

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175 Nifuate kwenye Twitter

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp Nipigie simu ya kawaida 0714800175