Siri 5 za watu wanaofanikiwa kuishi miaka mingi

Published by Fadhili Paulo on

siri za kuishi miaka mingi

Siri 5 za watu wanaofanikiwa kuishi miaka mingi

Hakuna mtu asiyependa kuishi miaka mingi.

Hakuna mtu anayependa kufa mapema.

Kila mtu anapenda kuishi walau miaka 100.

Anayepanga uishi miaka mingapi kwa sehemu kubwa ni Mungu peke yake.

Kwenye suala la kuishi miaka mingapi mwenye uwezo wa kudhibiti hilo ni Mungu peke yake ambaye yeye ana uwezo wa kuamua hilo kwa asilimia mpaka 98 huku asilimia 2 tu ndiyo zipo chini ya uwezo wako.

Wewe mwanadamu una asilimia 2 tu za uwezo wa kuamua uishi miaka mingapi na kuna mambo ambayo ninajadili kwenye makala hii unayoweza kuyatekeleza ili uweze kuishi miaka mingi.

Siri 5 za watu wanaishi miaka mingi duniani;

1. Wapo kwenye mahusiano

Sifa kuu ya kwanza ya watu wengi wanaoishi miaka mingi ni kuwa wapo kwenye mahusiano.

Hili linaweza kukushangaza sana maana kuna uwezekano mkubwa ulikuwa unadhani ili kuishi miaka mingi unahitaji mboga za majani, matunda na mazoezi ya viungo.

Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kanuni ya kwanza ili uishi miaka mingi ni kuwa kwenye mahusiano.

Ni vigumu kwa mtu asiye na mahusiano yoyote kuishi miaka mingi hata kama atakuwa bize na mazoezi ya viungo na kula mboga za majani kila siku.

Binadamu kaumbwa hivyo.

Tumeumbwa kama jamii na siyo mtu mmoja mmoja.

Huwezi kuishi kama kisiwa na utegemee uishi miaka mingi.

Ili kuishi miaka mingi unahitaji kuwa kwenye mahusiano hasa mahusiano bora na sahihi kwako.

Ninaposema mahusiano namaanisha kuwa na mchumba au mpenzi au mke au mme, kuwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Siyo lazima uwe na marafiki 5000 facebook, hapana; kwanza marafiki wengi wa kwenye facebook ni marafiki feki na huwezi kuwaona unapopata shida au tatizo.

Walau uwe na marafiki sahihi na bora 10 ni sawa kuliko kuwa peke yako au uwe na marafiki wengi ambao ni marafiki feki.

Unapokuwa na mahusiano na mtu mwingine au na watu wengine ambao ni sahihi kwako hao hugeuka na kuwa msaada mkubwa wakati utakapohitaji msaada kwani hakuna binadamu anayejiweza mwenyewe kwa kila kitu.

Msaada siyo lazima uwe hela au kitu fulani.

Hata mawazo tu au ushauri fulani vinaweza kuwa msaada mkubwa kwako.

Unaona? mimi hapa kwa mfano ninapoandika maelezo haya kuna mtu yanamponya na yanaweza kumuongezea maisha na miaka tele ya kuishi kwa kusoma tu maelezo haya hata kama hajanunua bidhaa yoyote kwangu au hajanilipa chochote!

Maelezo haya tu kuna mtu yanamsaidia na wapo watu hasa wale wenye moyo wa shukrani watakaokuwa tayari hata kunipa zawadi au hata kuninunulia soda kwa maelezo haya tu.

Najuwa na ninafahamu watu wengi hawana shukrani, na hata elimu kama hizi wanachukulia poa na kudhani wanastahili kupewa au kuandikiwa bure, hawajuwi huwa natumia muda mwingi na hela ili kuziandaa na kuziweka hewani kila mwezi mwaka hadi mwaka.

Kwahiyo unapokuwa kwenye mahusiano ni rahisi kupata msaada pale utakapohitaji kwa sababu kwa asili hakuna binadamu anayejiweza kwa yote.

Unapokuwa ni mtu wa kuwa peke yako huna mchumba, huna rafiki, huna ndugu wa karibu wala jamaa ni rahisi kuwa na afya mbovu na unaweza kupata au kuwa na matatizo mengine ya kiafya kama vile;

  • kuwa na uzito uliozidi,
  • shinikizo la juu la damu,
  • kuganda damu
  • homa za mara kwa mara
  • msongo wa mawazo (stress)
  • kushuka kwa kinga yako ya mwili
  • kujihusisha na punyeto au kujichua
  • kuwaza kujiua (sucide)
  • kuwa mlevi sana nk

Tafiti zinaonyesha watu walio kwenye mahusiano sahihi wengi wao wana afya nzuri na wanaishi miaka mingi bila kulazwa hospitali au kuugua ugua kila mara.

Ni jambo zuri, ni sahihi kabisa kuwa na marafiki.

Kinachosisitizwa hapa ni kuwa kwenye mahusiano sahihi.

Ukiwa kwenye mahusiano mabaya ni rahisi tena kuwa na afya mbovu na hata ukafa mapema.

Unapoona mahusiano uliyopo si sahihi na yanakuharibia afya yako na ustawi wako kwa ujumla unatakiwa ujitoe haraka na utafute mahusiano mengine tulivu na sahihi kwako.

Na pia ni mhimu kujichunguza ili isije kuwa wewe mwenyewe ndiyo kikwazo namba moja cha kuwa kwenye mahusiano.

Kama umeshaachana na wachumba watatu au watano kuna uwezekano una tatizo fulani unalopaswa kujirekebisha. Haiwezekani watu watano au marafiki watano wote wawe wabaya.

Kwa hiyo kama unapenda kuishi miaka mingi hakikisha una mpenzi, una mchumba, una mke au mme, una marafiki, na una ndugu na jamaa sahihi kwako na siyo uishi peke yako.

Kama wewe ni mwanaume na unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume au kwa ajili ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kumbuka nimeandika nitafute WhatsApp, sijaandika nipigie simu.

Ukipata muda soma hii pia > Je madhara ya punyeto hupotea baada ya muda gani

2. Wanaishi kwa kusudi fulani

Watu wengi wanaoishi miaka mingi wengi wao ni watu ambao maisha yao wametumia kuishi kwa kusudi fulani (purpose).

Kama wewe ni mtu wa kuamka hujuwi uelekee wapi, huna watu wanaokutegemea au huna malengo yoyote ya maisha yako au ya watu wako ni vigumu uishi miaka mingi.

Mtu anayeishi kwa kusudi fulani ana watu wanaomtegemea na kumhitaji.

Inawezekana ana watu 10 au watu 200 au watu 10000 na kuendelea wanaomhitaji.

Mtu wa namna hiyo lazima ataishi miaka mingi.

Kuna mtu ana wazo fulani zuri kwa ajili ya kijiji chake au mtaa wake au wilaya yake au mkoa wake au nchi yake na hata dunia yake; mtu huyu hawezi kufa haraka ili atimize wazo hilo.

Unapoishi kwa kusudi fulani ni rahisi wewe kuishi kwa kujilinda na kujiepusha na mambo yasiyofaa kwa sababu unajuwa kuna watu wanakuhitaji na kukutegemea hivyo utajilinda kwa ajili yao.

Unapoishi kwa ajili ya kusudi fulani na kwa ajili ya watu wengine huwezi kuchukua uamuzi wa kwenda kujinyonga au kujiua kwa sababu tu umeudhiwa na mtu mmoja.

Unatambua kuwa ni kweli umechukizwa na mtu mmoja lakini hapo hapo unakumbuka kuwa kuna watu wengine 10000 wanakuhitaji, hilo tu litakusaidia kushusha hasira zako ili kuruhusu maisha yaendelee kwa maslahi na ustawi wa watu wengine wanaokuhitaji.

Mfano mdogo ni kwenye maisha ya wanandoa, wengi hata kama wanagombana na kuchukizana bado utaona baba na mama wanaendelea kuishi pamoja au nyumba moja lakini kwa kigezo kikubwa ili kulinda watoto.

Ni kawaida kusikia kwenye ndoa nyingi mmoja wa wanandoa akisema isingekuwa ni kuwaonea huruma watoto ningekuwa nimeshaondoka ila navumulia ili watoto wakuwe waweze kujitegemea.

Kadharika ni kawaida kumuona mtu mwenye cheo cha waziri wa wizara fulani akiwa disko au kwenye ukumbi fulani wa starehe usiku wa manane, lakini ni vigumu kumuona Rais kwenye ukumbi wa disko.

Hata kama ulikuwa unapenda sana kwenda disko ukishakuwa tu Rais unatakiwa usahahu hayo kwani uhai wako na maisha yako vinahitajika na kutegemewa na watu wengi hivyo huwezi kupata nafasi ya kuwa disko kwani huko lolote linaweza kutokea na tukalazimika kuingia gharama za kufanya uchaguzi mwingine.

Sasa ninaposema kuishi kwa kusudi fulani siyo lazima liwe kusudi kubwa sana labda kama hilo la kuwa Rais wa nchi, hapana; mhimu tu uwe na malengo na mipango fulani ya maisha yako na uwe na watu wanaokuhitaji au kukutegemea.

Kadri unavyokuwa na watu wengi wanaokuhitaji na kukutegemea ndivyo kusudi lako linavyokuwa kubwa na ndivyo utakavyokuwa makini na maisha yako ya kila siku ili kujilinda mwenyewe na kuwalinda au kutowaangusha wengine wanaokutegemea.

3. Hawana mambo mengi

Watu wengi wanaoishi miaka mingi huwa hawajishughulishi na mambo mengi au shughuli nyingi.

Njia rahisi na nyepesi kabisa ya kufupisha maisha yako ni kuwa mtu wa mambo mengi au shughuli nyingi.

Kadri unavyokuwa na mambo mengi na shughuli nyingi ndivyo maisha yako yanavyozidi kuwa mafupi.

Ni mhimu kuchagua jambo moja au shughuli moja utakayokuwa na muda wa kutosha wa kuisimamia kwa kipindi kirefu cha kuishi kwako.

Ubongo wa binadamu unapotumika sana kwa mambo mengi ndivyo afya ya mtu inavyozidi kuwa mbaya.

Hata kama unategemewa na watu wengi jitahidi wasikutegemee kwa kila jambo au kwa kila sekta kwani huko ni kuhatarisha maisha yako mwenyewe pasipo kujua.

Kazi nyingi kwa wakati mmoja (multitasking) ndiyo kitu kinaharibu sana afya za watu wengi bila wao kujua.

Kama unataka kuishi miaka mingi, punguza kazi, punguza kuhangaika sana na kila jambo.

Chagua kazi moja au shughuli moja na uifanye kwa ubora wa hali ya juu hapo ndiyo utaishi miaka mingi.

Lakini kama wewe ni daktari wakati huo huo ni mwalimu wakati huo huo ni hakimu wakati huo huo ni mkulima wakati huo huo ni mfugaji wakati huo huo ni mfanyabiashara; ndugu yangu kwanini usife haraka?

4. Hawajali sana juu ya wengine wanafikiri nini

Siyo kwamba hawajali kabisa, hapana, bali HAWAJALI SANA.

Ili uishi miaka mingi usiwe mtu wa kujali sana watu wengine wanakuonaje au wanasemaje kuhusu wewe.

Kwa kifupi ni kuwa watu watakusema tu hata uweje, ndiyo kawaida ya binadamu hawawezi kujisema wenyewe lazima watafute mtu wa kumjadili na kumsema.

Ukiwa ni mtu unayejali sana, ukiwa ni mtu unayefikiri sana kuhusu watu wengine wanavyokuona na kufikiri juu yako huwezi kuishi miaka mingi.

Jifunze kuishi maisha yako, yakubali na uyapende maisha yako.

Ndiyo maisha yako na ndiyo uliyoyachagua mwenyewe mwingine yoyote hayamhusu.

Usisahau sijasema usiwe mtu usiyejali kabisa, hapana, unaweza kujali kidogo na usikilize nini watu wanasema juu yako pengine inaweza kukusaidia kuboresha sehemu ya maisha yako lakini isiwe shida na lisiwe jambo la kukunyima usingizi.

Watu wanaoishi miaka mingi ni watu wanaopenda kucheka, ni watu wanaopenda kuchukulia poa baadhi ya vitu na hawapo siriasi muda wote.

Ukiwa ni mtu wa kufuatilia kila kitu na kuwa bize na kila kitu ni vigumu wewe kuishi miaka mingi kwa sababu ubongo wako utakuwa na uchovu muda wote jambo litakalopelekea kuwa na magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyo na maana wala sababu.

Mambo mengine achana nayo, mengine yadharau tu na mengine samehe tu maisha yaendelee.

Kama kuna mtu anakudharau na kukuchukulia wewe ni maskini na unajiona kabisa wewe siyo maskini jaribu kumpotezea na uendelee na maisha yako kwa sababu kuna uwezekano huyo mtu hajuwi hata umaskini ni nini hasa.

Usiwe mtu wa kufuatilia vitu vidogo vidogo au vitu vya kimbeya kimbeya na vitu vya kiudaku.

5. Wanazingatia kanuni za afya bora

Hili haliwezi kuachwa kwenye sifa za watu wanaoishi miaka mingi bali ni la mwisho kati ya vitu mhimu ili kuishi maisha marefu.

Kuna vitu vinajulikana wazi ni mhimu ili kuishi miaka mingi.

Vitu kama mazoezi ya viungo ya mara kwa mara hasa ya kutembea tembea kwa miguu ni mhimu kwa afya bora na maisha marefu.

Tafiti zinaonyesha watu wanaopenda kutembea tembea kwa miguu wanaishi miaka mingi kuliko wale wanaotumia gari au boda boda kila mara.

Watu wanaoishi kwa kula zaidi mboga za majani, matunda na wale wanaopenda kunywa maji mara kwa mara wanaishi miaka mingi zaidi.

Inasemekana pia mvinyo (wine) unao mchango wa kumuwezesha mtu kuishi miaka mingi hasa unapokunywa kwa kiasi.

Glasi moja au mbili ya wine kwa siku ukiwa na marafiki au ndugu unaweza kukusaidia kuishi miaka mingi.

Kama dini au dhehebu lako haviruhusu kunywa wine; usinywe. Mimi naandika kwa ajili ya watu wote, siandiki kwa ajili ya watu wa dini au dhehebu fulani peke yake.

Kwahiyo endelea kuwa mtu wa kupenda mazoezi ya viungo mara kwa mara, kula zaidi matunda na mboga za majani, kunywa maji ya kunywa bila kusubiri kiu na ukiweza kunywa glasi 1 au 2 za wine na utaishi maisha marefu.

Siri 5 za watu wanaofanikiwa kuishi miaka mingi Click To Tweet
(Visited 231 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175