Soda za energy na nguvu za kiume

Soda za energy na nguvu za kiume

Kwenye makala hii naangazia uhusiano uliopo kati ya soda za energy na nguvu za kiume.

Soda za energy au ‘energy drinks‘ ni aina mpya ya soda zilizojitokeza miaka ya hivi karibuni na zimetokewa kupendwa na watu wengi sana hasa vijana.

Mimi mwenyewe ni mnywaji wa soda hizo wa mara moja moja.

Mara moja moja nimekunywa azam energy, MO extra, jembe, red bull, na siku za hivi karibuni nimetokea kuipenda Azam malt coffee.

Karibu kila kampuni ya soda inayo pia soda fulani ya energy.

Sasa kumekuwa na maswali ya hapa na pale ikiwa kuna uhusiano wowote wa soda hizi na nguvu za kiume.

Kuna watu wanataka kujua ikiwa unywaji wa soda hizo unaweza kuwasaidia kuongeza nguvu za kiume au la.

Chanzo cha haya yote ni neno ‘energy‘ kwenye hizo soda.

Energy ni neno la Kiingereza lenye maana ya NGUVU kwa Kiswahili.

Kwa sababu hiyo kuna mtu atakuwa anawaza kwamba lazima zitakuwa na uhusiano fulani na nguvu za kiume!

Kwa haraka haraka naweza kusema ndiyo ni kweli soda hizo zinaweza kumsaidia mtu kuwa na msisimko na mwamko zaidi wa kimapenzi na nitaeleza hilo linatokeaje hasa.

Kwenye hizo soda kuna vitu vingi vinaongezwa lakini kitu kikubwa zaidi ndani yake ni kahawa (coffee).

Kahawa inapotumika kwa kiasi inao uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kwa namna moja au nyingine.

Kahawa ni moja ya vinywaji maarufu sana duniani na tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika zinahitimisha kahawa inaweza;

1. Kuongeza nguvu za mwili,

2. Kongeza uwezo wa kuwa makini zaidi,

3. Kuchangamsha mwili na

4. Kuongeza msukumo wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye uume.

5. Kahawa pia husaidia kuondoa sumu mwilini na sumu mwilini ni moja ya vitu vinavyoweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume.

Kahawa ni moja ya vyakula au vinywaji vinavyoongeza nguvu za kiume hasa ikitumika kwa kiasi.

Mwanaume anayekunywa kikombe kimoja au viwili vya kahawa kwa siku hawezi kusumbuliwa na tatizo la kukosa nguvu za kiume.

Siyo hivyo tu, bali baadhi ya tafiti zinasema kahawa inaweza pia kuongeza uwepo na ufanisi wa homoni ya testosterone ambayo ni homoni mhimu kwa afya ya mwanaume na nguvu za kiume kwa ujumla.

Mpaka hapo unaweza kuona kuwa ni kweli kuwa soda za energy zinaweza kuwa na msaada fulani kwa upande wa nguvu za kiume.

Na kama hiyo haitoshi kahawa inasemwa ina msaada pia kwenye afya ya moyo.

Tafiti zinasema unywaji wa kiasi wa kahawa una uhusiano wa karibu na afya nzuri ya moyo na hivyo kuwa msaada katika kuzuia magonjwa ya moyo na shambulio la moyo kwa wanaume na hivyo kuwaongezea afya nzuri ya kitandani.

Kahawa kama kiondoa sumu (antioxidant) husaidia kulinda mishipa ya damu na inaweza kuzuia madhara kwenye moyo ambayo yanaweza kuletwa na kolesto iliyozidi.

Kwahiyo kahawa iliyomo kwenye soda za energy inaweza kuwa ndiyo sababu ya soda hizo kuitwa energy drinks na ndiyo sababu unaweza kujihisi kuchangamka na mwenye nguvu zaidi baada ya kunywa soda hizo.

Kuna jamaa zangu fulani hao ndiyo walinishangaza sana kuna siku nimekuta wamechanganya soda ya energy na gongo kidogo na wanakunywa bila shida yoyote!

Nakushauri ndugu msomaji kamwe usichanganye soda za energy na gongo au na konyagi au spirit yoyote ni hatari sana kwa afya yako.

Pamoja na kuwa kahawa iliyomo kwenye soda za energy ina msaada fulani katika kuongeza nguvu ya mwili kwa ujumla bado siwezi kusema unywe au uzitumie kama dawa ya kutibu tatizo lako la nguvu za kiume.

Kuna uwezekano wa wewe kunywa soda nyingi zaidi na ukapata kaffeina (kahawa) nyingi zaidi ya inavyotakiwa.

Kumbuka ili kahawa iwe na faida mwilini lazima unywe kwa kiasi, lakini ukinywa kupita kiasi haya madhara yake ya upande wa pili yanaweza kukutokea;

1. Ukosefu wa usingizi. Usingizi ni kitu cha mhimu sana ili kuwa na nguvu za kiume

2. Kichwa kuuma

3. Mvurugiko wa tumbo

4. Uteja wa kahawa (depenance / addiction)

5. Kukosa utulivu (hamaki)

6. Maumivu ya mgongo

Sukari nyingi kwenye soda hizo za energy inaweza kukuletea;

6. Shinikizo la juu la damu

7. Uzito kupita kiasi

8. Kolesto

9. Ugonjwa wa moyo

10. Upungufu wa nguvu za kiume

Baadhi ya hizo soda za energy zimeandikwa kabisa kwamba hutakiwi kunywa zaidi ya mbili kwa siku, zingine zimeandikwa kabisa hazifai kwa mama mjamzito na hazishauriwi kutumiwa nyakati za jioni au muda mchache kabla ya kwenda kulala.

Soda za energy na nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Scroll to top
WhatsApp WhatsApp +255714800175