Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo

Kwa kawaida vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria aitwaye Helicobacter pylori au kwa kifupi H. pylori. Watu wawili katika kila watu watatu hapa duniani wana huyu bakteria tumboni mwao Click To Tweet

Na ingawa wengi wa watu hawa wenye huyu bakteria hawaonyeshi dalili yoyote ya kuumwa vidonda vya tumbo bado baadhi yao wanatokewa kuumwa.

Karibu asilimia 2 mpaka 20 ya watu wenye H. pylori wanaugua vidonda vya tumbo.

Ukiacha uwezo huo wa huyu bakteria H. pylori wa kusababisha vidonda vya tumbo, bakteria huyu huyu anahusika na ugonjwa mwingine mbaya wa saratani ya tumbo.

Ukweli ni kuwa bakteria huyu H. pylori hushambulia ulinzi asili unaolinda ukuta wa tumbo jambo ambalo ni mhimu sana na kutokea kwa saratani ya tumbo.

Soma hii pia > Dawa ya asili inayotibu saratani ya tezidume

H. pylori siyo sababu pekee ya kuugua saratani ya utumbo, sababu nyingine zinazoweza kuleta saratani ya tumbo ni pamoja na zifuatazo:

  • Umri. Watu wengi wenye saratani ya tumbo wana miaka 70 na kuendelea
  • Kuwa na maumivu ya tumbo yasiyoisha
  • Ukiwa ni mwanaume
  • Uvutaji sigara, tumbaku, bangi na vingine kama hivyo
  • Kurithi
  • Kula sana vyakula vilivyokaushwa kwa moshi na kuongezwa chumvi
  • Pombe
  • Vyakula na vinywaji vingi vya viwandani
  • Nyama choma
  • Sukari

Habari njema ni kuwa ukiwa na mazoea ya kula mara kwa mara vyakula vyenye beta-carotene na vitamini C, vyakula kama vile matunda na mboga za majani kunaweza kukupunguzia uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo.

Majani mabichi ya mti wa mlonge yana vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa. Unaweza kula ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako kutwa mara moja kwenye kachumbali au usage sambamba na juisi yoyote ya matunda.

Majani fresh ya mlonge

Saratani yoyote siyo hii ya tumbo tu, ni matokeo ya mwisho ya asidi kuzidi na kudumu mwilini kwa kipindi kirefu.

Tunatambuwa kwamba asidi inahusika pia na kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Zaidi ya nusu ya watu wote wenye vidonda vya tumbo vidonda vyao ni matokeo ya asidi kuzidi mwilini na siyo H. pylori  bakteria moja kwa moja.

Ukiacha mboga za majani, matunda na maji ya kunywa vyakula na vinywaji karibu vyote vina asidi.

Kinyume cha asidi ni alkalini. Asidi hujulikana pia kama tindikali.

Vyakula na vinywaji vingi ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo anakatazwa kula na kunywa vina asidi nyingi ndani yake.

Tafiti za hivi karibuni zinathibitisha kwamba vidonda vya tumbo vinao uwezo wa kukuletea saratani ya tumbo ikiwa hutachukuwa hatua ya kuvitibu kwa muda mrefu.

Vitu vyote viwili vinavyoleta vidonda vya tumbo yaani huyo bakteria na asidi vinahusika moja kwa moja na kutokea kwa saratani ya tumbo.

Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyojitokeza ndani ya mwili kwenye kuta za tumbo. Vidonda hivi vinaunda uwazi kwenye ukuta wa tumbo wakati ulinzi wa ukuta wa tumbo unapokuwa dhaifu kama matokeo ya bakteria au asidi kuzidi mwilini.

Huo uwazi unaojitengeneza (yaani kidonda) ndiyo njia ambayo bakteria H.Pylori anaitumia kuziingia kuta za tumbo na kuleta saratani.

Bakteria huyu anapoziingia kuta za tumbo kupitia hivyo vidonda anasababisha mabadiliko kwenye kinasaba (DNA) na kusababisha kudhurika kwa seli za tumbo

Kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanaopata maumivu ya tumbo, kujisikia vibaya au kutokewa na kutapika mara kwa mara wanashauriwa kuwahi mapema hospitali kwa ajili ya vipimo haraka iwezekanavyo.

Dalili hizi zinaweza kuwa ni dalili za saratani ya tumbo na siyo vidonda vya tumbo pekee.

Ukiona miguu inavimba, inawaka moto au inachomachoma kwenye nyayo ni dalili za wazi za mwili wako kuzidiwa na asidi au sumu. Matokeo ya mwisho kabisa ya dalili hizi ni saratani.

Ni ishara unatumia muda mwingi kukaa kwenye kiti hivyo damu inashuka chini kwenye miguu na kubaki huko bila kurudi juu ya mwili ili ibadilike na kusafishwa na ndiyo mwisho inakuletea asidi kisha miguu kuwaka moto na mwisho kabisa kama hutajitibia mapema ni saratani.

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyue wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5. Zoezi hili linaondoa asidi mwilini haraka kuliko zoezi lingine lolote

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Mwisho jipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

Asidi ni sumu au takataka zilizomo ndani ya mwili zinazoweza kukuletea magonjwa na maumivu mbalimbali mwilini ikiwemo miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo na maumivu yoyote mwilini ambayo hayajaletwa na ajali au jeraha nje ya mwili

Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaotibika na hata saratani ya tumbo ni ugonjwa unaotibika hasa katika hatua za mwanzo.

Kitakachokuletea saratani ya tumbo ni kitendo cha wewe kuwa na vidonda vya tumbo na ukaamua kuishi navyo. Ni kitendo cha wewe kuwa na vidonda vya tumbo na ukakubali viwe ni sehemu ya maisha yako ndiko kunakopelekea saratani ya tumbo.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 (nimesema niachie ujumbe WhatsApp, sijaandika nipigie simu).

Kama unapenda kujifunza mengi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza HAPA.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo Click To Tweet

Share post hii na watu wengine uwapendao.

Imesomwa mara 196

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy Ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam. Ni mwanachama wa Chama Cha Waganga wa Tiba za Asili Tanzania (CHAWATIATA) pia ni mwanachama wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO). Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Bonyeza HAPA tuchat WhatsApp