Ukweli na uzushi kuhusu homoni ya testosterone

Published by Fadhili Paulo on

Homoni ya testerone

Ukweli na uzushi kuhusu homoni ya testosterone

Kichocheo cha testosterone ni homoni ambayo hupatikana zaidi kwa upande wa mwanaume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanaume pia.

Kadri umri unavyoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testosterone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kawaida huanza baada ya miaka 30 kwa upande wa wanaume.

Ili kuhakikisha uzalishaji wa homoni ya testosterone unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D.

Ukweli na uzushi kuhusu homoni ya testerone

1. Uzushi : Kupungua au kushuka kwa kiasi cha homoni ya testosterone ni kisababishi kikuu cha kushuka kwa nguvu za kiume.

Ukweli : Siyo kweli kwamba homoni hii inahusika moja kwa moja na kupungua kwa hamasa ya tendo la ndoa kwa wanaume.

Bali msongo wa mawazo wa muda mrefu, matumizi yaliyozidi ya vilevi, punyeto au kujichua, kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo na magonjwa kama ya shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na kisukari ndiyo sababu kuu ya tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume wengi.

2. Uzushi : Kadri homoni ya testosterone inavyokuwa vizuri au inapozidi juu ya usawa wake mwilini mwanaume huishi miaka mingi.

Ukweli : Hakuna uthibitisho wowote na uhusiano wa moja kwa moja kwamba ukiongeza kiasi cha homoni hii unaweza kuishi miaka mingi zaidi.

3. Uzushi : Kisababishi kikuu cha nywele kupotea na upara kwa wanaume ni matokeo ya kushuka kwa homoni ya testosterone.

Ukweli : Upara au nywele kupotea kwa wanaume kwa sehemu kubwa ni jambo la kurithi.

4. Uzushi : Testosterone ni homoni ya kiume au ni homoni kwa ajili ya wanaume

Ukweli : Ingawa inahusika na mambo kadhaa juu ya afya ya mwanaume lakini homoni hii haipatikani kwa wanaume tu na wala siyo homoni ya kiume.

Testosterone inapatikana pia katika mwili wa mwanamke na ni moja ya homoni mhimu katika afya ya uzazi ya mwanamke.

5. Uzushi : Homoni ya Testosterone ikiwa juu inasababisha saratani ya tezi dume.

Ukweli : Kuna uhusiano mdogo kati ya testosterone na saratani ya tezi dume.

Hata hivyo tafiti zinasema ni wanaume wenye kiwango cha chini cha homoni hii ndiyo wanaopatwa na saratani ya tezi dume kirahisi na si kinyume chake.

6. Uzushi : Ukiwa na kiwango cha juu cha homoni ya testosterone kitakusaidia kuwa mwanariadha bora

Ukweli : Ingawa homoni hii inahusika na mambo kama ya misuli na mishipa lakini bado haina uhusiano wa moja kwa moja na uwezo wa kukuongezea mbio na kuwa mwanariadha bora na bingwa.

Kuna mengine mengi nyuma ya pazia yanayoweza kukufanya kuwa mwanariadha bingwa na si testosterone peke yake kama baadhi ya watu wanavyodai.

7. Uzushi : Virutubishi vya Testosterone vinaweza kukuongezea wingi wa mbegu (sperm count)

Ukweli : Kwa haraka haraka hii inaweza kukuletea maana na ukahisi ni kweli kwa sababu unafikiri kwamba kadri homoni zinavyokuwa juu au zinavyokuwa sawa basi na mbegu zako nazo zitakuwa nyingi na sawa.

Hata hivyo ukweli wake ni kuwa virutubishi vya testosterone vinavyokuahidi kukuongezea wingi wa mbegu zako vinakuongopea na badala yake vinaweza kukuletea zaidi tatizo la kuwa na mbegu chache.

Wakati homoni kuu ya pituitari inapohisi kuongezeka kulikozidi kwa testosterone mwilini huzuia uzalishwaji wa homoni inayohusika na uzalishaji wa mbegu zaidi iitwayo ‘luteinizing hormone‘.

Kwa leo haya yanatosha kwanza siku nyingine nikipata muda zaidi nitaleta ufafanuzi zaidi na kuongeza uzushi mwingine zaidi.

Ukipata muda soma na hii post ifuatayo;

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Share post hii na wengine uwapendao;

Ukweli na uzushi kuhusu homoni ya testerone Click To Tweet

Ikiwa una tatizo lolote kuhusiana na mbegu zako labda zimekuwa chache, hazina afya na uwezo wa kutungisha mimba nk tuwasiliane WhatsApp +255714800175

(Visited 483 times, 1 visits today)

1 Comment

Ezekiel Mbise · 01/12/2021 at 6:49 pm

Homoni kushuka

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175