Ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu 1

Ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu

ULAJI WA CHIPS umetajwa kuwa HATARI kwa afya ya Binadamu.

ULAJI WA CHIPS umetajwa kuwa HATARI kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa FIGO, MOYO , SHINIKIZO LA DAMU,KISUKARI NA SARATANI za aina zote.

SAHANI moja ya CHIPS kavu huwa na MAFUTA yanayokaribia NUSU kikombe cha CHAI ambayo ni sawa na ujazo wa mililita 250.

Kwahiyo WALAJI wengi wa CHIPS wapo katika HATARI ya kutengeneza SUMU kwenye MIILI yao bila kujua.

UTAFITI unaonyesha WATU wengi hupendelea KULA chips mayai, kuku, soseji au hata kwa mishikaki maana yake ni kwamba KIWANGO hicho cha MAFUTA huzidi kwa sababu na vyenyewe huwa VIMEKAANGWA.

JAMBO la KUSIKITISHA ni kwamba WAFANYABIASHARA wengi wamekuwa hawazingatii UMUHIMU wa kutumia MAFUTA mara moja katika kukaanga VITU hivyo.

WENGI huwa wanapikia MAFUTA kwa zaidi ya mara mbili na hivyo kuzidisha HATARI zaidi.

“Wanazidisha HATARI kwa sababu… kawaida MAFUTA yanapaswa KUPIKIWA mara moja. Kadri unavyounguza MAFUTA ndivyo ambavyo ule MFUMO wa MAFUTA MASAFI ambayo yanatakiwa kwa MWILI wa MWANADAMU unabadilika na kuwa MACHAFU, maana yake ni kwamba unapopikia MAFUTA zaidi ya mara mbili tayari yanakuwa yametengeneza SUMU ambayo haitakiwi MWILINI ,”

MAFUTA ambayo yametumika kukaangia VYAKULA zaidi ya mara mbili hubadilika na kutengeneza UTANDO MWEUPE ambao huweza kuonekana iwapo MTU atayatazama kwa MACHO yake.

Ule UTANDO MWEUPE utakaouona unatoa ISHARA kwamba MAFUTA hayo HAYAFAI kwa MATUMIZI ya BINADAMU, lakini WATU wanataka kufanya BIASHARA hivyo huendelea KUYATUMIA bila KUJALI au pengine KUTOKUJUA kwamba wanaziweka AFYA za WALAJI katika HATARI ya kupata MAGONJWA .”

PAMOJA na KIWANGO hicho cha MAFUTA ambacho huingia MWILINI kwa ULAJI wa SAHANI moja pekee ya CHIPSI kavu, MLAJI hula CHUMVI nyingi iliyopo ndani ya NYANYA maalumu iliyosagwa (tomato).

TOMATO SAUCE jinsi ilivyotengenezwa ina CHUMVI nyingi, sasa umekula MAFUTA mengi jumlisha na hiyo CHUMVI nyingi na ninavyofahamu WALAJI wengi wa CHIPSI hupendelea KUSHUSHIA na KINYWAJI chenye SUKARI nyingi maana yake unakuwa umetengeneza SUMU ndani ya MWILI wako.

TAKWIMU zinaonesha kuwa idadi ya WAGONJWA wanaougua MAGONJWA yasiyokuwa ya KUAMBUKIZA nchini inaongezeka.

HATARI hii inaweza KUEPUKWA iwapo WATU watazingatia ULAJI unaofaa.

Ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu 2

WENGI hatuzingatii ULAJI wa CHAKULA BORA, tunakula mradi tule na hatuzingatii kupima AFYA zetu.

Wakati UMEFIKA tunapaswa TUBADILIKE kwa sababu WAGONJWA wanaongezeka.

UTAFITI unaonyesha KATI ya WATU 100 wenye UMRI wa kati ya MIAKA 25 na kuendelea, 9 kati yao tayari wanaugua UGONJWA wa KISUKARI huku WAWILI wakiwa hawajijui kuwa wana MARADHI hayo.

Kila MWAKA duniani WATU milioni 12 HUGUNDULIKA kuwa wana SARATANI , na ASILIMIA 60% ya MAGONJWA ya SARATANI yanasababishwa na MFUMO MBOVU wa MAISHA hasa ULAJI usiofaa.

Wenzetu WAZUNGU ni wajanja sio kwamba hawali CHIPS, wanakula lakini WANAZINGATIA ‘menu’ ya SAHANI wanayokula kwamba inakuwa na VIAZI kidogo, MBOGAMBOGA nyingi na MATUNDA.

SISI kwetu ni KINYUME Kabisa.

WATU wanapenda TOMATO sauce kwa wingi.

ULAJI wa MBOGAMBOGA ni jambo la MSINGI kwani huenda kusaidia kurahisisha MFUMO wa umeng’enywaji wa CHAKULA tumboni.

Kama unapenda chipsi basi usile kila siku na ikiwezekana upike mwenyewe nyumbani na mafuta yanayotumika kupikia yatumike mara moja tu vile vile unaweza kujiandalia kachumbali au hata pili pili au tomato sauce wewe mwenyewe nyumbani.

AFYA BORA KWA MAISHA MAREFU !!

Soma hii pia 👇

Kukaa muda mrefu kwenye kiti husababisha kufa mapema

Unataka kujuwa ikiwa una uzito sawa au uliozidi?

Tumia kikokotoo cha BMI (BMI calculator) hiki hapa chini.

Bonyeza Nataka Kupima Uzito kisha andika urefu wako katika sentimita na uzito katika kilogramu kisha bonyeza KOKOTOA itakuambia kama una uzito sawa au umezidi au una uzito pungufu.

Pima uzito hapa

require
require require

Your BMI is......

BMIClassification
less than 18.5:Underweight
18.5 - 24.9:Normal weight
25 - 29.9:Overweight
30 - 34.9:Class I Obese
35 - 39.9:Class II Obese
40 upwards:Class III Obese

.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu Click To Tweet
Fadhili Paulo
Imesomwa mara 166

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *