Usifanye mambo haya 9 muda mchache kabla ya tendo la ndoa

Published by Fadhili Paulo on

Usifanye mambo haya 9 muda mchache kabla ya tendo la ndoa

Tendo la ndoa ni moja ya jambo la starehe na lenye uwezo wa kukupa furaha kuliko kitu kingine chochote na mara nyingi halihitaji gharama yoyote.

Ni moja ya tendo la watu wawili wa jinsia tofauti lenye uwezo wa kuunda taifa.

Ni tendo lenye uwezo wa kuunganisha familia mbili tofauti kuwa ndugu.

Ni jambo takatifu na ndiyo maana ni tendo kwa ajili ya wanandoa wenye baraka zote za kidini na kiserikali na siyo kwa kila mtu tu.

Pamoja na hayo yote ni tendo linapatikana kwa matajiri na kwa maskini, kwa watakatifu na kwa wenye dhambi.

Ili lifanyike vizuri lazima mazingira fulani yawezeshwe kwanza kuanzia akili na mwili wako kwa ujumla.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili na ni MTanzania.

WhatsApp napatikana kwa namba +255714800175

Endelea kusoma…

Hapa nimekuandikia mambo 9 ambayo hutakiwi kufanya muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Muda mchache kama muda gani?

Kuna msomaji mmoja anauliza.

Muda mchache hapa namaanisha masaa matatu au mawili kabla ya kuingia uwanjani.

1. Usile chakula kingi

Kula chakula kingi muda mchache kabla ya tendo la ndoa kutakufanya ujisikie mchovu sana na mwenye usingizi hasa kama chakula ulichokula kina wanga mwingi kama ulivyo wali.

Matokeo yake hutakuwa na hamasa na nguvu za kutosha kushiriki tendo hilo.

Badala yake unaweza kula kidogo vyakula vya mbegu mbegu (nuts) kama vile karanga, korosho, mbegu za maboga, mbegu za tikiti maji, matunda kidogo na maji kidogo, hivi vyote vitakufanya ujisikie mpya, mwenye nguvu na afya.

2. Usinywe soda za energy

Miaka ya karibuni kumejitokeza aina mpya ya soda zinaitwa energy.

Energy ni neno la kiingereza lenye maana ya NGUVU kwa Kiswahili.

Kwa sababu unahitaji nguvu na unaona hizo soda zinaweza kukuongezea nguvu basi unaweza kushawishika kunywa kabla ya tendo la ndoa!

Hata hivyo soda hizo huongezwa pia sukari ndani yake ambayo huweza kukupa nguvu ya muda mfupi tu na baadaye hali huwa mbaya mara mbili zaidi ya kabla.

3. Usigombane na mwenza wako

Mapenzi huwa raha sana mwanzoni yakiwa bado mapya.

Miaka kadhaa baadaye wapenzi huanza kuzoeana na kuanza kuchukuliana poa.

Hali hiyo ya kuzoeana na mwenza wako inaweza kukuletea mazoea mabaya na ukaanza kuzozana au kugombana na mwenza wako muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Hali hiyo hupunguza hamasa na hamu kwa mwenzio na hivyo kumfanya kuwa na ushirikiano mdogo mkiwa uwanjani.

Hili napendekeza liwe sehemu ya maisha yenu na siyo uzingatie kabla tu mnapokaribia kuanza mechi ndiyo unakuwa mpole, hapana, jizoeshe kuwa mtu wa amani muda mwingi na siyo ugomvi, kelele, gubu kwa mwenzio kila mara.

Sijasema msigombane kabisa milele yote, hapana, nyie siyo mawe, ni binadamu, hivyo mara moja moja kugombana siyo jambo baya.

Kama hamgombani kabisa maana yake kuna kitu siyo sawa kwenu wote au kwa mmoja kati yenu, huenda mmoja kati yenu ameshakufa tayari bila kujua.

Unapopenda kumbuka pia kutumia ubongo siyo moyo peke yake.

4. Usiwe na mawazo mawazo yoyote (stress)

Mawazo mawazo yanaweza kuwa janga ukiwa nayo muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Huhitaji kuhofu ikiwa utafanya kazi ya kupongezwa au ndiyo utaishia kudharauliwa.

Unahitaji kuwa na utulivu sana akilini kwako muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Weka simu mbali, weka computer mbali, ondoa vitu vinavyoweza kukuondolea utulivu kirahisi.

Uwe ulikuwa huna uchovu na ulipata wasaa wa kupumzika japo masaa mawili kabla.

Kama mnaweza ni vema kila mmoja wenu akaweka simu mbali ikiwezekana zimeni kabisa simu.

Siyo mtu yupo kitandani anawaza mambo yake ya kazini au bado anaendelea kufanya kazi kwa njia ya mtandao akiwasiliana na wengine.

Even digital people are still people, hata watu wa kwenye mtandao bado ni watu.

Kuna mtu sababu hayupo ofisini nyakati hizo na anachat na watu kwenye mtandao huwa anadhani hiyo siyo kazi na haiwezi kumchosha mwili wake.

Pata muda wa kutosha wa kupumzika na kutulia muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Ukiweza mwambie mwenza wako akufanyie masaji.

5. Usiwaze mengi kuhusu mwili wako

Usiwaze kwamba labda mpenzi ataniona nina tumbo kubwa.

Kasoro yoyote kwenye mwili wako unayoiona wewe kama ni kasoro mara nyingi huwa ni mawazo yako tu binafsi na pengine mpenzi wako hana hata wazo hilo.

Unaweza kuwaza namna utakavyojiboresha afya na muonekano wako pole pole lakini lisiwe jambo la kuliwaza muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Tendo la ndoa ni jumla ya vitu vingi na siyo lazima mfanye tendo lolote ndiyo uone umeshiriki. Hata kubaki wawili tu chumbani kwenye viti mkipiga stori na kucheka bado hili nalo ni tendo la ndoa.

Ondoa hiyo hali ya kutaka uonekane mkamilifu kwenye mwili wako.

Jikubali vile ulivyo na usisikilize sana kila wanachokukosoa watu kuhusu mwili wako.

Kwa wanaume mara nyingi huwaza labda ataniona nina kibamia, labda ataniona ni mnene sana hivyo sitamfikisha na mengine kama hayo.

Muda mchache kabla ya tendo la ndoa ondoa mawazo hayo mgando na ujikubali vyovyote ulivyo.

6. Usiwe na matarajio makubwa sana

Hili hasa mara nyingi huwa shida kwa mtu anayeshiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza au unapokutana na mpenzi mpya.

Mara nyingi unakuwa na hamaki kwamba lazima ushiriki kwa namna ile na kiwango kile au na mpenzi wako anatakiwa awe hivi au aitike vile.

HAPANA.

Ondoa hayo matarajio makubwa uliyonayo na ukubali matokeo yoyote ya siku hiyo.

Kama juzi ulifanikiwa kurudia mara 3 basi hujaambiwa lazima iwe hivyo kila mara unaposhiriki tendo la ndoa na wala hiyo siyo fomula, hiyo siyo lazima na wala hiyo siyo ishara wewe ni mwanaume sana.

Relax na uwe tayari kwa matokeo yoyote.

Ni tendo la kawaida tu na siyo mafunzo ya kuwa fundi wa kutengeneza ndege.

7. Usifanye punyeto sana

Kuna baadhi ya wanaume ili kuepuka hali ya kuwahi sana kufika kileleni huamua kujichua muda mchache kabla ya mechi.

Kwa namna moja au nyingine hali hiyo inaweza kuwa msaada hasa kama wewe ni mtu unayekaa miezi au wiki kadhaa bila kushiriki tendo la ndoa.

Wanasema bao la kwanza huwa na kiherehere sana hivyo wapo wanaoona bora kulitoa kabisa mapema.

Sasa usije ukakosea ukapiga sana punyeto kabla, mara moja tu inatosha, ila kama utafanya mara mbili au tatu unaweza kuleta uchovu usiohitajika na ukashindwa kushinda mechi yenyewe kamili.

Kama unatumia mbinu hii basi fanya mara moja moja na siyo kila siku au mara nyingi kwa wakati mmoja muda mchache kabla ya tendo la ndoa.

Usisahau pia punyeto ina madhara mabaya kimwili na kiakili kama hutakuwa makini.

8. Usiwe mtu wa kukariri

Mapenzi yanahitaji ubunifu.

Jaribu vitu vipya.

Usiwe na muda maalumu wa kushiriki tendo la ndoa.

Mwingine amezoea ni mpaka wale, waoge, waingie kitandani ndiyo wapigane!

Siku nyingine unaweza kuanza na tendo la ndoa Kisha kula, halafu kuoga na mwisho kulala.

Usiwe na ratiba fulani maalumu.

Siyo lazima mfanye chumbani kila siku, siku nyingine fanyeni hata jikoni au hata kwenye gari.

Nendeni hata hotelini au guest house siku za weekend, siyo lazima iwe nyumbani tu tena chumbani kila siku.

Jaribu mitindo (style) mingine, fanya kitu fulani kipya kila mara.

9. Usilewe sana muda mchache kabla ya tendo

Ingawa pombe inaweza kukuamsha na pengine hata kukuongezea nguvu kidogo, bado unashauriwa kutokunywa sana au kulewa sana muda mchache kabla ya mechi.

Hapa ni kwa vilevi vyote ikiwa ni pamoja na sigara.

Sigara zinaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kwenye uume na kukupelekea kuwa na nguvu chache uwanjani.

Sasa sijasema usitumie kabisa kilevi chochote, kama hela unayo na siyo ya mawazo, glasi moja ya wine kwako na kwa mpenzi wako siyo jambo baya.

Mhimu kuwa na kiasi na kutokudhuru afya yako.


0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175