Usile vyakula hivi kama unaumwa Bawasiri

Published by Fadhili Paulo on

Usile vyakula hivi kama unaumwa Bawasiri

Usile vyakula hivi kama unaumwa Bawasiri

Wagonjwa wengi ninaokutana nao wakitafuta dawa ya bawasiri baadhi yao wamekuwa wakisema nahitaji dawa kwa ajili ya rafiki au ndugu yangu fulani na siyo kujisema wao moja kwa moja kwamba ndiyo wanaoumwa!

Uwe na amani haijalishi ni bawasiri au U.T.I au vidonda vya tumbo au nguvu za kiume, chochote utakachowasiliana na mimi kinabaki kuwa siri baina yangu na wewe tu na hiyo ni moja ya sheria na kanuni mhimu sana katika kazi nifanyayo. Hivyo uwe na amani.

Bawasiri au Kikundu au Puru ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa. Kwa Kiingereza hujulikana kama Hemorrhoid au Piles.

Katika hatua yake ya kuonekana wazi ugonjwa hujitokeza kama uvimbe au vivimbe kadhaa kwenye maeneo ya tundu la haja kubwa.

Karibu katika kila watu wanne watu watatu kati yao wanasumbuliwa na ugonjwa huu. Ni ugonjwa wa pili kati ya magonjwa yanayosumbuwa watu wengi zaidi duniani baada ya U.T.I

Tatizo la bawasiri linaonekana kuwawapata kirahisi zaidi wanawake kuliko wanaume.

 Unapoumwa bawasiri unapaswa kuwa makini sana juu ya chakula unachokula na vinywaji unavyokunywa kila siku kwani vinao uwezo wa kurahisisha au kukwamisha matibabu kwako.

Siri iliyopo katika kupunguza au kuitibu bawasiri ipo kwenye vyakula hasa vyakula ambavyo vinaweza kukusaidia usipate choo kigumu au ukose kabisa choo. Siri ipo hapo.

Kwa sababu hiyo leo nimechukuwa muda wangu kama masaa manne hivi nikikuandalia maelezo haya juu ya vyakula na vinywaji ambavyo itakulazimu uvikwepe ili kufanya bawasiri yako iweze kupona kwa haraka na kwa urahisi zaidi.

Mhimu vyakula hivi usivitumie kabisa wakati wote ukiumwa na miezi kadhaa baada ya kupona kabisa bawasiri.

Ni kwa kuzingatia maagizo kama haya unakuwa unajiwekea nafasi nzuri zaidi ya kupona kuliko kutegemea dawa pekee ndiyo ikuletee miujiza.

Epuka vyakula vifuatavyo kama unaumwa bawasiri:

1. Vyakula vya kusisimua (Spicy foods): 

IKama umekuwa ukisumbuliwa na bawasiri na kufunga choo au umekuwa ukipata choo kigumu kwa kipindi kirefu kuna uwezekano mkubwa umekuwa ukila vyakula vyenye kusisimuwa.

Kama una bawasiri vyakula vya kusisimuwa ni adui mkubwa kwako na unatakiwa uviache haraka ili kunusuru afya yako na uweze kupata kupona bawasiri.

Vyakula vya kusisimua ni pamoja na ketchup, chill sauce, tomato sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii.

Mwili wako utakushukuru sana kwa uamuzi huu wa kusitisha kutumia vyakula hivi.

2. Baadhi ya bidhaa zitokanazo na maziwa: 

Kama una bawasiri huna tofauti sana na mtu mwenye vidonda vya tumbo na mara nyingi vitu hufuatana au huwa pamoja.

Kama ilivyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwamba hatakiwi kupendelea kunywa maziwa fresh basi hata wewe mwenye bawasiri usinywe maziwa fresh na jibini (cheese).

Maziwa na jibini vinaweza kukuongezea aside tumboni mwako na kuleta shida au usumbufu zaidi kama una bawasiri. Unaweza kutumia vyakula hivi pengine mara moja tu kwa wiki na siyo kila siku.

3. Nyama nyekundu: 

Ukiacha vyakula vya kusisimua kitu kingine kinachoweza kuongeza maumivu zaidi au kuchelewesha kupona kwa bawasiri ni ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu.

Ukiwa na bawasiri maana yake mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula haupo sawa na haufanyi kazi kwa kiwango chake kama unavyotakiwa.

Na moja ya vyakula vyenye shida kwenye kumeng’enywa tumboni ni nyama nyekundu yaani nyama ya ng’ombe na nyama ya mbuzi.

Kama unahitaji sana kula nyama napendekeza ule mara 1 tu kwa wiki na uepuke kwa gharama nyama choma na mishikaki. Unaweza kula samaki au nyama ya kuku wa kienyeji mara kwa mara.

Ukiona unakosa choo au unapata choo kigumu mara kwa mara badili mlo wako kwa siku kadhaa na ule mboga za majani, matunda na maji tu.

4. Pombe: 

Siyo jambo baya kupata bia moja au glasi mbili za mvinyo mwekundu mara moja moja au siku za wikendi.

Hata hivyo kama wewe ni wale ambao haiwezi kupita siku bila kunywa pombe basi itakuwa vigumu kwako kupona bawasiri.

Pombe ina kawaida ya kukausha maji mwilini na mgonjwa wa bawasiri unahitaji sana maji mwilini mwako kuliko kitu kingine chochote.

Maji yanapopungua mwilini ni kukosa choo au kupata choo kigumu na matokeo yake ni kuongezeka zaidi na zaidi kwa ugonjwa badala ya kupona.

5. Vyakula vya viwandani na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi: 

Watu wengi wanaofanya kazi maofisini wanalazimika kula migahawani au kwenye maduka na vingi ya vyakula hivyo huwa si salama kwa mtu mwenye bawasiri.

Unahitaji kula vyakula vya asili zaidi unapougua bawasiri na utatakiwa uachane kabisa na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chips, maaandazi na vingine vyote vinavyopikwa kwa staili hii ya kuwa katikati ya mafuta mengi.

6. Kaffeina: 

Habari mbaya kwa wale wenzangu wapenda kahawa na chokoleti!

Kaffeina inajulikana kwa kusababisha maumivu na upungufu wa maji mwilini.

Kama una bawasiri nakushauri uache vitu hivi haraka navyo ni chai ya rangi, kahawa, chokoleti, energy soda zote, soda zote nyeusi na kinywaji kingine chochote kilichoandikwa kina kaffeina ndani yake.

Kama ni chai jaribu chai ya mchaichai na utumie asali badala ya sukari mara zote.

Unapoumwa au uanzapo tu kuona dalili za bawasiri ndiyo wakati muafaka wa kutafuta dawa na matibabu. Usisubiri mpaka tatizo liwe sugu au kubwa ndiyo uanze kutafuta dawa kwani hiyo itakupelekea na kupona kwako nako kuchukuwe muda mrefu zaidi.

Kwahiyo kama kuna rafiki yako au ndugu yako au wewe mwenyewe unaumwa bawasiri jaribu kuzingatia maelezo haya niliyotoa hapa na iwapo utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri iwe ya ndani au ya nje niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Ofisi yangu inaitwa *Tumaini Herbal Life* ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam 

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine.

(Visited 1,250 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175