Uvutaji bangi unaweza kukuletea saratani ya tezi dume

Published by Fadhili Paulo on

Uvutaji bangi unaweza kukuletea saratani ya tezi dume

Mtanisamehe kidogo ndugu wajumbe kwa leo sitawaonea aibu.

Baadhi ya tafiti zimeweza kuthibitisha juu ya uwepo wa uhusiano baina ya bangi na saratani ya tezi dume.

Zaidi ya tafiti 25 zilizofanywa ndani ya miaka 40 iliyopita zimeendelea kuona uhusiano wa uvutaji bangi na kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume.

Wakati uvutaji wa sigara unahusishwa na saratani ya mapafu, uvutaji wa bangi unahusishwa na kuleta saratani ya tezi dume.

Na kuna baadhi ya takwimu katika baadhi ya nchi zinaweza kuhitimisha juu ya hili.

Ukipata muda soma na hii 👇

Tendo la ndoa hupunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume

Saratani ya tezi dume inawapata wanaume wengi kuanzia miaka 40 kwenda juu.

Kwa kawaida saratani yoyote huwa haitokei tu haraka haraka mwilini.

Mpaka unaona dalili au kuumwa basi ujuwe tayari umekuwa nayo au imekuwa ikijiunda mwilini mwako kwa miaka kadhaa nyuma.

Watu wengi huanza kuvuta bangi wanapokuwa na miaka kuanzia 20 na kuendelea, wapo wanaoanza kabla ya hapo lakini wengi ni baada ya miaka 20, wengine kwenye miaka 25 hadi 27 hapo.

Idadi ya watu wanaopatwa na saratani mbali mbali imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Kati ya saratani 100 zilizopo, saratani ya tezi dume ni miongoni mwa saratani 4 ambazo wagonjwa wake wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ndani ya miongo minne iliyopita.

Ndani ya miaka 50 iliyopita mataifa mbalimbali yamekuwa yakiondoa zuio la kuvuta bangi katika nchi zao.

Nchi kadhaa duniani tayari zimeruhusu matumizi ya bangi na kuiondoa kwenye kundi la madawa makali ya kulevya

Karibu katika majimbo 40 ndani ya Marekani unaweza kuvuta bangi bila shida wala wasiwasi wowote wa polisi wala sheria.

Nchi hizo zinasema madhara ya bangi kwa ujumla siyo makubwa kiasi hicho kama watu wengi wamekuwa wakiamini kwa miaka mingi na hivyo hakuna sababu ya kuizuia sana na kwamba ni bora itumike bila kificho na kodi ya serikali ipatikane.

Hata hapa Tanzania wapo baadhi ya wabunge wamekuwa wakipendekeza bangi iruhusiwe ili serikali ipate kodi au ilimwe kwa ajili ya kuuzwa kibiashara nchi za nje.

Baada ya pombe, bangi ndicho kilevi kinachotumika na watu wengi sana hasa vijana na watu wazima popote duniani.

Kwa hiyo ukitazama takwimu hizo utaona wazi kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya uvutaji wa bangi na saratani ya tezi dume.

Ndiyo, bangi inaweza kuwa na faida mbili au tatu za kiafya lakini ubaya wake unaweza kuwa hatari zaidi kwa afya kuliko faida zake.

Kuvuta bangi bado ni kosa kwa sheria za Tanzania lakini nchi kama Marekani, Canada, Uholanzi, Jamaica, Uruguai, Afrika Kusini, Costa Rica, Zimbabwe, Colombia, Lesotho, Zambia, Morocco na Hispania bangi imeruhusiwa.

Rwanda wameruhusu ilimwe kwa ajili ya biashara na iuzwe nje.

Mpaka mwishoni mwa 2019 Afrika ilikuwa inaingiza karibu dola bilioni 37.3 kwa zao la bangi na kuchukuwa asilimia 11 ya mapato ya bangi kidunia.

Kama unatafuta vitu vya kuviepuka ili kujilinda na kujikinga na saratani ya tezi dume unashauriwa kukaa mbali na bangi.

Kama unahitaji dawa nzuri ya asili kwa ajili ya saratani ya tezi dume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175. Maelezo yake zaidi unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Share na wengine uwapendao.


0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175