Vitu 10 vinavyoweza kusababisha upate watoto mapacha

Published by Fadhili Paulo on

jinsi ya kupata watoto mapacha

Vitu 10 vinavyoweza kusababisha upate watoto mapacha

Tafiti zinaonyesha kwamba uwezekano wa mwanamke mmoja kubeba mimba ya mapacha ni aslimia 3 na kuna njia mbalimbali zinaweza kuongeza uwezekano huu mpaka asilimia tano au kumi na tutaziona hapo chini.

Kwenye ulimwengu huu wa maisha magumu wanawake wengi hupenda kuzaa mapacha mara moja tu wa jinsia tofauti au jinsia moja na kufunga kizazi.

Japokuwa watoto mapacha wanapendeza sana na kufurahisha nyumba sio wanawake wote wanapenda watoto mapacha na mapacha hubeba hatari kubwa kipindi cha ujauzito kwani sio rahisi kuwazaa kwa njia ya kawaida huku wakiongeza dalili za ujauzito kua kali zaidi kama kutapika sana, kuchoka sana nk.

Watoto mapacha wanatokea vipi kwenye kizazi?

Kuna aina mbili za watoto mapacha.

a) Mapacha wa kufanana au identical twins

Hawa ni mapacha ambao hutokea pale yai moja la mwanamke lililorutubishwa na na mbegu ya mwanaume linapogawanyika na kutengeneza watoto wawili.

Watoto hawa hufanana kwa kila kitu yaani sura, tabia mpaka jinsia na hua ni vigumu sana kuwatofautisha kwa macho.

b) Mapacha wasiofanana au non identical twins

Mapacha hawa hutokea pale mayai mawili ya mama yanavyorutubishwa na kujishikiza tofauti kwenye mfuko wa uzazi.

Mapacha hawa hua wako tofauti kwa sura, jinsia na hata tabia.

Hawa ni kama ndugu waliofuatana tu.

je unawezaje kupata watoto mapacha?

Kusema ukweli hakuna njia ya moja kwa moja inayojulikana wazi ya kupata watoto mapacha.

Hata hivyo kuna baadhi ya sababu zinaongeza nafasi kubwa ya kubeba mimba ya watoto mapacha na tafiti nyingi zimeonyesha kwamba matumizi ya njia hizo yanaongeza nafasi kubwa sana ya kubeba watoto mapacha.

Watoto mapacha wapatao milioni 1.6 wanazaliwa kila mwaka duniani kote, katika watoto 100 wanaozaliwa kuna mapacha 6 kati yake.

Kuchelewa kuzaa na teknolojia za kitabibu kama vile IVF zimeongeza idadi ya mapacha kuzaliwa kwa asilimia mpaka 70 tangu miaka ya 1980.

Vitu 10 vinavyoweza kusababisha upate watoto mapacha

1: Kutumia dawa za kupata ujauzito

Kuna dawa ambazo hutumiwa na wanawake ambao wanashindwa kubeba mimba, dawa hizi hufanya yai zaidi ya moja kuachiwa kutoka kwenye mirija ya uzazi na hii huongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mapacha, na wanawake wanaotumia dawa hizi hujikuta wanabeba mapacha.

2. Umri

Mwanamke mwenye umri wa miaka 30 na kuendelea ana uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito wa mapacha.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba homoni ijulikanayo kama Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ huongezeka mwilini mwa mwanamke kadri anavyozidi kuwa na umri mkubwa.

Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ ndiyo inahusika na ukuaji na afya ya mayai kwenye mirija ya mayai ya uzazi kabla hayo mayai hayajatolewa tayari kwa kurutubishwa.

Kadri umri unavyoongezeka ndivyo na homoni hii inavyohitajika kwa wingi sabbau mayai ya uzazi yanakuwa yanahitaji kusiisimuliwa zaidi ili yaweze kukua kuliko kwa wasichana wadogo.

Hili linaweza lisieleweke kirahisi kwa sababu kwa kawaida Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ huwa inaongezeka kwa mwanamke anayekuwa hana uwezo wa kupata ujauzito kirahisi na ana dalili za kuwa mgumba

Hata hivyo kuna nyakati vijishimoyai (follicles) vinapigana na kuongezeka kwa Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na matokeo mayai mawili au zaidi hutolewa na hivyo mimba ya mapacha inatungwa

3. Historia

Ikiwa kwenye familia yenu kuna historia ya kuwepo watoto mapacha basi kuna uwezekano na wewe ukapata.

Kama mama yako mzazi amewahi kupata mapacha kuna uwezekano na wewe ukapata mapacha

Kama mama yako au hata baba yako wote wawili kwenye familia zao kumewahi kutokea mapacha basi na wewe unaweza kupata mapacha

Hili siyo la lazima lakini kuna asilimia fulani ya ukweli japo siyo kwa asilimia mia moja

4. Uzito

Mwanamke mwenye uzito mkubwa anao uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito wa watoto mapacha kuliko mwanamke mwembamba na mwenye uzito mdogo

Mafuta yanapozidi kidogo mwilini yanapelekea kuongezeka kwa usawa wa homoni iitwayo estrogen. Homoni hii inapoongezeka inasababisha msisimko uliozidi kwenye mirija ya mayai.

Kwahiyo badala ya yai moja kutolewa, msisimko unapoongezeka ndani ya mirija ya mayai basi kunaweza kutolewa mayai mawili au zaidi ili kutungishwa mimba na mapacha wanatokea

Hapa napo pana miujiza ya Mungu kwa sababu kwa baadhi ya wanawake uzito mkubwa unaweza kuwa ndiyo chanzo cha wao kutopata ujauzito na hata kuwa wagumba

5. Urefu wa mwanamke

Wanawake warefu zaidi kuliko kawaida wana uwezekano mkubwa wa kupata mimba ya mapacha kuliko wanawake wafupi kwa kimo.

ukiwa na urefu wa futi 5 kwenda juu kama mwanamke unayo bahati ya kuweza kupata watoto mapacha.

Hili halina ufafanuzi wa kueleweka kisayansi kwanini linatokea hata hivyo wanasayansi wanahisi kwamba mwanamke anapokuwa mrefu basi kuna uwezekano mkubwa akawa na afya nzuri na viinilishe vya kutosha mwilini mwake na hivyo kupelekea kupata mimba ya mapacha

6. Aina ya chakula

Jamii ambazo chakula chao kikuu ni viazi vikuu, zimeonyesha kua na mapacha wengi kuliko jamii zingine, tafiti zinasema kwamba viazi hivyo vina kiasi kikubwa sana cha homoni za oestrogen ambazo zinasababisha mama kutoa mayai mengi kitaalamu hujulikana kama ‘hyperovulation’.

7. Kupata ujauzito ukiwa bado unanyonyesha

Kuendelea kunyonyesha mtoto wako kwa muda mrefu; kuna homoni moja inaitwa prolactin ambayo inahusika na kutoa maziwa kipindi mama ananyonyesha, sasa kuendelea kuwepo kwa homoni hii kwa kiasi kikubwa wakati mama ameanza kushiriki tendo la ndoa kuna muongezea nafasi kubwa ya kupata mapacha akibeba mimba.

8. Matumizi ya folic acid

Dawa za folic acid hutumika na wajawazito wote ili kuzuia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile hasa kwenye mishipa ya fahamu, lakini matumizi ya dawa hizi mwezi mmoja kabla ya kubeba mimba yanaongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mimba za mapacha.

9. Kuwa na watoto tayari

Wanawake ambao wamezaa mtoto mmoja au wawili kabla wana nafasi kubwa sana ya kuzaa mapacha kuliko wale ambao hawajawahi kuzaa kabisa, ukifuatilia mapacha wengi hua hawazaliwi mimba ya kwanza ila kwanzia mimba ya pili kwenda mbele.

10. Kupata mimba ukiwa kwenye dawa za uzazi wa mpango

japokua sio rahisi sana lakini tafiti zinaonyesha kwamba mimba zinazoingia kwa bahati mbaya mwanamke akiwa anatumia dawa za uzazi wa mpango hutengeneza mapacha lakini pia mimba zinazoingia muda mfupi baada ya kuacha dawa za uzazi wa mpango pia huwa zinaleta watoto mapacha.

Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito bonyeza hapa.

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175