Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo

Published by Fadhili Paulo on

VITU 6 NILIVYOJIFUNZA KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

 

1. Vinaweza kumpata mtu yeyote.

Mwanzoni  mwa miaka ya 1980 wakati madaktari na watu wengine wote walipokuwa wakiwaambia watu kwamba vidonda vya tumbo vilikuwa vinasababishwa na msongo wa mawazo (stress) na vyakula vyenye kusisimua (vyenye pilipili – spiced foods), wanasayansi wawili kutoka Australia wakagundua kwamba pamoja na hayo kisababishi kikuu kingine cha vidonda vya tumbo ni bakteria ajulikanaye kama ‘Helicobacter pylori’.

Ugunduzi huo wa hawa wanasayansi wawili ndiyo ukawawezesha kupata tuzo ya Nobel ya mwaka 2005 na kukaanza zama za kutibu vidonda vya tumbo kwa kutumia antibiotiki.

Pamoja na hayo yote bado jinamizi la vidonda vya tumbo limeendelea kusumbuwa mamilioni ya watu kote duniani mwaka hadi mwaka.

Inakadiriwa katika kila watu watatu mtu mmoja ana vidonda vya tumbo na wengi wa hawa wagonjwa tayari wamekata tamaa kwamba kuna kupona vidonda vya tumbo na wameamua na wamekubali kuishi na vidonda vya tumbo kama sehemu ya maisha yao.

Pia matumizi ya muda mrefu mrefu au ya mara kwa mara ya baadhi ya dawa za hospitali kama vile ibuprofen au aspirin nayo huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo.

2. Inachukuwa muda kufahamu ni nini hasa unatakiwa kula

Inachukuwa muda kufahamu ni chakula gani hasa unatakiwa kula na ni vyakula vipi hutakiwi kula.

Vyakula vikuu unavyopaswa kupenda kula ni vile vinavyokupeleka kupunguza asidi, gesi na sumu mwilini.

Kumekuwa na mkanganyiko na marumbano ya hapa na pale juu ya nini mgonjwa wa vidonda vya tumbo unaweza kula au usile.

Kwa hapa mimi nilipata somo kuu moja tu nalo ni kuhakikisha asilimia 80 ya chakula chako kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani.

Hii ina maana kwamba kama kwa siku unakula chakula cha uzito wa kg 2 kwa mfano basi kg 1 na gram 80 ziwe ni matunda na mboga za majani na gram 20 tu ndiyo viwe vyakula vingine ambavyo bado ni vyakula rafiki kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Watu wengi tunaposema ule kwa wingi matunda na mboga za majani huwa hawaelewi.

Wanafikiri ni kitendo cha wewe kula wali sahani imejaa halafu umalizie na chungwa au parachichi moja eti ndiyo umekula matunda.

Siyo hivyo.

Inafaa hiyo sahani iliyojaa ugali ndiyo ijae mboga za majani au matunda na ugali uwe ndiyo matonge 10 au 15 tu.

Ili kupata faida hasa kwa upande huu amua na utenge mlo mmoja katika milo yako mitatu kwa siku mlo mmoja uwe ni matunda au mboga za majani pekee.

Ningekushauri mlo wa asubuhi uwe ni matunda tu au juisi ya matunda yenye asali ndani yake na siyo sukari au mlo wako wa usiku uwe ni matunda na mboga mboga za majani tu.

Kama utaweza kupata mboga ya majani unayoweza kuila ikiwa mbichi bila kupikwa katika moto hiyo ndiyo nzuri zaidi kwako.

Wazungu wana mboga nyingi za namna hii ambazo huliwa mbichi hivyo hivyo bila kupikwa.

Nakushauri upande mti wa mlonge nyumbani kwako, majani yake yanaweza kuliwa mabichi na yana vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa. Ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako kwa siku inakutosha kwenye kachumbali au hata katika juisi ya matunda.

Pia pendelea kula kabeji mbichi mara kwa mara.

Ukifeli hapa kwenye vyakula kupona kwako vidonda vya tumbo itakuwa ni mtihani na utakata tamaa na utaamini vidonda vya tumbo havitibiki jambo ambalo si kweli.

Ukweli ni kwamba hata madaktari wenyewe bado hawafahamu ni kwa vipi baadhi ya vyakula vinasababisha gesi na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.

Ukiacha vyakula au vinywaji, tumbo lenyewe kwa asili huitengeneza hii asidi ili kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake ya kumeng’enya chakula.

Kwa ujumla kama una vidonda vya tumbo utalazimika kuacha kabisa vitu kama pombe, sigara, sukari, soda, kahawa, chai ya rangi, vyakula vinavyosindikwa viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi.

3. Kufunga kula au kuacha kula ni hatari kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo

Kufunga kula au kuacha kula hakuwezi kukusaidia na pengine kunaweza kukuongezea vidonda zaidi.

Kwa sababu unapoumwa vidonda vya tumbo mawazo yako mengi yanakuwa kwenye kuwaza ule nini na usile nini ili kuhofia madhara yanayoweza kukutokea kuna wakati unaweza kuamua bora usile kabisa chochote.

Huo ni uamuzi mbaya kuliko wote unaweza kuuchukuwa unapoumwa vidonda vya tumbo.

Bila kula chochote au kukaa masaa mengi bila kula tumbo lako linakuwa limebaki kwa sehemu kubwa na asidi tu ambayo inaweza kupelekea kuongezeka zaidi kwa vidonda vya tumbo.

Kula milo midogo midogo mingi na usikae muda mrefu bila kula na wala huhitaji kufunga kula.

Kanuni ni ile ile, matunda na mboga za majani.

4. Usile chakula na kulala wakati huo huo

Usile wakati wa kulala.

Kuna nyumba zingine zina mambo ya ajabu huwezi hata kuamini. Eti mama anaingia jikoni kupika chakula cha usiku saa tatu usiku!

Ukila saa tatu au saa nne usiku utalala saa ngapi?

Kuna mtu akimaliza tu kula anajitupa kitandani kulala.

Kama kweli unaumwa vidonda vya tumbo na umeamua kupona au kuzuia usipatwe na vidonda vya tumbo huwezi kuishi hivyo.

Kama unataka maumivu ukiwa usingizini au maumivu ya vidonda vya tumbo nyakati za usiku basi wewe maliza tu kula na ujitupe kitandani, utaniambia habari yake.

Tangu umekula chakula na unapoenda kulala kuwe na tofauti ya kati ya lisaa limoja hata masaa mawili.

Hivyo kama wewe huwa unaingia kitandani kulala saa tatu usiku basi jitahidi kwenye saa moja kamili au saa moja na nusu jioni uwe tayari umekula.

Na ukishakula usikae chini. Ukimaliza kula tembea tembea kwa miguu hata nusu saa ndiyo utulie.

Kitendo cha kumaliza kula na ukaamua kutembea tembea huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake kwa kiwango chake cha juu kabisa na kwa ufanisi mkubwa.

Unapomaliza kula na kujitupa kitandani unauzuia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizui na utaambulia maumivu zaidi ya vidonda.

Kwa kipande hiki napenda kuongeza pia kama utaweza kuwa unakula chakula chako huku umesimama na ukimaliza hukai chini unatembea tembea kama nusu saa hivi wewe unaweza kupona haraka zaidi vidonda vya tumbo.

Unapokuwa umekaa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unakuwa unafanya kazi chini ya kiwango na pengine gesi na asidi vinaweza kujitengeneza kirahisi kwa njia hiyo ya kukaa kwenye kiti au chini muda mwingi.

5. Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi

Mara nyingi sana nakutana na comment zinazouliza je mwenye vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau? Ndimu? Tangawizi? Kitunguu swaumu? Machungwa ? na mengine mengi ya namna hiyo.

Na wengine wanaweza hadi kukujaji na kukuona hujuwi lolote kwa sababu umemwambia ale chakula fulani ambacho daktari wake alimwambia asile.

Kwa sehemu kubwa tumbo lenyewe huitengeneza hii asidi hata kama utakula vizuri kiasi gani.

Matokeo ya mwisho kabisa ya asidi ni saratani.

Ndiyo maana unakutana na mtu hajawahi kuvuta sigara wala kunywa pombe na anaugua saratani fulani!

Nimekutana na wachungaji wanaumwa saratani, wachungaji hata mashehe wanaumwa bawasiri na kadharika na watu hawa ni wale wapo makini sana juu ya nini wale na nini wasile au kunywa.

Wanawake wengi sana wanaumwa saratani ya matiti na wengi wao hawajawahi kutumia kilevi chochote.

Kwahiyo unakutana na mtu hapa anauliza eti mwenye vidonda vya tumbo anaruhusiwa kutumia limau? Ukimjibu ndiyo anakuona wewe hujuwi kitu kutokana na alivyoaminishwa na daktari wake.

Ni msitu mkubwa. Hivyo mpendwa kuwa mpole.

Limau kwa mfano lina vitamini C ambayo ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Limau linapokuwa nje ya mwili ni asidi lakini kile wewe hufahamu ni kuwa limau linapofika chini tumboni hubadilika na kuwa alkalini tena alkalini ile nzuri kuliko hata ya kwenye mboga za majani au matunda mengine.

Kwahiyo usiwe bize sana kukariri hiki ni asidi na hiki siyo asidi kwa sababu tumbo lenyewe kwa asili lazima liizalishe hii asidi ili mfumo wake wa mmeng’enyo wa chakula uweze kufanya kazi yake.

Uwe ni mtu uliye tayari kujifunza > open minded.

Endelea kupenda kula zaidi matunda na mboga za majani huku ukiepuka kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi.

6. Usiidharau stress (msongo wa mawazo)

Kuna uhusiano kati ya msongo wa mawazo na vidonda vya tumbo na kila kimoja kinaweza kumleta mwenzake.

Msongo wa mawazo (stress) unaweza kuleta vidonda vya tumbo na vidonda vya tumbo vinaweza kuleta msongo wa mawazo.

Jambo baya na la kipuuzi kabisa unaweza kufanya unapoumwa vidonda vya tumbo ni kuwa na stress.

Kwahiyo jikaguwe na ujipeleleze ni kitu gani hasa ndiyo sababu ya wewe kuwa na msongo wa mawazo na ukiondowe hicho kwenye maisha yako bila kujali ni nini au ni nani.

Usiiuguze stress wala usikubali kuishi nayo.

Haijalishi itakugharimu nini, uamuzi mzuri kabisa unaweza kuufanya kwenye maisha yako ni kuamua kuishi maisha ya amani na utulivu bila msongo wowote wa mawazo usio na kichwa wala miguu.

Kumbuka maisha ni mafupi na maisha ni yako na hii dunia ni kubwa sana ina mahitaji ya kumtosha kila mtu ni wewe tu kuamua kubadilika na kufungua akili zako.

Usijifungie kwenye boksi.

Lolote linalokusibu lina suluhisho lake.

Ongea na watu, kaa na watu.

Kwa kawaida hata kama hupendi au hutaki mwili wenyewe utaelekeza nguvu kushughurika na stress kwa sababu ni jambo linalohitaji kutokuwepo.

Sasa hizi nguvu ambazo mwili wako unazielekeza kushughulika na stress ndiyo hizo hizo zingetumika kuutibu mwili dhidi ya vidonda vya tumbo.

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Kwamba wewe ushughulike na stress na mwili ushughulike na uponyaji au wewe ushughulike na uponyaji jambo ambalo huliwezi na mwili ushughulike na stress.

Upe mwili uwezo wake wa asili wa kujitibu kwa kuamua kujitenga mbali na msongo wa mawazo.

Kumbuka duniani tunapita na tuna muda mchache sana wa kuwa hapa.

Ishi vizuri kwa amani, furaha na upendo.

Kama unapenda kujifunza mambo mengine zaidi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza hapa

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

(Visited 692 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175