Vitu 6 wanawake wanatakiwa kufanya ili kujikinga na uvimbe kwenye kizazi

Published by Fadhili Paulo on

Vitu 6 wanawake wanatakiwa kufanya ili kujikinga na uvimbe kwenye kizazi

Inakadiriwa asilimia 70 mpaka 80 ya wanawake wanaweza kupatwa na ugonjwa huu katika safari yao ya kuishi.

Hata hivyo si wanawake wote wenye uvimbe kwenye kizazi wanaweza kuonyesha dalili kwamba wanao au wanahitaji matibabu.

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid.

Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Jambo la mhimu kufahamu kuhusu uvimbe huu ni kuwa si kweli kwamba unaweza kupelekea saratani kama hatua zake za mwisho za ugonjwa kama baadhi ya watu wanavyoweza kukutisha.

Jambo la mhimu kufahamu kuhusu uvimbe huu ni kuwa si kweli kwamba unaweza kupelekea saratani kama hatua zake za mwisho za ugonjwa kama baadhi ya watu wanavyoweza kukutisha. Click To Tweet

Vile vile si kweli kwamba ni upasuwaji tu ndiyo njia pekee ya uhakika ya kutibu uvimbe kwenye kizazi.

Zipo dawa rafiki zinazoweza kutumika na ukapona bila kulazimika kufanya upasuwaji.

Uponyaji wake kwa kawaida huwa ni wa pole pole lakini kwa uvumilivu na kuendelea kuzingatia maelezo na ushauri wa daktari ni ugonjwa unaotibika.

Ingawa uvimbe kwenye kizazi unaweza kuwa ni moja ya sababu inayokuzuia usipate ujauzito, bado wapo baadhi ya wanawake wana uvimbe kwenye kizazi na ujauzito wanapata.

Vitu 6 wanawake wanatakiwa kufanya ili kujikinga na uvimbe kwenye kizazi (Fibriod)

1. Weka sawa homoni zako

Ili kuepuka kupata uvimbe kwenye mji wako wa uzazi unahitajika kuhakikisha homozi zako zipo sawa kila mara.

Wakati wowote usawa wa homoni ya ‘estrogen’ unapozidi mwilini mwako ni wakati huo pia uvimbe kwenye mji wako wa uzazi unaweza kujitokeza.

Kuongezeka zaidi kwa usawa wa homoni ya ‘estrogen’ mara nyingi kunaweza kuwa ni matokeo ya matumizi ya mara kwa mara ya dawa za uzazi wa mpango au inaweza kutokea pia unapopata ujauzito.

Soma pia hii 👇

Dawa ya asili ya kuweka sawa homoni

2. Dhibiti uzito wako

Vitu 6 wanawake wanatakiwa kufanya ili kujikinga na uvimbe kwenye kizazi 1

Kuwa makini na uzito wako wa mwili ili kujikinga na tatizo la uvimbe kwenye mji wa uzazi (fibroids).

Uzito uliozidi ni sababu nyingine inayoweza kurahisisha kutokea kwa ugonjwa huu mwilini mwako.

Tabia zifuatazo zitakusaidia kupunguza uzito wako;

 • Kupunguza kiasi cha chakula unachokula,
 • Kufunga kula mara kwa mara,
 • Kupunguza kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi, na
 • Mazoezi ya viungo ya mara kwa mara

Soma hii pia 👇

Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi

Unataka kujuwa ikiwa una uzito sawa au uliozidi?

Tumia kikokotoo cha BMI (BMI calculator) hiki hapa chini.

Bonyeza Nataka Kupima Uzito kisha andika urefu wako katika sentimita na uzito katika kilogramu kisha bonyeza KOKOTOA itakuambia kama una uzito sawa au umezidi au una uzito pungufu.

Pima uzito hapa

require
require require

Your BMI is......

BMIClassification
less than 18.5:Underweight
18.5 - 24.9:Normal weight
25 - 29.9:Overweight
30 - 34.9:Class I Obese
35 - 39.9:Class II Obese
40 upwards:Class III Obese

.

3. Acha baadhi ya vipodozi

  Ili kujikinga, kuzuia au kujiongezea nafasi ya kupona haraka uvimbe kwenye kizazi kama mwanamke utahitaji kuacha kutumia vipodozi ambavyo vimekatazwa wazi na wizara ya afya na hata vile ambavyo vimeruhusiwa lakini siyo vya asili zaidi.

  Losheni, krimu na vipodozi vingi vya dukani vina kemikali ambazo zinaweza kuuingia mwili wako kirahisi kupitia ngozi yako na kukuletea wewe usawa usio sawa wa homoni (endocrine imbalance) na uwezekano mkubwa wa kupatwa na uvimbe kwenye kizazi.

  Ndiyo sababu tatizo hili la uvimbe kwenye kizazi limeongezeka sana miongo mitatu iliyopita sababu ndiyo wakati wanawake wengi wamekuwa bize sana na vipodozi kuliko miaka ya nyuma.

  4. Weka sawa shinikizo lako la juu la damu

  Utatakiwa pia kupunguza na ikiwezekana kutibu shinikizo lako la juu la damu (high blood pressure – BP) kama unalo.

  Tafiti nyingi zinathibitisha kwamba wanawake wanaoumwa shinikizo la juu la damu wanapatwa kirahisi zaidi pia tatizo la uvimbe kwenye kizazi.

  Pengine umeshaambiwa kuwa shinikizo la juu la damu halina dawa ya kutibu na hivyo utatakiwa kuwa mtumwa wa kumeza dawa miaka yote!

  Ningependa kukuambia habari mpya kwamba shinikizo la juu la damu linaweza kutibika na kuisha kabisa hasa kwa kutumia dawa za asili na kuzingatia vyakula na mazoezi ya viungo.

  Soma na hii pia 👇

  Ukweli kuhusu chumvi na maajabu yake

  Vitu vingine viwili unavyotakiwa kuvifanya ili kujikinga au kujiongezea nafasi ya kuweza kupona uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na

  5. Utaacha kula nyama nyekundu ikiwemo nyama choma na mishikaki

  6. Utaacha pia vilevi vyote

  Soma zaidi kuhusu uvimbe kwenye kizazi kwa kubonyeza hapa.

  Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

  Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

  Vitu 6 wanawake wanatakiwa kufanya ili kujikinga na uvimbe kwenye kizazi Click To Tweet

  Share post hii na wengine uwapendao

  Fadhili Paulo
  Imesomwa mara 285

  Fadhili Paulo

  Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

  2 Comments

  chriss · 09/19/2020 at 11:07 am

  je kuwa na kauvimbe kwenye korodani inaweza kusababisha usitungishe mimba? na tendo la ndoa naenda nalo vizuri

   Fadhili Paulo · 09/22/2020 at 3:35 am

   Hapana hiyo siyo sababu ya wewe kushindwa kutungisha mimba. Ni vizuri ufanye kipimo cha sperm analysis kuona ubora wa mbegu zako na afya yako ya uzazi kwa ujumla

  Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *