Vyakula 14 vya mhimu zaidi kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu

Published by Fadhili Paulo on

Vyakula 14 vya mhimu zaidi kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu

Last Updated on 22/05/2021 by Fadhili Paulo

Vyakula 14 vya mhimu zaidi kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu

Shinikizo la juu la damu ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu.

Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la juu la damu ni mojawapo ya magonjwa ambayo huitwa muuwaji wa taratibu (silent killer), magonjwa mengine ya namna hii ni pamoja na kisukari, ugonjwa wa moyo, kansa na virusi vya magonjwa ya ini.

Silent killers ni magonjwa ambayo wakati mwingine unaweza usione dalili zozote lakini yanaweza kupelekea kifo kama hutachukua hatua stahiki mapema.

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini.

Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Kujifunza mengi zaidi kuhusu shinikizo la juu la damu bonyeza HAPA.

Vyakula 14 vya mhimu zaidi kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu

1. MAJI YA KUNYWA

Maji ni uhai.

Sababu ya kwanza ya watu wengi kupata shinikizo la juu la damu ni kutokana na ukweli kwamba hawanywi maji ya kutosha kila siku.

Na wengi kama siyo wote wanasubiri kiu ndipo wanywe maji.

Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji, huhitaji usikie kiu ndiyo unywe maji.

Asilimia 85 za ubongo wa binadamu ni maji, wakati asilimia 94 za damu yako ni maji.

Sasa kama asilimia 94 ya damu yako ni maji ina maana ubora wa damu yako unategemea unakunywa maji kiasi gani kila siku.

Hivyo ili kupona shinikizo la juu la damu kutegemea na uzito wako, hakikisha unakunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu.

Wakati huo huo utumie chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako hasa ile chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijapita kiwandani.

Najuwa tayari umeambiwa kuwa chumvi ni mbaya na kuwa ni lazima ukae nayo mbali ili kujikinga na kupona shinikizo la juu la damu, hata hivyo hilo siyo kweli, ingekuwa ni kweli kwanini sasa madrip ya maji huwekwa chumvi ndani yake?.

Hakuna daktari anayeweza kumtundikia mgonjwa drip la maji lisilokuwa na chumvi ndani yake. Kila lita moja ya drip la maji huwa pia na chumvi gramu 9 ndani yake!

Kama huna mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku ndiyo hapo chumvi inaweza kuwa mbaya tofauti na hapo unahitaji chumvi ya kutosha kila siku.

Soma hii pia > Ukweli kuhusu Chumvi na Maajabu yake

2. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu kimeendelea kujipatia umaarufu katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Kitunguu swaumu pia husaidia damu isigande mwilinini sifa ambayo ni nzuri sana kwa afya ya moyo.

Kitunguu swaumu pia ni kikojoshi cha asili (natural diuretic) na hivyo kinasaidia kuyalazimisha maji yaliyozidi mwilini pamoja na sodiamu kutoka nje ya mwili ya kupitia mkojo ambao utauzalisha kama matokeo ya kutumia kitunguu swaumu.

Utaona unapata mkojo mara kwa mara ambao ni msafi mweupe, tendo hili husaidia kudhibiti shinikizo la juu la juu na wakati huo huo kuupa utulivu moyo wako kwa ujumla.

Soma hii pia > Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

3. KAROTI

Karoti ina sifa kuu ya kuondoa sumu mwilini, pia ina vitamini A na vitamini C.

Vitu hivi vya asili vinavyoondoa sumu mwilini hupunguza mwilini vitu vinavyosababisha kutokea kansa pia hulinda mishipa ya damu isidhurike na kupunguza kufa kwa seli.

Karoti pia zina kiasi kingi cha elektrolaiti na potasiamu.

Potasiamu ni madini mhimu kwa ajili ya kuweka sawa usawa wa maji mwilini na hivyo kuweka sawa shinikizo la damu.

Potasiamu huziweka chini ya ulinzi hasara zinazoweza kuletwa na sodiamu mwilini.

Jinsi ya kutumia : Kunywa glasi 1 (robo lita) ya juisi ya karoti asubuhi na nyingine 1 jioni kila siku bila kuongeza sukari ndani yake.

4. NYANYA

Nyanya zina beta-carotene, vitamini E, potasiam, na huondoa sumu pia mwilini, vitu vyote hivi ni mhimu katika kushusha shinikizo la juu la damu.

Nyanya pia zina kitu kinaitwa ‘lycopene’, hii ni kemikali ambayo huipa nyanya rangi nyekundu na ambayo ndiyo husaidia kuondoa kolesto mbaya mwilini na kuzuia mafuta kujijenga kwenye mishipa ya damu.

Mafuta haya yanayojijenga kwenye mishipa ndiyo pia husababisha magonjwa ya moyo.

Namna ya kutumia: Kula kikombe kimoja cha nyanya fresh kila siku, au tumia kikombe kimoja cha juisi ya nyanya kila siku.

Epuka juisi au nyanya za dukani.

5. KOMAMANGA (Pomegranate)

Komamanaga siyo tu zina viinilishe vingi mhimu bali pia zina kazi mhimu ya kuondoa sumu mwilini.

Komamanga ni matunda yenye gamba gumu na juisi inayotokana na mbegu zake ndiyo hutumika kama dawa.

Komamanga zina vitu vitatu mhimu navyo ni ‘phytochemicals’ ambacho huondoa sumu mwilini na kuzuia seli zisizulike kirahisi, kitu cha pili na cha tatu vilivyomo kwenye komamanga ni ‘polyphenols’ na ‘punicalagin’ ambavyo hivi hupigana dhidi ya magonjwa ya moyo, kuweka sawa kolesto, kushusha shinikizo la juu la damu, kuzuia mishipa isizibe na kansa.

Komamanga zina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini kuliko hata mvinyo mwekkundu (red wine) au zaidi hata ya chai ya kijani (green tea).

Namna ya kutumia: Kunywa kikombe kimoja cha juisi ya mbegu za komamanga kutwa mara 2 asubuhi na jioni kila siku. Au ongeza mbegu za komamanga kwenye kachumbari (salad) yako kila siku.

6. MAFUTA YA UFUTA (Sesame)

Mafuta yatokanayo na ufuta yana omega 6, vitamini E, na kiinilishe kingine kijulikanacho kama ‘sesamin’ ambacho chenyewe ndiyo huhusika moja kwa moja na kushusha shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na kisukari.

Namna ya kutumia: Fanya mafuta ya ufuta kuwa ndiyo mafuta ya kupikia vyakula vyako unavyokula kila siku na ndani ya mwezi mmoja mpaka miwili hivi utaona hata shinikizo lako la juu lipo sawa.

7. TANGAWIZI

Kwa karne nyingi tangawizi imetumika na watu wa India na bara la Asia kwa ujumla kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu.

Tangawizi pia hutumika kushusha kolesto na kuzuia damu isigande.

Shinikizo la juu la damu ni matokeo ya damu kutokupita kwa uhuru wote kwenye mishipa ya damu, kama tangawizi ina uwezo wa kuzuia damu isigande ni wazi ni nzuri kwa mtu mwenye shinikizo la damu.

Tangawizi pia huzuia mshtuko au kukamaa kwa mishipa na shambulio la moyo.

Namna ya kutumia: Tumia juisi ya tangawizi kikombe kimoja kutwa mara 2 asubuhi na jioni.

Namna inavyoandaliwa hii juisi; tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Unaweza kutengeneza nyingi zaidi na kuihifadhi katika friji, mhimu hapo ni tangawizi. Tumia blenda kutengeneza hi juisi.

Ongeza pia tangawizi kwenye vyakula vingi unavyopika kila siku.

8. MAJI YA NAZI (dafu)

Maji ya nazi yana potasiam na magnesium vitu viwili mhimu kwa mishipa ya moyo.

Maji ya nazi hufanya kazi kama vile dawa za kukojosha (diuretic) kwa kuyalazimisha maji yaliyozidi mwilini kutoka nje huku yakisaidia kushikilia ndani ya mwili madini mhimu ya potasiamu.

Maji ya nazi ni mazuri kama ni freshi na siyo yawe yametengenezwa na kuuzwa dukani tena.

Namna ya kutumia: Kunywa glasi moja (ml 250) za maji ya nazi kutwa mara 3.

Ukiacha kushusha shinikizo la juu la damu maji haya husaidia pia kushusha uzito.

Soma hii pia > FAIDA 39 ZITAKAZOKUSHANGAZA ZA MAFUTA YA NAZI KIAFYA

9. ILIKI (Cardamom)

Iliki ni kiungo (spice) ambacho kimekuwa kikitumika katika dawa za asili za kihindi kwa maelfu ya miaka mingi sasa.

Inatumika zaidi kwa matatizo ya moyo, matatizo ya tumbo, matatizo ya kibofu cha mkojo, kiungulia na matatizo mengi katika mfumo wa upumuwaji.

Iliki ina sifa nyingi ikiwemo ya kuondoa sumu, kuondoa bakteria na kansa.

Iliki husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kuruhusu damu kupita kirahisi zaidi na hivyo kupunguza shinikizo shinikizo la juu la damu kwa asili kabisa bila madhara mengine mabaya.

Namna ya kutumia: Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha iliki ya unga katika maji ya uvuguvugu glasi 1 ongeza asali kidogo kupata radha koroga vizuri na unywe yote.

Fanya hivi kutwa mara 2 asubuhi na jioni kila siku.

10. BINZARI (Turmeric)

Binzari ndiyo kiungo au dawa ya asili pekee ambayo inafuatiliwa na kusomwa na watu wengi zaidi duniani.
Inajulikana kwa uwezo wake wa kuondoa maambukizi karibu katika kila sehemu ya mwili.

Kwa kuondoa maambukizi, bizari huuongezea nguvu msukumo wa damu na kazi za moyo kwa ujumla.

Binzari inaweza kusaidia pia kuondoa takataka zinazojijenga kwenye kuta za mishipa, pia ni dawa ya asili ya kufanya damu isigande mwilini kama matokeo yake huweka sawa shinikizo la juu la damu.

Namna ya kutumia: Ongeza kijiko kidogo kimoja cha binzari ya unga kwenye glasi 1 ya maji ya uvuguvugu, ongeza tangawizi kidogo na asali kidogo kupata radha, koroga vizuri na unywe yote kutwa mara 2 kila siku.

Ongeza pia binzari kwenye vyakula vyako vingi unavyopika.

Soma hii pia > JITIBU ALEJI KWA KUTUMIA BINZARI

11. VYAKULA VYENYE OMEGA 3

Vyakula au kingine chochote chenye Omega 3 husaidia sana kuweka sawa shinikizo la juu la damu na kolesto pia.

Unahitaji kutumia vyakula vyenye omega 3 kila siku iendayo kwa Mungu kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu.

Vyanzo vizuri vya omega 3 ni mafuta ya samaki au samaki wenyewe, mayai (mayai ya kienyeji), parachichi, spinachi, mbegu za maboga au mafuta yake, pia mafuta ya asili ya nazi.

Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi kutwa mara 2 kila siku ili kuweka sawa shinikizo lako la damu.

Tafuta pia vyakula vingine vyenye omega 3 na upendelee kuvitumia hivyo kila mara.

12. VITAMINI D

Vitamini D hupatikana kirahisi katika miale ya jua, nah ii ndiyo vitamini inayohusika na udhibiti wa jeni (genes) zaidi ya 200 mwilini.

Vitamini hii pia inahusika usitawi na ukuwaji sahihi wa seli za mwili.

Kwa kawaida asilimia 50 mpaka 90 za vitamin D hupatikana kwa mwili kutoka kwenye jua moja kwa moja.

Pamoja na jua tunatakiwa pia kutumia vyakula vyenye vitamini D kwa wingi tunaposhambuliwa na shinikizo la juu la damu.

Viatmini D inapatikana kirahisi katika mayai, samaki, na katika nyama pia.

Maisha ya kisasa yanapelekea watu wengi kuwa ndani ya ofisi karibu kutwa nzima na hivyo kuwapelekea kukosa mwanga wa jua moja kwa moja.

Upungufu wa vitamini D mwilini ni tatizo linaloendelea kuongezeka kila siku duniani.

Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha matatizo kama shinikizo la juu la damu na magonjwa mengine kadhaa ikiwemo matatizo ya akili, kansa, kushuka kinga ya mwili na matatizo mengine yanayohusiana na uzazi.

Katika utafiti mmoja mwaka 2014 iligundulika kuwa vitamini D husaidia kushusha shinikizo la juu la damu.

Vitamini D huidhibiti homoni ya ‘renin’ na kuleta matokeo sawa na yanayoletwa na homoni nyingine ya ‘angiotensini’.

Dawa sawa zinazodhibiti kazi za rennin na angiotensin hutolewa kwa wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu.

Tembea kwenye jua lisaa limoja kila siku iendayo kwa Mungu ukiwa hujavaa nguo nyingi ili jua liweze kukufikia kila sehemu ya mwili wako.

13. PUMZIKA (Relax) na USIKILIZE MUZIKI UUPENDAO

Jambo moja la kushangaza ni kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja wa msongo wa mawazo (stress) na shinikizo la juu la damu.

Na mara nyingi nimesema stress inaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50 ikiwemo shinikizo la juu la damu.

Muziki unao matokeo ya kukupa pumziko na kukuletea utulivu wa akili na nafsi.

Sikiliza muziki uupendao kama ni wa kidunia au wa kiMungu ni sawa mhimu ukuletee utulivu unaohitaji.

Aina ya muziki ni jambo la mhimu pia, usiwe muziki wa kukuongezea mawazo au shida nyingine tena bali ni ule mzuri mtulivu wenye kuiweka akili yako sawa na siyo wa kukuletea hamasa ya mipasho mingine tena.

Kusikiliza muziki mzuri kwa dakika 30 tu kwa siku kunaweza kusaidia kushusha shinikizo lako la damu, kushusha mapigo ya moyo na kupunguza hamaki (panic).

Muziki unaosemwa kusaidia kushusha shinikizo la juu la damu ni ule unajulikana kwa kiingereza kama ‘slower tempo classical music’, utafute kwenye google au youtube.

Miziki hii ifuatayo inaongeza presha nayo ni rap (ya kufokafoka), pop, jazz, na rock .

Tenga muda kila siku usikilize muziki uupendao.

14. MAZOEZI YA VIUNGO

Uzito wako unapokuwa juu unaongeza shida zingine kwenye kuta zako za mishipa ya damu na kuulazimisha moyo wako kufanya kazi kwa shida masaa 24 siku 7 za wiki.

Uzito uliozidi pia unakuweka katika hatari ya kupatwa na magonjwa mengine kama matatizo mbalimbali ya mishipa ambayo yanaweza kupelekea shinikizo la juu la damu, shambulio la moyo na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (stroke0.

Maisha ya kukaa tu kwenye kiti masaa yote yanapelekea hatari ya kupatwa shinikizo la juu la damu kwa zaidi ya asilimia 30.

Kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku ndiyo zoezi mhimu kuliko yote unaloweza kulifanya kwa ajili ya afya ya mwili wako.

Tafiti zinaonyesha kutembea kwa miguu saa moja kila siku bila kupumzika (none stop) au kukimbia mdogo mdogo (jogging) kila siku kunasaidia sana kuweka sawa shinikizo la juu la damu pia husaidia kupata usingizi mzuri na mtulivu.

Soma pia hii > Jinsi ya kupungua uzito huku unacheka

MHIMU SANA:

Ni mhimu kuhakikisha kuwa unaliweka katika hali ya usawa shinikizo lako la damu. Kwa bahati mbaya hakuna njia ya mkato ya kulitekeleza hilo wala hakuna dawa ya kukuponya ndani ya siku 2.

Lishe bora na mazoezi ya nguvu ya kila siku ni mhimu katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Mambo 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la juu la damu:

1. Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
2. Kula nyama isiyo na mafuta mengi
3. Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
4. Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
5. Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
6. Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
7. Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
8. Acha kunywa pombe
9. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
10. Punguza mfadhaiko au stress
11. Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.

Ikiwa utahitaji dawa za asili au dawa lishe za asili kwa ajili ya shinikizo la juu la damu, niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175.

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao.

Vyakula 14 vya mhimu zaidi kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu Click To Tweet

Nifuate kwenye Twitter

Bonyeza kengele ili kujiunga kupokea kidokezo kila mara makala mpya inapoandikwa hapa.

Fadhili Paulo
(Visited 10 times, 1 visits today)

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175 Nifuate kwenye > Twitter

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175