VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI

Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.

Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani kama umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu na ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula na mitishamba 16 inayoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

Vyakula vinavyoongeza Kinga ya mwili

1. Mtindi

Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako.

Mtindi pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza kinga ya mwili wako

2. Matunda

Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Unaweza kuamua pia moja ya mlo wako katika siku kama ni wa jioni au wa mchana au wa asubuhi uwe ni matunda tu na si kitu kingine zaidi. Jaza kwenye sahani yako ndizi, embe, papai, nanasi, tikiti maji, parachichi nk, sahani iwe na matunda tu kula hadi ushibe matunda tu.

3. Tui la Nazi

Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huwa na uwezo wa kuiimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

Matumizi ya nazi kama tiba ya kuimarisha kinga ya mwili duniani yalishika kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii. Waathirika wa UKIMWI toka sehemu mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba.

Dozi yake ni rahisi, kunywaji glasi nne za tui la nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na kupungua kwa kinga ya mwili na pia hung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama kinga yako imepunguwa basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu.

Kama tayari una vidonda mwilini visivyopona basi uwe unapakaa mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

Hata hivyo najua kuwa si watu wote wako kwenye mazingira ya kupata nazi kirahisi au kupata nazi bora yenye virutubisho vinavyotakiwa.

Hivyo ikiwa utahitaji tui la nazi lililoandaliwa tayari kwa matumizi niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

4. VITUNGUU SWAUMU

Hupatikana kwa wingi Tanzania!

Japokuwa vitunguu swaumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu.

Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

Chukuwa kitunguu swaumu kimoja, Kigawanyishe katika punje punje, chukua punje 6 menya punje moja baada ya nyingine. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu, Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala.

5. Asali yenye Mdalasini

Asali ni dawa kwa kila ugonjwa.

Zingatia tu unapata asali mbichi na nzuri ya asili kwani endapo utauziwa asali iliyochakachuliwa kuna hatari ya kuharibu afya yako zaidi.

Asali ina sifa ya kudhibiti bakteria. Nadharia hii inathibitishwa na tafiti nyingi kadhaa. Asali hupigana dhidi ya maambukizi ya ndani na ya nje.

Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe, pia huondoa sumu mwilini.

Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili yaani asali na mdalasini vinatengeneza muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.

Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

Asali yenye Mdalasini ni dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

Kama unahitaji Asali yenye Mdalasini niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

6. UYOGA

Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

7. SUPU YA KUKU

Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

Mhimu ni kuwa supu hii ya kuku hakikisha ni ya kuku wa kienyeji tu.

8. Ubuyu

Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku (kumbuka uwe ubuyu halisi). Ubuyu una vitamini C nyingi zaidi kuliko ile ipatikanayo kwenye machungwa au maembe.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Kama unahitaji unga wa ubuyu niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

9. VIAZI VITAMU

Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu

10. KAROTI

Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

11. SAMAKI

Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

12. MATIKITI

Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Faida 13 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake

13. MAJI YA KUNYWA

Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunwya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau glasi 8 hadi 10 za maji kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.

Kila mtu ana kiasi cha maji anachohitaji kunywa kila siku kwa mjibu wa uzito wake.

14. Unga wa Mbegu za Maboga

Unga wa mbegu za maboga pia una kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida lukuki mwilini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari nk.

Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

Kama unahitaji unga wa mbegu za maboga niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Dawa za asili kwa ajili ya kuongeza Kinga ya mwili

1. Mafuta ya habbat soda

Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi.

Wengi wetu tunakumbwa na tatizo la kupungukiwa damu (anemia) na hili linaweza kuiweka miili yetu katika hali ya hatari zaidi. Kwa mara nyingine tena mafuta ya habbat soda yanaonekana kuokoa tatizo hili baya la kiafya.

Yamethibitika kutibu tatizo la upungufu wa damu moja kwa moja.

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia vizuri kila mara.

Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat soda kwa siku 30 hivi.

Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni au kufadhaika.

Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili na maisha kwa ujumla.

Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.

Mafuta ya habbat soda ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa muda mfupi.

*Unaweza kutumia dawa hii mpaka miezi 6 mfululizo pia unaweza kuitumia hata kama huumwi chochote.

*Ili ifanye kazi vizuri dawa hii haipaswi kutumiwa sambamba na dawa nyingine yoyote ya hospitali.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

Kama unahitaji mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

2. Unga wa majani ya Mlonge

Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean.

Mti huu umeripotiwa kuwa dawa nzuri kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa bali kwenye majani yake ndiko kuna viinilishe vingi mara dufu zaidi hasa yanapoandaliwa na kuwa katika mfumo wa unga.

Majani ya mlonge yana faida nyingi kiafya yanapokuwa katika mfumo wa unga. Yanaweza pia kutafunwa mabichi yenyewe kama yalivyo au unaweza kuyachanganya kwenye kachumbari, na yanaweza pia kuchemshwa kidogo na kuliwa kama mboga nyingine yoyote ya majani.

Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani.

Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

*Ili ifanye kazi vizuri dawa hii haipaswi kutumiwa sambamba na dawa nyingine yoyote ya hospitali.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu

Kama una swali zaidi niulize hapo chini kwenye comment

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Imesomwa mara 390

Imehaririwa


Avatar

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy Ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam. Ni mwanachama wa Chama Cha Waganga wa Tiba za Asili Tanzania (CHAWATIATA) pia ni mwanachama wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO).

Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp +255714800175