Vyakula 25 vinavyoongeza nguvu za kiume

Published by Fadhili Paulo on

vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi

Katika makala hii nitakueleza juu ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi na nitakueleza chakula kimoja baada ya kingine kiundani zaidi.

Jina langu naitwa Fadhili Paulo.

Endelea kusoma …

Unachotakiwa ni kujijengea mazoea ya kuhakikisha mlo wako kwa siku haukosi hivi vyakula.

Ukiwa mbunifu kwenye kupika kuna uwezekano ukatumia vyote au nusu yake katika chakula chako cha kutwa nzima

Kama bado hujuwi nguvu za kiume ni nini hasa bonyeza HAPA.

Vyakula 25 vinavyoongeza nguvu za kiume

1.Ndizi

.

Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana.

Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi.

Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito.

Ndizi ina kimeng‟enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume na ashki ya mapenzi (libido).

Ndizi ni tunda zuri na tamu sana, lina potasiamu na vitamini B kwa wingi viinilishe ambavyo ni mhimu ili kuamsha hamu ya tendo la ndoa na uzalishwaji wa homoni ya „testosterone‟ kwa ujumla.

Ndizi huongeza nguvu ya mwili kwa ujumla ikiwemo nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa wanaume pia kwa wanawake.

Kula ndizi 2 hadi 3 zilizoiva kila siku.

2. TikitiMaji

.

Tikiti maji ni tunda mhimu sana kwa kulinda ndoa na inatakiwa walau kwa siku upate vipande viwili au vitatu na sasa yapo kwa wingi ushindwe wewe na ni muhimu ukala na mbegu zake kwani ndizo ambazo huwa na nguvu za kiume.

Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga, Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamini A, B6, na C.

Viinilishe vingine kwenye tikiti maji ni pamoja na Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda hili linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalisha misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.

Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni „lycopene‟, „beta-carotene‟ na „citrulline‟ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

Tikiti maji ni viagra ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.

Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi mara kwa mara.

3. Kitunguu Swaumu

.

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.

Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake

kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.

Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali

iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzunguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.

Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Namna ya kutumia kitunguu swaumu:

 • Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
 • Kigawanyishe katika punje punje
 • Chukua punje 6
 • Menya punje moja baada ya nyingine
 • Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
 • Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.

Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama umepona tatizo lako.

Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1

.

4. Siagi ya Karanga

.

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini.

Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini.

Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.

Kwakuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba, magnesium, na potasiamu, siagi ya karanga ni nzuri sana katika kuuweka katika usawa mzuri mzunguko wa damu mwilini.

Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikika kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza mishipa mingi na imara zaidi.

Mimi napenda zaidi kuitumia hii siagi kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi ya karanga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika.

Ukiacha radha yake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi na isiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili.

5. Parachichi

Chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi.

.

Chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi.

Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni.

Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Hili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.

Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E.

Vitamini E husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume.

Kulingana na watafiti tofauti, watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali haswa wakati wa kufanya mapenzi.

Parachichi hujulikana pia kama mkuyati wa asili.

Parachichi ni dawa ya asili ya kuamsha hamu ya tendo la ndoa.

Hapa Tanzania maparachichi yanapatikana kwa wingi sana mkoa wa Kilimanjaro na hata Mbeya pia.

Parachichi lina potasiamu, vitamini B6, folic acid nk, vitu hivi vitatu ni mhimu sana katika kuongeza hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Potasiamu husaidia kuongeza ufanisi wa kazi wa tezi ya „thyroid‟ ambayo yenyewe husaidia kuongeza hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa kama itakuwa ipo kwenye usawa wake mzuri.

Vitamini B6 huhamasisha uzalishwaji wa homoni za kiume na „folic acid‟ ni mhimu katika kuwezesha umeng‟enywaji na kuweka sawa usawa wa protini mwilini.

Kula parachichi moja kila siku.

Unaweza pia kunywa juisi ya parachichi kikombe kimoja kila siku ukiongeza asali vijiko vikubwa viwili ndani yake.

6. Pilipili

Pilipili inaongeza nguvu za kiume

.

Pia pilipili unaweza changanya kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwani zinasaidia mzunguko mkubwa wa damu kwa maana hiyo kufanya kuwa na hisia kali za mapenzi kwa hiyo pili pili ni chachu ya kuuamsha hisia.

Hata hivyo usizidishe kwani zina madhara kama utazitumia kwa wingi.

Kipande kidogo tu cha pili pili kwa siku kinakutosha.

7. Pweza

.

Aina hizi za samaki wanaovuliwa baharini huwa na madini ya zinki na chumvi vitu ambavyo vinatajwa kusaidia kuzalisha vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

Wataalam na wanasayanzi wa ndani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na wa Kimataifa wamethibitisha kuwa supu ya pweza ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.

Wataalam hao wanadai kuwa supu hiyo inafanya kazi hiyo kwa asilimia kubwa tofauti na madawa mengine ya kemikali.

8. Chokoleti

.

Chocolate inasaidia kuongeza stamina katika tendo la ndoa kwa sababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid.

Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati watendo la ndoa na alkaloid huongeza stamina na nguvu.

Usizidishe hata hivyo kwani huwa na kaffeina ambayo ni mbaya tena kwa afya kama utatumia kwa kuzidisha. Kipande kidogo tu cha chokoleti kinatosha na isiwe ni kila siku.

9. Maji ya Kunywa

.

Inapendeza kunywa maji mengi kwa siku na mtu ajitahidi anywe mengi kila siku bila kusubiri kiu.

Maji pia husaidia kuondoa sumu, magonjwa mwilini na homa za mara kwa mara.

Kitu gani husababisha uume usimame?

Unaweza kujibu ni msisimko.

Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi.

Hata hivyo msisimko ni matokeo.

Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko.

Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia.

Kutokusoma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME.

Na kablahujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’.

Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji.

Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU kila siku.

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?

Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume.

Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa.

Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.

Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume.

Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.

10. Komamanga

.

Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na tufaa (apple).

Haya yanatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa zaidi.

Pendelea kula matunda haya mara kwa mara.

11. Mvinyo Mwekundu

red wine

Mvivyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa.

Hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.

Utafiti umedhihirisha kuwa mvinyo mwekundu una wezo wa kuongeza msukumo wa damu.

Elewa kwamba kiwango cha msukumo wa damu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa uume umesimama wakati wa tendo la ndoa.

Pia ni mhimu kutambua kuwa ingawa hii inaweza kutumika kama dawa lakini kama utazidisha kutumia inaweza kukuletea madhara tena badala ya faida.

Kumbuka ni kilevi hivyo ukizidisha utapata shida zaidi.

Inapendekezwa glasi 1 au 2 tu kwa siku inatosha.

Wengi hupendelea kunywa kabla ya chakula.

12. Blueberry

.

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita „viagra‟ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini.

Blueberries kama yanavyoonekana kwenye picha yana virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.

Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa lehemu (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu.

Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.

13. Mtini (FIGS)

.

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini.

Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini.

Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

14. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinki.

Madini ya zinki hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone na mbegu za kiume.

Uwingi wa uzalishwaji wa homoni ya testosterone mwilini huathiri pia hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.

Kupungukiwa kwa madini ya zinki husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

15. Tangawizi

Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume.

Unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai asubuhi, mchana na jioni

Pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kuchanganya pamoja habbat soda, asali, kitunguu swaumu na tangawizi yenyewe.

Kunywa mchanganyiko huu kijiko kimoja cha chakula kutwa mara 2 kwa wiki 3 hivi au hatazaidi na hutakawia kuona tofauti.

Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini.

Kwa hivyo, ni bayana kuwa uume wako utakuwa na damu ya kutosha na pia utaweza kusimama kwa muda mrefu.

Pia, ulaji wa tangawizi husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

16. Ugali wa Dona

Kula ugali wa dona kila siku.

Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume.

Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 20 ongeza ngano kilo 1 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake.

Au wakati unasaga mahindi mwambie msagaji arudie kusaga mara 3 ndiyo utapata unga mzuri mlaini.

Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

17. Kahawa

Kutumia kahawa kupita kiasi kunaweza kusiwe kuzuri kwa afya yako.

Lakini hatukatai kwamba kafeini iliyomo kwenye kahawa inaweza kukupa nguvu nyingi sana za kuweza kuchelewa kufika kileleni mapema.

Tumia kinywaki hiki kwa busara kwani kinaweza kikawa kina faida na hasara kwa upande mwingine pia.

Kikombe kimoja kwa siku kinatosha.

18. Zabibu

Kemikali ya anthocyanins iliyomo kwenye zabibu husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuisafisha mishipa ya ateli na hivyo kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri hasa katika sehemu za uume wako.

Hii ni kwa sababu mishipa ya damu inakuwa imefunguka na damu kutiririka vizuri katika maeneo hayo.

19. Mayai ya Kuku wa Kienyeji

.

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake.

Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.

Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.

Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.

Vyovyote utakavyotaka kama ni ya kukaanga au kuchemsha ni sawa.

20. Spinachi

.

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume.

Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa „folate‟ kwenye mfumo wako wa mwili.

Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi.

Kula Spianchi pia mboga zingine za kijani kila siku.

21. Asali yenye Mdalasini

vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi

.

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa.

Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.

Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali.

Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana.

Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini.

Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI.

Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine – TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East – Tibb).

Kwa mjibu wa wataalamu wa tiba asili nchini China, mdalasini huongeza joto mwilini. Mdalasini hutengeneza joto mwilini lijulikanalo kwa kichina kama “yang”.

Yang hutibu “yin” (yin kwa kichina humaanisha baridi).

Wakati asali yenyewe kwa asili huweka sawa usawa wa joto na baridi mwilini.

Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili.

Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza nguvu ya mwili.

Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja.

Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia.

Lamba vijiko vikubwa viwili kila unapoenda kulala.

Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake.

Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari.

Au unaweza kuweka vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe yote kutwa mara 1 ambapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini.

22. Chumvi ya mawe ya Baharini

.

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili.

Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku na uweke ya kutosha yaani ionekane kwamba humu kwenye chakula kuna chumvi.

Usiogope chumvi kama wewe ni mpenzi wa kunywa maji mengi kila siku.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi Click To Tweet

Share na wengine post hii

(Visited 21,764 times, 1 visits today)

18 Comments

alute · 21/05/2019 at 9:33 am

kwa wenye sukari vipi unawashauri nini katika tendon la ndoa

  Fadhili Paulo · 24/05/2019 at 2:27 am

  Wajitibu kwanza kisukari kabla ya yote. Dawa ipo kwa ajili ya Kisukari, tuwasiliane WhatsApp +255714800175

frank · 23/05/2019 at 10:01 am

hivi ntajuaje kama nimepungukiwa na nguvu za kiume!!?

  Fadhili Paulo · 24/05/2019 at 2:26 am

  Bonyeza HAPA

  Joseph dananilely · 13/01/2022 at 10:49 am

  Nashukru kwa somo

   Fadhili Paulo · 19/01/2022 at 1:22 pm

   Karibu sana Joseph

kyando · 08/02/2020 at 10:20 am

Asante kwa elimu nzuri!!

  Fadhili Paulo · 14/02/2020 at 6:20 am

  Karibu sana ndugu

Denis msonyi · 04/03/2020 at 6:08 am

Good knowledge dr!

  Fadhili Paulo · 04/03/2020 at 5:40 pm

  Thanks Denis

Malik · 28/05/2020 at 1:45 pm

Asante sana kwa kutumia ujuzi wako katika kutuelimisha hasa katika nyanja muhimu zaidi kwa binadam, nyanja ya Afya. Kiongozi mimi nina tatizo linalonisibu, na kwa kuwa umeweka mawasiliano ni vyema nikuelezee kwa kina kupitia namba hii. Shukran ndg.

  Fadhili Paulo · 02/06/2020 at 6:15 pm

  Karibu sana Malik. Tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Said s · 16/07/2020 at 7:03 am

Ahsante kwa elimu dktor

  Fadhili Paulo · 18/07/2020 at 12:49 pm

  Karibu sana ndugu

MAGANYA · 15/10/2021 at 9:33 am

Nimeelewa tunaweza kula kama mlo wa kawaida hivi vyakula vyote na vikatusaidia

  Fadhili Paulo · 17/10/2021 at 4:46 am

  Nafurahi kusikia hivyo

Peter Jackson Odongo · 17/04/2022 at 6:34 pm

uchambuzi mzuri utasaidia wengi.

  Fadhili Paulo · 20/04/2022 at 5:00 am

  Nafurahi kusikia hivyo. Endelea kuja tena na tena

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175