Vyakula 6 vinavyoongeza uume

Published by Fadhili Paulo on

Vyakula 6 vinavyoongeza uume

Afya nzuri kabisa ya tendo la ndoa ni jambo linalotamaniwa na watu karibu wote popote duniani

Na katika juhudi zao za kutaka kuimarisha afya zao za kitandani watu wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuanzia kwenye kutumia dawa hadi kubadili tabia na aina ya maisha wanayoishi ikiwemo kuacha vilevi, kubadili vyakula na kadharika

Tafiti nyingi zilizowahi kufanywa huko nyuma na hata ambazo zinaendelea kufanywa zinathibitisha pasipo na shaka kwamba ukubwa wa uume hauna maana yoyote kwenye mapenzi na uhusiano kwa ujumla

Ni wanaume ndiyo huwa bize kutaka kuongeza uume kidogo huku wake zao wakiwa hawana habari yoyote juu ya hilo

Hata hivyo bado wanaume wameendelea na juhudi zao za kutaka kuongeza uume kwa namna yoyote kote duniani

Siyo wanawake pekee ndiyo huwa bize na muonekano wao, baadhi ya wanaume wanaishi na msongo wa mawazo (stress) kwa sababu ya kuwa na uume mdogo

Unaweza usitambue wala kufahamu hili lakini wanaume wengi huwa na mawazo sana linapokuja suala la ukubwa wa uume wao

Baadhi ya wanaume huchukuwa maamuzi magumu kwa kuamua kutokuwa na mahusiano na mwanamke kwa sababu tu anahisi uume wake ni mdogo

Siyo wanaume wote wamebarikiwa kuwa na uume mkubwa kwa asili

Utasoma pia na hii 👇

Vitu vitatu vinavyoharibu afya ya uume wako

Kwahiyo kama unahitaji kuongeza uume wako kidogo na kwa njia salama bila madhara pendelea vyakula hivi vifuatavyo :

Kwa leo nitaviandika vitatu tu siku nyingine nikipata muda nitaandika vingine vitatu vilivyobaki, endelea kutembelea fadhilipaulo.com

Vyakula vinavyoongeza uume

1. Tende

Tende ni moja ya matunda machache ambayo yanaweza kuimarisha nguvu za kiume, kuimarisha ubora wa mbegu za kiume na kupelekea kukupa korodani kubwa na kukuletea uume kusimama kwa nguvu na hatimaye uume mkubwa

Tende husaidia pia kuongeza ukubwa wa matiti kwa kina mama

Tende zipo kibao huko madukani, jiwekee mazoea ya kula tende au juisi ya tende mara kwa mara na hutachelewa kuona mabadiliko kidogo kidogo kwenye ukubwa wa uume wako

Kila siku kula tende 3 mpaka 4.

2. Ndizi

Pengine mpaka sasa ulikuwa hujuwi bado kama ndizi inaweza kukusaidia kukuongezea ukubwa wa uume wako

Ndizi za kuiva zina kiasi kingi cha madini ya potassium ambayo ni madini mhimu kwa ajili ya kuongeza msukumo wa damu mwilini na kwenye ogani za uzazi

Ndizi pia husaidia kuweka sawa usawa wa sodium mwilini

Kula ndizi mbili mpaka 3 kila siku hasa usiku na utaona hata tatizo lako la kukosa usingizi linapotea kwani ndizi ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuleta usingizi

Wakati matunda haya mawili yaani tende na ndizi hayawezi kukuletea mabadiliko ya kimiujiza na ya haraka lakini ukiwa mdadisi na mvumilivu pole pole utaanza kuona mabadiliko

3. Mizizi ya mnazi

Juisi ya mizizi ya mnazi au mti unaozaa nazi inaweza pia kukusaidia kuongeza kidogo ukubwa wa uume wako.

Mizizi ya mnazi ina vitu viwili mhimu ambavyo ni ‘saponin na flavonoids’ ambavyo husaidia kuondoa sumu kwenye mishipa ya uume na kuongeza wingi wa damu na msukumo kwenda kwenye uume.

Kama juisi hii itaandaliwa kwa ufasaha na kutumika kama inavyotakiwa inaweza kuwa msaada mkubwa katika kukusaidia kuongeza kiasi ukubwa wa mashine yako.

Inashauriwa kutumia maji ya mvua wakati wa kuiandaa juisi hii ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Chukua mizizi kadhaa ya mnazi kama gram 200 hivi kisha weka kwenye sufuria na uongeze maji (hasa maji ya mvua kama yanapatikana) lita 5 na uchemshe kwenye moto huku umefunika mpaka maji yabaki lita 4, ipua toka kwenye moto na acha ipoe kidogo.

Kunywa kikombe kidogo (ml 250) kutwa mara mbili asubuhi na jioni baada ya chakula kila siku kwa siku 18. Unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani ya hicho kikombe cha dawa ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kabla hujaondoka soma pia hii 👇

Jinsi ya kuongeza uume bila dawa


0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175