Vyakula vinavyosababisha vidonda vya tumbo

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni lazima uwe makini sana na chakula unachokula kila siku.

Chakula unachokula kila siku kitaamua ikiwa dawa unayotumia kutibu vidonda vya tumbo itakuponya na kukuacha huna vidonda tena milele au ndiyo utapata nafuu ya muda mfupi tu na baadaye utaendelea kuumwa vidonda tena na tena mpaka utakapokata tamaa na kutoamini kama kuna kupona vidonda vya tumbo.

Chakula unachokula kinapaswa kiwe ni dawa pia. Ulivyo ni kile unachokula kila siku.

Usile tu ili kushiba au kwa sababu unasikia njaa. Lazima ujuwe hiki unachokula ni nini, kina kazi gani mwilini na je kinaweza kusaidia kupona au kupunguza makali ya vidonda vya tumbo?

Hiki unachokula ni nini? Kina kazi gani mwilini? Je kinaweza kusaidia japo kupunguza gesi au kupunguza asidi tumboni na kutibu vidonda au majeraha tumboni?.

Kanuni ya jumla ya chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwa siku ni kuwa asilimia 80 ya chakula unachokula katika siku iwe ni mboga za majani na matunda.

Hii ni kusema kama jumla ya chakula unachokula kwa siku kina ujazo wa kilo 3 basi kilo 2 na nusu ziwe ni matunda na mboga za majani na nusu kilo iliyobaki ndiyo viwe vyakula vingine.

Cha kwanza kabisa unapoamka kitandani asubuhi, yaani ile unatua tu mguu kutoka kitandani ni maji ya kunywa. Ukiamka tu kabla hata ya mswaki unapaswa unywe maji glasi moja (robo lita) au glasi 2 (nusu lita) ndiyo uendelee na maandalizi ya chai na kupiga mswaki na shughuli zingine.

Na hii ni kwa wote haijalishi unaishi sehemu zenye baridi au joto ni lazima kunywa maji.

Maji ya kawaida siyo ya kwenye friji wala siyo ya moto au ya uvuguvugu.

Maji ya kawaida (room temperature).

Soma hii pia > Vyakula vya asubuhi vya mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

1. Vyakula vya kusisimua

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula 1

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo.

Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, tomato sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo na kuongeza zaidi vidonda vya tumbo.

2. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula 2

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

3. MAZIWA Fresh

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula 3

Kwa miaka mingi watu wenye vidonda vya tumbo wamekuwa wakihimizwa kunywa maziwa kwa wingi kwa matumaini kwamba yanaponyesha vidonda vya tumbo.

Utafiti wa karibuni umebaini maziwa si salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Utafiti wa karibuni umebaini maziwa si salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo. Click To Tweet

Kwahiyo kama umekuwa ukinywa vikombe na vikombe vya maziwa kwa matumaini unajiponya vidonda vya tumbo habari hii haikuachi salama

Ndiyo ukinywa maziwa unaweza kusikia nafuu fulani kwa dakika kadhaa lakini baadaye hubadilika na kuwa mbaya zaidi
Ni vizuri zaidi kunywa maziwa mtindi kuliko maziwa freshi. Mtindi una bakteria wazuri mhimu kwa ajili ya tumbo na kinga ya mwili

Unajuwa imefika mahali watu hawaamini kama kuna dawa ya kuponya vidonda vya tumbo.

Wengine hawaamini kabisa kama huu ugonjwa unatibika. yaani ukiwaambia dawa ninayo kwa ajili hiyo wanasita sana na wanaanza kuona ni utapeli.

Lakini uchunguzi wangu umebaini wengi wanatumia dawa lakini hawajuwi wale nini na nini wasile. Vidonda vya tumbo ili upone siyo dawa hasa, mhimu ni kujua nini ule na nini usile kwa kipindi kirefu kisichopungua miezi 6.

Ukiwa makini kwenye vyakula na vinywaji ninakuhakikishia kupona vidonda vya tumbo bila shida yoyote kwa asilimia 100

Kwa sehemu kubwa vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi kuzidi tumboni kwa muda mrefu mfululizo bila wewe kujua. Kwa sababu hii kuendelea kunywa tena na tena maziwa katika siku kunapelekea kuundwa kwa hydrochloric acid ambayo ni chanzo pia cha vidonda vya tumbo.

Kuanzia leo punguza kabisa au ikiwezekana acha kabisa kunywa maziwa huku ukiendelea kutumia dawa na uone kama hutaona tofauti

4. Chumvi NYINGI

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula 4

.

Utafiti uliowahi kufanywa nchini marekani umeonyesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi nyingi na vidonda vya tumbo. Angalia nimeandika chumvi nyingi, hii inamaanisha si kwamba hutakiwi kutumia chumvi, hapana unahitaji chumvi kila siku bali isiwe nyingi sana.

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anashauriwa kuepuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi, HASA VYAKULA VYA KUSINDIKA AMBAVYO HUWEKWA CHUMVI NYINGI ili visiharibike haraka.

Pia jiupeshe na kuongeza chumvi mbichi kwenye chakula ambacho unakula.

Vitu vingine mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula au kunywa ni pamoja na sukari, vilevi vya aina yoyote, nanasi, karanga, maharage, dagaa, kuku wa kisasa, mayai ya kisasa, maandazi, nyama choma, wali wa pilau, wali mweupe unaweza kula mara 1 au mara 2 tu kwa wiki kumbe wali wa nazi unaweza kula hata kila siku.

Orodha hii itaendelea kuboreshwa.

Soma hii pia > Dawa ya vidonda vya tumbo

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula 5

.

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyue wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5. Zoezi hili linaondoa asidi mwilini haraka kuliko zoezi lingine lolote

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Mwisho jipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

Asidi ni sumu au takataka zilizomo ndani ya mwili zinazoweza kukuletea magonjwa na maumivu mbalimbali mwilini ikiwemo miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo na maumivu yoyote mwilini ambayo hayajaletwa na ajali au jeraha nje ya mwili

Pia ifahamike vyakula au vinywaji hivi haviruhusiwi kutumika kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ili kumuongezea kasi ya uponyaji wa ugonjwa wake ila kama wewe huumwi vidonda vya tumbo unaruhusiwa kuendelea kula na kunywa vinywaji hivi kwa raha zako.

Kama kuna chakula au kinywaji unatumia na huna uhakika ikiwa kinaruhusiwa kwako au hakiruhusiwi kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo kiandike hapo chini mimi nitakujibu.

Je unatafuta dawa ya asili ya kuponya vidonda vya tumbo? kama ndiyo nipigie simu 0714800175

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 12,525

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *